Moi University Journals
Not a member yet
    344 research outputs found

    Ufemerali katika Nyimbo za Muziki wa Bongofleva nchini Tanzania: Mifano kutoka Nyimbo Teule

    No full text
    Makala haya yamechunguza ufemerali katika nyimbo za muziki wa Bongofleva nchini Tanzania, mifano kutoka katika nyimbo teule za wasanii wa muziki huu ambao nyimbo zao zimeonekana kuwa na ufemerali. Istilahi ufemerali iliyotumika katika Makala haya imetoholewa kutoka lugha ya Kiingereza katika neno “Ephemeral” likimaanisha hali ya kitu kupendwa sana, kuvuma na baada ya muda mfupi kitu hicho kuchuja na kupoteza mvuto au umaarufu wake. Nyimbo za muziki wa Bongofleva zinazotolewa na wasanii zina sifa ya ufemerali yaani pindi zinapotolewa hupedwa sana, huvuma na baada ya muda mfupi huchuja, kupoteza mvuto na umaarufu wake kwa wasikilizaji. Katika jamii ya Watanzania kumekuwa na hali ya vitu, matukio au mtu kuvuma katika muda fulani kisha kuchuja na kupoteza umaarufu wake kutokana na matukio yanayoambatana. Miongoni mwa mambo au matukio yanayoongoza kwa ujitokezaji huu ni pamoja na nyimbo za muziki wa Bongofleva. Data zilizotumika katika Makala haya zilipatikana kwa kutumia njia kuu mbili yaani usaili na ushuhudiaji. Katika Makala haya imebainishwa kuwa sifa ya ufemeralikatika nyimbo za muziki wa Bongofleva, ni kitendo cha kuvuma na kuchuja baada ya muda mfupi. Dhana ya ufemerali inahusisha kitendo cha nyimbo kupendwa, kuvuma na kisha baada ya muda mfupi nyimbo hizo kupoteza mvuto na umaarufu wake. Hivyo Makala haya yameonesha kuwa katika nyimbo za muziki wa Bongofleva imeonekana kuwa dhana ya mawanda mapana ya kupendwa na kuvuma inajitokeza zaidi katika nyimbo za muziki huu ikilinganishwa na aina nyingine ya nyimbo zinazoonekana kuendelea kupendwa licha ya kutungwa na kuimbwa miongo kadhaa iliyopita, mfano nyimbo za muziki wa dansi, maarufu kwa jina la zilipendwa. Ijapokuwa lengo la Makala haya sio kulinganisha nyimbo za muziki wa Bongofleva na nyimbo za muziki wa dansi, dhima ya Makala haya ni kuchunguza ufemerali katika nyimbo za muziki wa Bongofleva kwakumakinikia kuchunguza sababu za ufemerali katika nyimbo za wasanii teule

    Mwingiliano Matini kama Kunga ya Uandishi katika Riwaya za S.A Mohamed: "Dunia Yao" (2006) na "Nyuso za Mwanamke" (2010)

    Get PDF
    Makala haya yameshughulikia mwingilianomatini kama kunga ya uandishi katika riwaya mbili za S.A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010) zilizondikwa katika mwongo wa kwanza wa K21. Riwaya hizi zinaonekana kuwa changamano zikilinganishwa na riwaya za kimapokeo kwa kugeukia mtindo wa uandishi wa ubaadausasa. Makala haya yaliongozwa na nadharia ya ubaadausasa inayopendekeza uanuwai katika kueleza tajriba tofauti za binadamu.  Uchanganuzi ulibaini kuwa riwaya hizi zina matumizi mengi ya mwingilianomatini yaliyojikita katika matini mbalimbali zikiwemo za kifasihi, kidini, kihistoria na kifalsafa. Makala haya yamedhihirisha kuwa matumizi ya mwingilianomatini ni mbinu ya kiumbuji ambayo mwandishi ameitumia kuendeleza dhamira mbalimbali zinazoathiri ulimwengu katika K21. Hata hivyo imebainika kuwa riwaya hizi huenda zikaitenga hadhira isiyobobea katika fani mbalimbali za kijamii na aghalabu huleta ugumu wa kufuatilia dhamira mbalimbali zinazojitokeza katika kazi hizi

    The Problematics of Language Choice in The Kenyan Film: Lessons from \u27Nairobi Half Life\u27

    No full text
    The authenticity and originality of film is not only realised through settings and events but also through actor performance (characterization) in the representation of those events and experiences. This paper analyses how choice of language in film affects actor performance especially in the portrayal of a realistic and authentic characterization, and how this impacts the overall authenticity in the film Nairobi Half Life by David Gitonga. Employing selected tenets of the realist film theory espoused by Andre Bazin, Stanley Cavel, Rudolph Arneheim and Siegfried Kraucer, the paper undertakes a critical analysis of language and performance in the selected film and looks at how choice of language aids in the enactment of character that meets the threshold of being genuine, authentic and realistic – ‘reality’ and ‘authenticity’ being at the centre of a film’s quality. It interrogates how actor performance in the scenes is affected by the spoken language used by the actor in two ways; one, whether the language spoken corresponds to the actual language used in the real world and two, whether the language chosen fits the character’s physiognomy in bringing out a genuine rendition

    Utata baina ya Dhana za Unyambulishaji na Uambatizi katika Ufafanuzi wa Sarufi ya Kiswahili

    Get PDF
    Makala hii imelenga kuibua utata uliopo baina ya dhana za unyambulishaji na uambatizi katika mofolojia ya Kiswahili. Unyambulishaji na Uambatizi ni dhana zinazohusu michakato ya uundaji wa maneno. Mgawanyo wa dhana hizi ulifanywa kwa kutumia chujio la lugha za Ulaya ambazo mofolojia yake ni tofauti na mofolojia ya lugha za Kibantu (Kosch, 2011). Hivyo, dhana hizo zinapotumika katika ufafanuzi wa sarufi ya lugha za Kibantu, kikiwemo Kiswahili, hubua utata. Makala hii imebaini kwamba utata huo husababishwa na mambo matatu. Kwanza, ni suala la dhima za viambishi vya unyambulishaji na uambatizi kuingiliana. Pili, ni suala la nafasi ya viambishi vya unyambulishaji na uambatizi katika mzizi au shina la neno. Tatu, ni kuwepo kwa istilahi tofauti tofauti zinazotumiwa na wanaisimu wa Kiswahili kurejelea dhana hizo. Makala hii imefafanua mambo hayo kwa kina na kuonyesha namna yanavyosababisha utata baina ya dhana ya unyambulishaji na uambatizi

    Language and Gender Identity Marking in Litungu Music and Dance

    Get PDF
    As a social institution, music and dance can be viewed as sites for social action i.e. for the construction of social phenomenon, including identity (Malchiodi, 2006; Coleman, 2005; Leuthhold, 1998). Yet with respect to Litungu (lyre) music and dance (henceforth LMD) - among the Bukusu people of Western Kenya - research on how the litungu players, singers, and dancers (de)construct gendered identities is yet to be done. Litungu music is one of the traditionally male-dominated social institutions, yet - as a result of globalization - it is one of the sites that have received a lot of influence from other forms of music within and across other cultural groups. This raises the question as to whether LMD has changed or not, especially with respect to gender issues. Against this background, this paper takes a linguistic perspective to investigate the shifting Bukusu identity in the context of music and dance. Specifically, we investigate how language is used to construct gender identities in the context of LMD. Using a descriptive design, both primary and secondary data is analyzed using Fairclough’s (1995) approach to critical discourse analysis (CDA). The findings of this study form the basis for reflections on the nature and future of LMD on the one hand, and how language is used in the context of music and dance on the other hand

    Mchango wa Mbinu ya Familia Wenyeji katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni

    No full text
    Kijalizo na kiegesho ni viambajengo ambavyo vimeelezwa na wataalamu mbalimbali. Kijalizo kinaweza kurejelewa kama kiambajengo muhimu cha sentensi au kishazi ambacho huwa na kazi ya kukamilisha maelezo ya msingi katika neno, kirai au sentensi. Kiegesho ni kiambajengo kisichokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na maneno mengine kisintaksia bali hufanya kazi ya kutoa taarifa za ziada katika neno au kundi la maneno. Kwa hiyo vijalizo na viegesho ni vipashio muhimu katika kutoa taarifa za msingi na za ziada kuhusu sentensi. Maandiko ya wataalamu mbalimbali yamepelekea kuchanganywa kwa dhana hizi mbili, hasa katika kuvielezea vipashio hivyo katika utokeaji wake kinafasi katika sentensi za Kiswahili. Hii ni kwa sababu kuna wakati kijalizo huonekana kama kiegesho na wakati mwingine kiegesho ni kama kijalizo. Makala haya yakiongozwa na nadharia ya Eksibaa yamekusudia kubainisha zaidi kati ya kijalizo na kiegesho kwa kuchunguza makutano na mwachano wa vijalizo na viegesho katika sentensi za Kiswahili. Yaani wakati gani vipashio hivyo hujitokeza pamoja katika sentensi na wakati gani haviwezi kutokea pamoja katika sentensi. Imegundulika kuwa vipashio hivyo hukutana katika mfuatano wa miundo maalumu ya virai na huachana kulingana na  mifuatano hiyo maalumu  katika sentensi za Kiswahili kwa mkabala wa kimuundo

    Majina Fiche ya Asili Wanayopewa Watu na Uchanuzi wake wa maana katika Lugha na Semi za Kiswahili

    Get PDF
    Azma ya makala haya ni kuonesha jinsi majina majina ya asili yenye maanafiche wanayopewa watu yanavyochanuza maana tofauti katika lugha ya Kiswahili. Watu wa jamii mbalimbali wana desturi ya kuwapa watoto wao majina yenye maana iliyojificha kwa malengo maalumu. Malengo hayo yanaweza kutokana na mazingira au vigezo mbalimbali vinavyosababisha watu wa jamii zingine kuwapa watoto wao majina ya namna hiyo. Pamoja na ukweli huo, bado baadhi ya watu hawajaelewa sawasawa maana ya majina hayo katika Kiswahili. Hivyo basi katika makala haya tumejikita zaidi na kuangazia majina hayo yanatoa maana gani katika lugha ya Kiswahili na jinsi maana hizo zinavyoakisi semi mbalimbali za Kiswahili. Data za makala haya zilikusanywa uwandani kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili, mahojiano, udusuru wa nyaraka mbalimbali pamoja na kamusi ili kuapata maana ya majina hayo. Aidha, uchanganuzi wa data na uwasilishaji wake, ulitumia njia ya kitaamuli na wakati mwingine data zilichambuliwa kitakwimu. Zaidi ya hayo nadharia ya semiotiki ilitumika kuogoza uchanganuzi wa data za makala haya

    Mchango wa Tafsiri za J.K. Nyerere katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili

    Get PDF
    Makala hii inatathmini mchango wa tafsiri za J.K. Nyerere katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili ili kuona ni kwa kiasi gani kazi zake za tafsiri zimeweza kukuza na kuendeleza fasihi ya Kiswahili. Kwa maneno mengine, makala hii inaonesha jinsi kazi za tafsiri za J.K Nyerere zilivyochangia maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. Ili kufikia lengo hilo, makala hii inatumia data kutoka katika vitabu viwili vya tafsiri ambavyo ni Julius Kaizari (1963) na Mabepari wa Venisi (1969) vya mwandishi Shakespeare vilivyotafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili. Data za makala hii zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini. Uchambuzi, uwasilishaji wa data na mjadala wa matokeo ya uchunguzi umeongozwa na Nadharia ya Skopos ya Hans J. Vermeer (1970). Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa kazi za tafsiri zimetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili kifani na kimaudhui. Kwa sababu kazi hizo zimeitajirisha fasihi ya Kiswahili, kuibua msamiati, mbinu za kisanaa, mtindo, misemo, kuchagiza utunzi wa tamthiliya na maendeleo ya dhamira katika fasihi ya Kiswahili. Kwa ujumla, tunaweza kusema kuwa kazi za tafsiri za J.K. Nyerere zimechangia kwa kiasi kikubwa kukuza na kuendeleza fasihi ya Kiswahili sio tu nchini Tanzania bali duniani kote

    Mental Health and Minority Status: A Reading of William Faulkner’s "A Rose for Family"

    Get PDF
    This paper undertakes a postmodernist reading of William Faulkner’s ‘A Rose for Emily’. It imbibes the binary notion of order versus chaos to interrogate the seeming madness of the main character in the story. The aim is to demonstrate how Emily, being a minority in her community, battles with mental or psychological challenges, which are products of her environment. The study relies on a close reading of the short story, and deploys postmodernism as a theoretical basis. In this paper, we argue that, the main character, Emily represents the minority in society. She is mentally unhinged (mad) because of the tragedies she has gone through. She is also a social recluse. Besides, she is a woman. To top it all, she is a criminal, a murderer. Faulkner thus uses Emily to give voice to the socially awkward or eccentric individuals. As we read the story, we begin to see that her madness is not random. It is a product of a larger society that has gone rogue. Emily is a product of the maltreatment and segregation she has suffered from a society that refuses to accept her. She embodies well Francis Imbuga’s (1987) statement: “When the madness of an entire nation disturbs a solitary mind, it is not enough to say that the man [or woman] is mad.

    Usawiri wa Mhusika Ngoromiko katika Ngano na Masimulizi ya Kijamii: Mifano kutoka Vijiji vya Kware na Kwasadala

    Get PDF
    Makala hii inachunguza usawiri wa mhusika Ngoromiko katika Ngano za Kichaga. Kwa jumla, mhusika Ngoromiko ni mhusika wa kufikirika anayepatikana katika ngano na masimulizi ya kijamii katika vijiji vya Kware na Kwasadala vilivyopo wilaya ya Hai-Kilimanjaro. Utafiti uliofanywa uliongozwa na malengo mawili ambayo ni kubainisha usawiri wa mhusika Ngoromiko kupitia ngano na masimulizi ya kijamii kutoka vijiji teule na, pili, kubainisha dhamira zinazowasilishwa na mhusika Ngoromiko. Mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji ilitumika katika ukusanyaji wa data. Watafitiwa ishirini walihusika katika utafiti huu. Nadharia ya Uhalisiajabu ilitumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data. Kwa jumla, matokeo ya utafiti yanaonesha mhusika Ngoromiko amesawiriwa katika namna ya kutisha na kuogopesha na kuwa ana jicho moja, mguu mmoja na kuwa na makazi katika maeneo yenye kutisha. Vilevile, mhusika huyu amehusishwa na dhamira mbalimbali kama vile chuki, vitisho, vimbwanga vya usiku, ufantasia na kupinga usasa na kuumbatia ukale

    145

    full texts

    344

    metadata records
    Updated in last 30 days.
    Moi University Journals
    Access Repository Dashboard
    Do you manage Open Research Online? Become a CORE Member to access insider analytics, issue reports and manage access to outputs from your repository in the CORE Repository Dashboard! 👇