Moi University Journals
Not a member yet
    344 research outputs found

    Makosa ya Kiisimu katika Filamu Fasiriwa kwa Kiswahili kutoka Kiingereza: Tafsiri ya Utokeaji wa Sauti

    Get PDF
    Wataalamu mbalimbali kama Cintaz (1997); Luyken na wenzake, (1991) na Franco (2001) wanahukumu tafsiri ya utokeaji sauti kuwa tafsiri rahisi, thabiti, halisi na yenye kuaminika ambayo huzuia kiwango cha kutokuaminika kutoka mazungumzo asili. Hukumu kama hiyo inaleta ukakasi kutokana na mchakato wa tafsiri. Hali hiyo imesababisha kuchunguza makosa ya kiisimu ya tafsiri ya utokeaji sauti katika filamu fasiriwa kwa Kiswahili kutoka Kiingereza. Lengo la makala hii ni kubainisha makosa mbambali ya kiisimu pamoja na kujadili sababu ya utokeaji wa makosa hayo. Data za utafiti huu zimechambuliwa kutokana na modeli ya Nord (1991). Modeli ya Nord ilijihusisha na makosa manne ya tafsiri ya matini kama vile; makosa ya kiisimu, makosa ya kipragmatiki, makosa ya kiutamaduni na makosa ya matini mahsusi. Utafiti huu uliongozwa na mkabala wa kimaelezo. Data za utafiti zimekusanywa kwa kuangalia na kusikiliza CD tano. CD hizo ni pamoja na Skip Trace, Deleted, Real Steel, Behind the Enemy line na Tiger Cage. Kwa upande wa data za lengo la pili zilipatikana kwa njia ya uchambuzi wa makala tatu. Matokeo yameonesha kwamba makosa ya kisemantiki yamechukua nafasi kubwa ukilinganisha na makosa ya kisarufi na kileksikia. Aidha, mtafiti amebaini sababu mbalimbali zilizosababisha ufanywaji wa makosa ya filamu fasiriwa kama vile tofauti za kiutamaduni, raghba ya mfasiri, msisimko wa mchezo wenyewe, uchache wa maarifa na misamiati, athari za lugha mama, ukosefu wa taaluma ya tafsiri nakadhalika. Utafiti huu umetoa mchango wa kukuza taaluma ya tafsiri katika fani ya filamu. Vilevile, umetoa mapendekezo ambayo yatapunguza makosa ya tafsiri kwa wafasiri, wanataaluma na watafiti

    Challenges of Translating Conversational Implicatures from English to Kiswahili Using Computer Assisted Tools: A Case of "Google Translate"

    Get PDF
    In this study, we investigated challenges faced by computer assisted translation software with special focus on Google Translate, in translating conversational implicatures from English to Kiswahili. The data for this study were sourced from William Shakespeare\u27s play, “The Tragedy of Othello the Moor of Venice” which has been translated to Kiswahili as “Othello, Tanzia ya Mtu Mweusi.” The data was informed by Grice’s (1975) conversational implicature theory, and the relevance-theoretic translation approach as postulated by Gutt (1991). To evaluate the quality of Google Translatecomputer assisted translation system, we made a comparison of the computer translated output with the human translated text to ascertain to what extent the meaning of the conversational implicatures in the source language is preserved in the target text. We further examined challenges encountered by Google Translate in the process of translating conversational implicatures and suggested what could be done to improve Google Translate method to ensure accuracy in translating conversational implicatures. The results indicate that, there is inferior translation quality of the target text with ambiguous words and sentences. Also, it was observed that it is challenging to translate conversational implicatures using Google Translate because it has not been programmed to process aspects of source culture or adapt to the aspects of target culture thus cannot correctly translate conversational implicatures. Besides that, other challenges posed range from lexical, syntactic, and semantic to pragmatic mismatch

    Changamoto Zinazoathiri Matumizi ya Filamu za Kibongo zenye Tafsiri katika Ufundishaji wa Msamiati wa Kiswahili kwa Wageni

    Get PDF
    Makala haya yamechunguza changamoto zinazoathiri matumizi ya filamu za Kibongo zenye tafsiri katika ufundishaji wa msamiati wa Kiswahili kwa wageni nchini Tanzania. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Ujifunzaji kwa njia ya Media Anuwai ya Mayer (2009). Uchambuzi wa data za utafiti huu umetumia mkabala wa kitaamuli na mbinu ya kuchambua maudhui. Data za utafiti huu zilipatikana kutoka katika vituo vitatu vinavyofundisha Kiswahili kwa wageni ambavyo ni Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Kiswahili na Utamaduni (KIU) na Kituo cha Mafunzo ya Ushirikiano na Maendeleo ya Kimataifa (MS-TCDC). Data za makala haya ni sehemu ya data zilizokusanywa kwa ajili ya shahada ya umahiri[1] ya mwandishi wa makala haya akishirikiana na msimamizi wake ambaye ni mwandishi mwenza wa makala haya. Mbinu za usaili na ushuhudiaji zilitumika kukusanya data kutoka kwa walimu tisa wanaofundisha Kiswahili kwa wageni. Matokeo ya utafiti huu yameonesha changamoto mbalimbali zinazoathiri matumizi ya filamu za Kibongo zenye tafsiri katika ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni. Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa vitendeakazi, filamu kuchukua muda mwingi wa kipindi, filamu kuwa na makosa kwenye tafsiri zake, changamoto ya utamaduni, filamu kwenda kwa kasi, mtazamo hasi wa wanafunzi na changamoto ya umeme. Utafiti huu umependekeza kwamba vituo vinavyofundisha Kiswahili kwa wageni viboreshe mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.   [1] Kukamilika kwa shahada hiyo ni kutokana na ufadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Mchango wao tunautambua na kuuthamini sana

    Tofauti ya Kimiundo kati ya Vivumishi na Vibainishi katika Lugha ya Kiswahili kwa Mtazamo wa Eksibaa

    Get PDF
    Pamoja na wanasarufi wa lugha ya Kiswahili kukubaliana kuwapo kwa uainishaji wa vivumishi na vibainishi lakini kwa kiasi kikubwa, ukipitia kazi za wataalamu mbalimbali, dhana hizo zimekuwa zikichanganywa katika kapu moja la uainishaji katika lugha ya Kiswahili. Kwa mantiki hiyo, maneno ya vivumishi yameanishwa kama vibainishi na vibainishi kuainishwa kama vivumishi. Hivyo uainishaji wa vivumishi na vibainishi katika lugha ya Kiswahili umekuwa na dosari hasa katika uingizaji wa mifano ya maneno katika kategoria hizo. Maneno yaliyoelezwa kama vibainishi na wataalamu kama; Habwe na Karanja, (2004), Biber na wenzake (2005), Richards na wenzake (2010), Khamis (2011). Pia yameelezwa kama vivumishi na wataalamu wengine au wataalamu walewale. Maneno ya aina moja kutumika katika kategoria mbili tofauti, kumeleta ukinzani wa kiuchanganuzi hasa katika sintaksia ya lugha ya Kiswahili. Makala haya yamekusudia kubainisha tofauti ya kimiundo kati ya vivumishi na vibainishi kwa mtazamo wa Eksibaa, ili kuweka wazi tofauti kati ya vibainishi na vivumishi na kufanya uainishaji wa kategoria mbili hizi, kutoingiliana kama inavyojitokeza katika kazi za wataalamu. Makala haya yameweka wazi mwachano kati ya vivumishi na vibainishi kama kategoria mbili tofauti katika lugha ya Kiswahili

    Urudiaji wa Kisimulizi na wa Kisemantiki kama Mtindo katika Tenzi: Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi

    Get PDF
    Riwaya na tamthilia kama tanzu za fasihi ya Kiswahili ni mazao ya karne ya ishirini, tofauti na utenzi ambao uliandikwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1570. Sifa moja kuu tena ya kimsingi katika utanzu wa ushairi hasa utenzi ni matumizi ya urudiaji wa kisimulizi na ule wa kisemantiki. Sifa ya urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki ambayo ni wazi kabisa katika maisha ya binadamu ina utata wake unaotokea katika vipengele mbalimbali. Urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki hutokea katika viwango mbalimbali na vipengele hivyo ndivyo kiini cha fani na maudhui. Licha ya kazi na umuhimu wa urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki katika tenzi za Kiswahili, kwa uelewa wetu hakuna uhakiki wa kina ambao umefanywa katika vipengele hivi, licha ya utenzi kuchunguzwa sana. Yaliyomo ni mambo ya kijumla kuhusu urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki ambayo hayajaangazia majukumu na umuhimu huo. Kazi nyingi zimekosa kuhakiki kwa kina urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki kama mtindo katika ushairi. Kwa hivyo, katika makala haya, lengo letu limekuwa kujadili kwa kina urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki kama mtindo unaofanikisha fani na maudhui katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi

    Uchanganuzi wa Vigezo Vinavyotumika Kuwajenga Wahusika katika Ushairi wa Kiswahili

    Get PDF
    Makala hii imechunguza vigezo vilivyotumiwa kuwajenga wahusika katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii imetokana na madai ya tafiti kueleza kwamba mashairi mengi andishi hayana wahusika bali mashairi simulizi (Samwel, Selemani na Kabiero; 2013). Kutokana na madai hayo tuliona ipo haja kuchunguza vigezo vinavyotumika kuwajenga wahusika katika ushairi andishi wa Kiswahili pamoja na wahusika waliojengwa kupitia vigezo hivyo. Ili kutimiza azma ya makala hii, utafiti umefanywa kwa kurejelea diwani tatu, yaani Fungate ya Uhuru (1988), Wasakatonge (2003) na Vifaru Weusi (2016). Data za msingi za makala hii zilipatikana maktabani kwa mbinu ya usomaji matini na uchambuzi wa nyaraka. Kadhalika, katika makala hii Nadharia ya Uhalisia ndiyo iliyoongoza mchakato mzima wa uwasilishaji na uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti yaliyozaa makala hii yameonesha vigezo kama vile kigezo cha kitaswira, kigezo cha usimulizi, kigezo cha kifasihi simulizi na kigezo cha kiishara ndivyo vilivyotumiwa na mwandishi Seif Khatib kuwajenga wahusika katika diwani teule. Pia, makala hii imeonesha kila kigezo kilivyotumika kuwajenga wahusika katika ushairi wa Kiswahili kupitia diwani teule za makala hii. Makala hii inapendekeza kufanyika kwa tafiti nyingine katika fasihi andishi zitakazotofautisha na kulinganisha vigezo vinavyotumika kuwajenga wahusika wa ushairi na tanzu nyingine za fasihi andishi kama vile riwaya, tamthiliya na hadithi fupi

    Sera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili kati ya Miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania

    Get PDF
    Makala hii inachunguza jinsi sera ya lugha ya kipindi cha ukoloni ilivyochochea mabadiliko ya kimaudhui ya ushairi wa Kiswahili kati ya mwaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Kulingana na makala hii hali ni matukio mahsusi yanayoathiri ubunifu wa maudhui ya ushairi. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii imezingatia sera ya lugha ya kipindi cha utawala wa Wajerumani na Waingereza. Uchunguzi unazingatia mashairi teule kutoka diwani za watunzi wafuatao: Mathias Mnyampala, “Diwani ya Mnyampala (1965)”, Amri Abedi, “Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954)”,  Akilimali Snow-White, “Diwani ya Akilimali (1963)”, Shaaban Robert , “ Koja la Lugha (1969), Pambo la Lugha (1966), Kielezo cha Fasili (1968), na Masomo Yenye Adili (1967)”, na Saadani Kandoro, “Mashairi ya Saadani, (1966)”. Mashairi yaliyoteuliwa yanasomwa na kuhakikiwa ili kubainisha maudhui yaliyomo. Uchanganuzi wa data unaongozwa na mihimili ya Nadharia ya Utegemezi na Nadharia ya Ubidhaaishaji wa Lugha. Katika mashairi teule, inabainishwa namna washairi walivyotetea na kuinua hadhi ya lugha ya Kiswahili kwa kueleza sifa na umuhimu wake katika ushairi wao. Pia, inadhihirishwa jinsi ushairi uliotungwa kwa Kiswahili sanifu ulivyotumiwa kama chombo cha umma cha kujieleza kwa kupigania haki, usawa, na uhuru pamoja na kuwahimiza wananchi wakae kwa amani, udugu na heshima

    Mwachano wa Taratibu za Uundaji wa Istilahi za Kiswahili na Changamoto Zake katika Lugha: Mifano kutoka Istilahi za TATAKI na BAKITA

    Get PDF
    Suala la uundaji wa istilahi katika lugha limekuwa ni la muda mrefu, hivyo, linapaswa kuratibiwa kwa taratibu maalumu na za kudumu. Taratibu hizo zinapaswa kuwa bayana na zisizobadilika jambo linalotajwa kuchochea kudumishwa kwa nidhamu katika mchakato wa uundaji wa istilahi. Utafiti ulilenga kuchunguza mabadiliko katika taratibu mbalimbali za uundaji wa istilahi za lugha ya Kiswahili na changamoto zake katika istilahi zinazoundwa katika mazingira hayo. Taratibu zilihusisha: hatua za uundaji wa istilahi, miongozo inayotumika na ushirikishwaji wa wataalamu wa istilahi kutoka nchi nyingine zinazotumia lugha ya Kiswahili.  Data za utafiti zilikusanywa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, BAKITA na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. Mbinu ya usomaji nyaraka maktabani, hojaji na usaili zilitumika kupata data. Data zilikusanywa kwa kuongozwa na nadharia ya Jumla ya Istilahi na kujalizwa na nadharia ya Istilahi za Kisayansi na kuchanganuliwa kwa mkabala wa kitaamuli. Matokeo yamebainishwa kuwa; kila jopo lina hatua zinazofuatwa jambo linaloweza kuchochea kuundwa kwa istilahi zenye changamoto katika lugha. Pia matokeo yamebainishwa kuwa licha ya mwongozo wa BAKITA kuonekana una manufaa zaidi katika kuunda istilahi za Kiswahili, bado pamekuwa na matumizi ya kuchanganya miongozo. Matokeo yameeleza changamoto na mabadiliko yanayoukumba msisitizo unaotolewa na mwongozo wa ISO, hivyo, kuufanya ushindwe kutekelezeka kikamilifu. Kuhusu ushirikishwaji wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili kutoka nchi nyingine, imebainishwa kuwa ushirikishwaji umekuwa ukifanyika kwa kiwango kidogo na mara nyingine, nchi zinazoshirikishwa hubadilika takribani kila jopo. Matokeo yamehimiza haja ya kuwa na utaratibu maalumu, bayana na pangilifu katika kuunda istilahi za lugha. Pia, matokeo yamehimiza kuwapo kwa juhudi za pamoja za nchi watumiaji wa Kiswahili ili kukipa Kiswahili sura moja katika eneo lote kinamotumika na kuipunguzia lugha mzigo wa istilahi zenye sura ya kanda

    Sifa za Vitanzandimi vya Kiswahili katika Mawasiliano ya Jamii

    Get PDF
    Vitanzandimi ni nui muhimu ya fasihi simulizi. Nui hii ina mnasaba wa moja kwa moja na jamii kulingana na zama, itikadi pamoja na utamaduni wa jamii ikiwemo mila, dasturi, mtindo wa maisha, ufundi wa aina zote na kadhalika. Utanzu huu wa semi katika fasihi simulizi una kazi lukuki katika jamii, miongoni mwa kazi hizo ni kutoa motisha kwa wanafunzi kutamka maneno (Morris, 1975). Kadhalika, vitanzandimi huleta raha kwa watu kwa sababu ndani yake mna marudio ya sauti fulani ambazo huleta ladha ya kimuziki na hata pale msemaji anaposhindwa kuyatamka maneno hayo (Wanjala, 2011). Hata hivyo, vitanzandimi kama utanzu muhimu wa semi huiburudisha jamii hasa watoto (Wamitila, 2004). Licha ya umuhimu na kazi kubwa ifanywayo na vitanzandimi katika jamii, nui hii ya fasihi simulizi bado haijafafanuliwa kwa kiwango cha kutosha katika lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu ya kutoelezwa kwa uwazi sifa za maneno hayo (vitanzandimi) zaidi ya kudokezwa kijumla tu kupitia fasili zilizotolewa na wataalamu mbalimbali wa fasihi. Kadhalika, kumekuwa na utofauti na mwachano mkubwa wa mifano ya vitanzandimi kutokana na miegamo ya fasili za vitanzandimi zilizodokezwa na wataalamu mbalimbali wa fasihi. Kwani, baadhi ya wataalamu huamini kuwa vitanzandimi ni mchezo wa maneno, wengine huamini ni maneno yanayotatiza kimatamshi, na wengine wakiamini ni maneno yanayokaribiana sana kimaana na kisauti pale yanapotamkwa. Ingawa si jukumu wala lengo la makala yetu kushughulikia utofauti ama mwachano huo wa mifano ya vitanzandimi kutokana na miegamo hiyo ya fasili za vitanzandimi zilizodokezwa na wataalamu wa fasihi ‘la hasha’. Makala hii ilitia nanga katika kubainisha sifa zinazovitambulisha vitanzandimi vya Kiswahili katika mawasiliano ya jamii (watu). Hivyo, kupitia makala haya imebainika kuwa vitanzandimi vya Kiswahili vina sifa zake kadha wa kadha kutokana na uamilifu wake kwa jamii

    Ubainikaji wa Mahusiano na Mamlaka kupitia Usemi kwenye Nyumba za Watawa za Malezi

    Get PDF
    Utafiti huu unahusu kujieleza na ubainikaji wa mahusiano na mamlaka yanayowezeshwa kupitia matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye nyumba za watawa za malezi katika kanisa Katoliki nchini Kenya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Sarufi amilifu msonge ya Michael Halliday (1985). Data ya uchunguzi ya utafiti huu ilikusanywa kutoka nyanjani katika nyumba za malezi mjini Mombasa ambapo lugha ya Kiswahili hutumika kwa kiasi kikubwa na ni mojawapo ya lugha kuu za mawasiliano. Matini zilizoangaziwa zilikuwa katika kiwango cha kishazi na sentensi. Maswali matatu yaliyopaniwa kujibiwa na makala haya ni kwamba je, lugha hutumiwa vipi kati ya walezi na walelewa wakati wa kujieleza. Pili, je mamlaka hubainikaji vipi kwenye mawasiliano katika nyumba za watawa za malezi? Tatu je, mamlaka na mahusiano hudhihirika vipi katika matumizi ya lugha iliyo rasmi na isiyo rasmi katika nyumba za watawa za malezi? Matokeo ya utafiti yanatanaonyesha kuwa kujieleza na ubainikaji wa mahusiano na mamlaka yasiyo wazi kati ya walezi na walelewa hudhihirika katika usemi katika nyumba za watawa kupitia matumizi ya lugha ya Kiswahili

    145

    full texts

    344

    metadata records
    Updated in last 30 days.
    Moi University Journals
    Access Repository Dashboard
    Do you manage Open Research Online? Become a CORE Member to access insider analytics, issue reports and manage access to outputs from your repository in the CORE Repository Dashboard! 👇