Moi University Journals
Not a member yet
    344 research outputs found

    Community Perception and Attitudes Towards Tourism Development in Rimoi National Reserve, Kenya

    Get PDF
    Tourism development in Rimoi National Reserve has been expanding, yet little research has examined how local community perceive its impacts and how these perceptions influence their attitudes towards tourism development. This study aims to address this gap by examining the perceptions and attitudes of residents towards tourism development in the reserve. The study employed a Mixed Methods approach within a pragmatic paradigm and a convergent research design. The target population consisted of 548 household heads in the Rimoi community. The sample size included 231 household heads selected using systematic random sampling, and 10 resident youths selected through purposive sampling. Data was collected using survey questionnaire and a focus group discussion. Quantitative data was analyzed using frequency tables, percentages, means, standard deviations, and hierarchical multiple linear regression, while qualitative data was analyzed thematically. Quantitative findings showed that tourism\u27s economic (β =.148, p<.05) and socio-cultural impacts (β =.452, p<.05) positively influence community attitudes toward tourism development. However, environmental impacts have a negative effect (β = -.126, p<.05). Qualitative findings revealed that residents had mixed attitudes toward tourism development in Rimoi National Reserve, appreciating its economic benefits like job creation but fearing environmental harm and unequal gains. While some embraced cultural exchange, others were concerned about tradition loss and social inequalities. The study concludes that economic, environmental and social-cultural tourism impacts have a significant impact on community attitudes towards tourism development. The study recommends the development of sustainable tourism initiatives that prioritize economic benefits and community well-being, implementation of environmental conservation programs, and promotion of socio-cultural exchange and understanding between tourists and the local community. The results of this study have invaluable implications for policy and tourism management and practice in the development of targeted interventions for sustainable tourism development.

    Mitazamo ya Waafrika kuhusu Urithishwaji wa Mali: Uchunguzi wa Bunilizi za Kiswahili

    Get PDF
    Kurithisha mali katika jamii nyingi za Kiafrika ni suala linalohifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii. Hivyo, thamani ya mwanadamu katika ulimwengu wake hubainika pia kupitia mali anazorithisha wengine. Vilevile, kupitia mali hizo, mrithishaji anaendelea kuishi katika fikra za wanaorithishwa hata baada ya kifo chake. Kwa msingi huo, urithishwaji wa mali ni hazina inayoendeleza kizazi na kuleta kumbukumbu idumuyo katika ulimwengu halisi wa mwanadamu. Fasihi ni akiso la maisha ya mwanadamu katika mazingira yake halisi. Kwa mantiki hiyo, bunilizi za Kiswahili huhifadhi na kudokeza misingi mbalimbali inayozingatiwa katika kuendesha maisha ya jamii. Mathalani, ile inayohusu suala la urithishwaji wa mali kupitia wahusika wanaosukwa kwa ustadi unaokidhi haja ya kufikisha maudhui lengwa. Hata hivyo, haijaelezwa bayana mitazamo ya Waafrika kuhusu suala la urithishwaji wa mali kwa kuhusianisha na bunilizi za Kiswahili. Hivyo basi, makala hii imeshughulikia jambo hilo kwa kujiegemeza katika riwaya za Rosa Mistika (1971) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975). Makala hii ni matokeo ya data zilizopatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji. Vilevile, katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo hayo, misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi imetumika. Matokeo yanaonesha kuwa katika suala la urithishwaji wa mali kwa Waafrika, kuna mitazamo mbalimbali inayozingatiwa. Makala hii inajadili mitazamo mikuu mitatu, ambayo ni: mtazamo wa kitamaduni, kihiari, na kimabavu

    Sababu za Mkengeuko wa Malezi kwa Wahusika katika Riwaya ya \u27Rosa Mistika\u27

    No full text
    Ingawa wahusika hukengeuka malezi, wataalamu na wachambuzi hutofautiana katika kuelezea jambo hili. Wapo wanaoona kuwa, kukiuka malezi kwa wahusika katika kazi za fasihi kunasababishwa na wazazi au walezi (Wanjala, 2015; Mbatiah, 2016; Doepke na Zilibotti, 2019). Kwa upande mwingine, wapo wataalamu wanaowatupia lawama watoto kuwa wanabadilika hasa wanapotoka mikononi mwa wazazi na kuingia katika jamii kutokana na kushindwa au kupuuza malezi na maelekezo kutoka kwa wazazi au walezi wao (Ondieki, 2015; Jonas, 2017). Aidha, upande mwingine jamii hulaumiwa kwa kushindwa kuendeleza malezi yanayofaa kutoka kwa wazazi au walezi wa watoto (Mitchell, 2010; Martin, 2017; Sanga, 2018). Tofauti hizi za kimtazamo ndizo zilizosukuma kuandikwa kwa makala hii. Kwa hivyo, makala hii inakusudia kujadili sababu za mkengeuko wa malezi kwa wahusika kwa kutumia riwaya ya Rosa Mistika (Kezilahabi, 1971)

    Unsung Hero(ine)ism in the Making of a Nation: A Reading of Muthoni Likimani’s "Fighting Without Ceasing"

    Get PDF
    This article delves into the exploration of unsung Hero(ine)ism, with particular focus on the role of heroines, in the context of nation-building through an in-depth analysis of Muthoni Likimani\u27s work, Fighting Without Ceasing. Likimani\u27s self-narrative serves as a rich source for understanding the often-overlooked contributions of individuals in shaping a nation\u27s destiny. We uncover and elucidate the unsung heroine(s) portrayed in the text, shedding light on their pivotal roles in the making of a nation. Through a close reading of Likimani\u27s autobiography, the paper unveils the nuanced facets of Hero(ine)ism, emphasizing the multifaceted efforts that go beyond conventional narratives. It underscores the importance of recognizing and acknowledging these unsung heroines as integral contributors to the collective story of nationhood, thereby enriching our understanding of the complex dynamics involved in the formation of a nation

    Mwanamke Dhidi ya Uanauke Wake katika Karne ya 21

    No full text
    Nafasi ya watunzi wa ushairi wanawake, katika ushairi wa Kiswahili inaendelea kukua kwa kiasi kikubwa. Mwanamke baada ya kuchorwa katika kazi mbalimbali za kifashi kwa mtazamo duni na watunzi wa kiume anawajibu wa kujitetea yeye mwenyewe. Makala haya yanalenga kutathmini mtazamo wa mshairi mwanamke juu ya mambo mbalimbali yanayomzunguka mwanamke katika maisha yake ya kila siku. Data za makala haya zilipatikana katika diwani ya Kurunzi ya mwandishi Rose Mbijima kwa mbinu ya usomaji makini. Matokeo yanaonesha kuwa mwanamke anapiga hatua kujiodoa kuwa mtu wa hadhi ya chini, kama ambavyo anachorwa katika kazi nyingi za kifasihi. Hata hivvyo, data zinaonesha kuwa Mwandishi Rose Mbijima anaendelea kumchora mwanamke kwa mtazamo hasi na wakimapokeo zaidi kuliko alivyomfunua kwa matazamo wa kisasa na chaya. Data zinadhihirisha kuwa yapo mambo kuhusu mapenzi na ndoa ambayo mtunzi anamtazamo wa kimapokeo kama zilivyo jamii nyingi za kiafrika. Aidha, kuhusu mtazamo chanya na wakimapinduzi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii yake, mwanamke ameonekana akipaza sauti na kutoa maoni yake. Makala haya, yanahitimisha kwa kutoa mapendekezo kuwa, watunzi wa kike wa ushairi wapewe majukwaa mengi zaidi ili waweze kuwasilisha kazi zao, hali ambayo itaendelea kuchochea mabadiliko makubwa ya wanawake juu ya mtazamo wao kuhusu uanauke wao na jamii kwa ujumla kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii

    Lugha kama Nyenzo Inayotumiwa na Viongozi ili Kutimiza Malengo Yao Nchini Tanzania na Kenya

    No full text
    Viongozi ni watu wanaoongoza watu au kikundi fulani cha watu. Viongozi hutumia mbinu za ushawishi ili kuwafanya watu wanaowaongoza kuelewa, kuamini na kisha kutekeleza jambo ili kutimiza malengo yao katika taasisi, shirika au nchi. Ili kushawishi watu kuelewa, kuamini na kutekeleza jambo, viongozi hutumia nyenzo mbalimbali zikiwamo rasilimali fedha, rasilimali watu, rasilimali muda, mikakati, mipango pamoja na lugha. Hivyo, makala haya yanahusu lugha kama nyenzo inayotumiwa na viongozi ili kutimiza malengo yao nchini Tanzania na Kenya. Malengo yake ni kudadavua aina ya lugha ya ushawishi inayotumiwa na viongozi pamoja na kueleza namna lugha hiyo inavyoshawishi wananchi ili kutimiza malengo ya viongozi. Data zilizotumika zilikusanywa kwa njia ya uchambuzi matini pamoja usaili. Data hizo zimechambuliwa kimaelezo na kisha kufasiliwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Balagha ya Aristotle (367). Baada ya kufasili data hizo, matokeo yanaonesha kwamba aina ya lugha ya ushawishi inayotumiwa na viongozi ni hii ifuatayo: matumizi ya nafsi ya kwanza wingi, kaulimbiu, maneno ya kilugha, nahau/tamathali za semi/misemo, istilahi rasmi, lugha isiyo rasmi, takwimu, sifa faafu za kiarudhi, lugha ya kujiamini, lugha ya kujali na lugha ya motisha. Imebainika pia kwamba aina hii ya lugha hutumiwa kushawishi wananchi kwa kujinasibisha, kuaminisha, kuhamasisha, kutumainisha, kuunganisha na kuongeza motisha. Kutokana na matokeo haya, imehitimishwa kwamba lugha ni nyenzo ya ushawishi ambayo inafanya kazi kama nyenzo nyingine zinazotumika ili kufikia malengo ya uongozi nchini Tanzania na Kenya

    Mchango wa Mbinu ya Familia Wenyeji katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni

    Get PDF
    Familia Wenyeji ni moja kati ya mbinu mashuhuri zinazotumika katika ufundishaji wa lugha za kigeni kwa kuzingatia ufundishaji kimawasiliano. Tafiti mbalimbali zimeonesha umuhimu na ufaafu wa mbinu hii katika maendeleo ya ujifunzaji lugha kwa wajifunzaji wa lugha ya kigeni. Licha ya kuwepo uhusiano kati ya mbinu hii na ufundishaji na ujifunzaji wa lugha darasani, tafiti hizo hazikuonesha mchango wa matumizi ya mbinu hiyo katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kigeni darasani. Makala hii imebainisha mchango wa mbinu hiyo katika ufundishaji na ujifunzaji wa darasani wa Kiswahili kama lugha ya kigeni kwa kuchunguza ni kwa namna gani walimu na wajifunzaji wanatumia familia wenyeji kama mbinu ya kufanikisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji wa darasani. Data za makala hii zimetokana na mahojiano yaliyofanyika kwa kuhusisha walimu wa Kiswahili kwa wageni, wajifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni na waratibu wa familia wenyeji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MS TCDC) na kuchambuliwa kwa mkabala wa kimaelezo na kuongozwa na Nadharia ya Umahiri wa Kimawasiliano na Tamaduni Mchanganyiko ya Hall (1992). Matokeo ya utafiti yaliyojadiliwa katika makala hii yameonesha upo mchango wa matumizi ya mbinu hii katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni darasani

    Nafasi ya Lugha za Kiasili katika Mchakato wa Kutoa Huduma za Matibabu: Mifano kutoka Tumbatu na Kojani, Visiwani Zanzibar

    Get PDF
    Zanzibar ina jamii ambayo ndani yake mna jamiilugha ndogondogo. Ingawa lugha kuu ya mawasiliano ni Kiswahili, matumizi ya lahaja kama lugha za kijamii yanabainika kwa kiasi kikubwa katika jamiilugha zilizo mahususi. Matumizi ya lugha za kijamii yana mchango mkubwa katika kufanikisha mawasiliano baina ya watu wa jamiilugha. Lengo la makala haya ni kubainisha umuhimu wa lugha za kijamii katika huduma za afya pamoja na athari za kutozingatiwa lugha za kijamii katika huduma za afya, huku mtafiti akirejelea jamiilugha mahususi za Zanzibar. Kwa hiyo, makala yaligundua umuhimu wa lugha za kijamii kama vile elimu ya afya kuwafikia walengwa kwa urahisi, kufanikisha mawasiliano baina ya mtoa huduma na mpokea huduma za afya, n.k. Aidha, makala yanaelezea athari zinazojitokeza katika huduma za afya ambazo chanzo chake ni kutozingatia lugha ya mawasiliano ya jamii husika. Athari hizo ni kama vile woga wa kujieleza kwa upande wa mgonjwa, muuguzaji na hata mtabibu, ambapo huchangia kutopata tiba stahiki, n.k

    Mchomozo wa Usitiari katika Lakabu za Watu Mashuhuri na Maarufu nchini Tanzania

    Get PDF
    Makala haya yanachunguza mchomozo wa usitiari katika lakabu za watu mashuhuri na maarufu nchini Tanzania. Lakabu ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipa kutokyana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au kimatendo (Mulokozi, 2019). Majina haya ni maneno au mafungu ya maneno yenye maana iliyofumbatwa. Mara nyingi maneno au mafungu ya maneno hayo huwa na mchomozo wa usitiari ndani yake. Data ya makala haya kwa kiasi kikubwa imekusanywa maktabani kwa mbinu ya usomaji makini na kwa kiasi fulani uwandani kwa kuwasaili wanajamii kuhusu mchomozo wa usitiari katika lakabu hizo. Uchambuzi na uchanganuzi wa data umeongozwa na nadharia ya Jumuishi ya (Giles, 1979) na Nadharia ya Semiotiki (Saussure, 1976). Matokeo ya yanaonesha kuwa lakabu za watu mashuhuri na maarufu ni za kisitiari na zinabeba maana na ujumbe kuhusu ukweli ndani ya jamii husika. Hivyo, mchomozo wa usitiari unaojitokeza katika lakabu hizo unaibua dhamira za kisiasa, kijamii, kimajigambo na kiutamaduni. Kwa ujumla, uchunguzi wa makala unadhihirisha kuwa maumbile ya kimwili, nasaba na tabia au matendo ya mhusika vina nafasi kubwa katika utoaji wa lakabu za watu mashuhuri na maarufu katika jamii ya Watanzania

    Usawiri wa Nguvu-uhai katika Jamii za Kiafrika: Mifano Kutoka katika Riwaya ya "Mzishi wa Baba Ana Radhi"

    Get PDF
    Nguvu-uhai ni kipengele muhimu katika falsafa ya maisha ya Waafrika na kitu muhimu kinachofanya tajiriba za Waafrika. Msukumo wa kuchunguza Nguvu-uhai katika jamii za Kiafrika kupitia riwaya ya Kiswahili unatokana na kuwapo kwa madai kuwa msingi wa jamii za Kiafrika kuamini kuwa viumbe vyote vina roho au uhai haukidhi kanuni za kimantiki na umepitwa na wakati (Smith, 1961).  Hii ina maana kuwa Nguvu-uhai huchukuliwa kwa mitazamo tofauti kutegemeana na tajiriba na imani za kijamii.  Kutokana na tofauti hizo za kimtazamo, tuliona ipo haja ya kuchunguza Nguvu-uhai katika jamii za Kiafrika ili kubainisha ujitokezaji wake katika riwaya za Kiswahili. Ili kutimiza azma hiyo ya utafiti huu riwaya ya Mzishi wa Baba Ana Radhi ilirejelewa. Data kutoka maktabani zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uhakiki wa riwaya teule. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Kwa kutumia mkabala wa kitaamuli data zilichambuliwa, zilichakatwa na kuwasilishwa. Matokeo yanaonesha kwamba Nguvu-uhai ni dhana pana katika jamii za Kiafrika na hugusa nyanja zote za maisha yao.  Baadhi ya nyanja hizo ni kama vile na mila na desturi, maadili, afya ya jamii na uzazi. Kupitia vipengele hivyo maudhui mbalimbali kuhusu Waafrika huelezwa

    145

    full texts

    344

    metadata records
    Updated in last 30 days.
    Moi University Journals
    Access Repository Dashboard
    Do you manage Open Research Online? Become a CORE Member to access insider analytics, issue reports and manage access to outputs from your repository in the CORE Repository Dashboard! 👇