Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Uchanganuzi wa Makosa ya Kitahajia katika Mawasiliano Andishi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu: Mifano kutoka Chuo Kikuu cha St John’s cha Tanzania
Maandishi ya wanafunzi ni njia muhimu ya kuwasilisha hoja zao chuoni hususan katika masuala yanayohusiana na utahini. Utokeaji wa makosa katika kazi za wanafunzi ni jambo ambalo hupelekea kuvurugika kwa mawasiliano na wakati mwingine hata huwafanya wapate alama za chini wanapotahiniwa. Ingawa kuna tafiti nyingi ambazo zimefanywa kuhusu utokeaji wa makosa katika maandishi ya wanafunzi, makosa katika maandishi ya wanafunzi wa vyuo vikuu hayajaangaziwa sana. Ni kutokana na hali hii ambapo makala haya yanalenga kutambulisha na kuainisha makosa ya kitahajia yanayojitokeza katika mawasiliano andishi ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kupendekeza mbinu zinazoweza kutumiwa ili kupunguza utokeaji wake. Data imekusanywa kutokana na mawasiliano andishi ya wanafunzi katika mawasilisho ya semina na mijarabu ya darasani. Wanafunzi waliohusishwa kama watafitiwa ni wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu. Uchanganuzi wa data umefanywa kwa njia ya kimaelezo huku vitengo vikuu vya makosa ya kitahajia vikiwekwa wazi. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa muhimu kwa walimu wa Kiswahili kwa kuwa yatatoa mwongozo wa kuwasaidia katika kutambulisha na kuainisha makosa ya kitahajia ya wanafunzi kama njia muhimu ya kuzua mikakati ya kupunguza utokeaji wa makosa katika mawasiliano andishi ya wanafunzi wao. Aidha, wanafunzi watapata maelekezo kuhusu mbinu za kutumia ili kuboresha uandishi wao kwa kuepuka makosa anuwai yanayochanganuliwa katika makala haya. Kwa usomi wa Kiswahili, makala itachangia kuweka misingi ya uchanganuzi wa makosa anuwai yanayojitokeza katika matumizi ya Kiswahili
Mikakati ya Upishaji na Unyakuzi wa Zamu katika Mawasiliano ya Facebook
Upishanaji zamu ni mkakati maarufu katika mawasiliano ya ana kwa ana. Hii ni miafaka ambayo hutawala mawasiliano na kuwasaidia wazungumzaji kuwasiliana bila kuwepo kwa mizozo ya kizamu. Facebook, hata hivyo, ni mtandao unaotawaliwa na mawasiliano ya kimaandishi. Ingawaje ni hivyo, mawasiliano hayo huwa ya kimajibizano kama yale ya mazungumzo ya ana kwa ana. Uatafiti huu unatalii mawasiliano ya Facebook na kuchanganua mbinu za marafiki za kupishana zamu ya mawasiliano. Matokeo yake yatasaidia kutoa fahamisho la viashiria vya mwisho na mwanzo wa tamko katika mawasiliano ya Facebook ikikumbukwa kwamba mawasiliano ya Facebook ni ya kimaandishi japo yana sifa za mazungumzo ya ana kwa ana
Metaphorical Extension of Kiswahili Tense: An Application of Conceptual Metaphor Theory
This paper takes a metaphorical analysis of the Kiswahili tense. The metaphorical mapping processes of the past tense, the present tense and the future tense are interrogated to investigate how these tenses reflect the universal cognitive mechanism of human beings, that is, how learners acquire knowledge from known to unknown. Tense is a grammatical category of Kiswahili verb, and the verb form is used to express these time distinctions. The Kiswahili verb has three tenses; the future tense, the present tense and the past tense
Ubadilishaji Msimbo kama Mbinu ya Upole Chana katika Vipindi vya \u27Sobetab Kapchi\u27 kwenye Idhaa ya KASS FM
Makala haya yanahusu nafasi ya ubadilishaji msimbo kama mbinu ya upolekatika vipindi vya Sobetab Kapchi (SK) katika idhaa ya KASS FM. Utafiti uliongozwa na maswali mawili: je, wahusika katika vipindi vya SK wanachopeka maneno ya Kiswahili kwenye mazungumzo yao? Je, huku kubadilisha msimbo kunatokea katika hali zipi? Aidha, utafiti ulielekezwa na Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1987), hasa kipengele cha kuokoa uso. Vipindi vinne vya mazungumzo ya SK vilinaswa. Data zilizohusiana na upole kutoka kwa vipindi husika zilinakiliwa na kuchanganuliwa. Baadhi ya data zilinukuliwa moja kwa moja na zingine zilifupishwa kutegemea urefu wa data. Ilibainika kuwa, wasemaji wa Kinandi katika mazungumzo ya SK huchopeka maneno ya Kiswahili kwenye mazungumzo yao. Aidha, UM hutokea wakati wasemaji wanafikiria kuwa neno la Kinandi linaweza kutishia nyuso za wahusika wa mazungumzo
Mitandao ya Kijamii na Mabadiliko ya Kiswahili katika Karne ya Ishirini na Moja
Wanafalsafa wa kale walidai kuwa, duniani, hakuna kitu ambacho hakikosi kubadilika. Mojawapo ya vitu vinavyobadilika ni lugha. Lugha za binadamu hubadilika katika kila kizazi kwa sababu mbalimbali za kiisimujamii na kiteknolojia. Kwa kuwa lugha za binadamu ni kitu changamano, mabadiliko yake hutokea kwa matawi ya kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia, kisemantiki na kipragmatiki. Kuna sauti ambazo hutoweka katika lugha, na zingine hukopwa. Maana za leksimu hupanuka au hufinyika kutegemea matumizi yake kimuktadha. Kwa njia hii, mawasiliano ya binadamu huathirika kwani mabadiliko ya lugha hubadilisha mawasiliano na jinsi washiriki wanavyofasiri maana za kauli. Utafiti huu ulichunguza mabadiliko ya lugha ya Kiswahili mintarafu mitandao ya kijamii. Hii ni kwa sababu mojawapo ya vitu vinavyosababisha lugha kubadilika katika karne ya 21 ni teknolojia
Challenges of Translating Creative Literature from English into Kiswahili
The translation of the classical 18th and 19th century Swahili poetry into English was an important step in disseminating this art-form to a global audience way beyond the African continent. Not only did this translation and adaptation of the classical poetry lead to the translation of Swahili prose in early 20th century but also offer useful insights into the nature of Swahili poetry in general. But, what was the criteria used in selecting the poetry works to be translated? The paper which is guided by the tenets of the Equivalence theory as expounded by Xie (2014) briefly looks at the major arguments for and against this theory in achieving meaning equivalence between SL and TL. In doing this, it explores the style and language of a number of classical Swahili poems and concludes that although it is difficult, if not impossible, to achieve a perfect equivalence in translating a rigid form such as poetry, varieties in translations are an asset rather than a liability. Secondly, since poetry is a means of expressing personal or national ideology, feelings and attitudes, its translation acts as a bridging tool through which different cultures can get closer. This is best exemplified in case of the translated Swahili classical poetry
Uchanganuzi Linganishi wa Suala la Maadili kwa Vijana wa Kiume katika Tenzi Mbili: \u27Siraji\u27 na \u27Adili\u27
Makala hii imeshughulikia maadili kwa vijana wa kiume yanayojitokeza katika tenzi za Siraji na Adili. Katika uchunguzi huu tumeongozwa na nadharia ya maadili ambayo inalenga kazi za fasihi kutatua matatizo ya jamii kwa njia ipasavyo na kujenga jamii bora yenye maelewano. Malengo ya uchunguzi wetu ni kulinganisha jinsi ambavyo watunzi Kijumwa na Robert wamelishughulikia suala la maadili kwa vijana wa kiume katika tenzi Siraji na Adili na hatimaye kubaini sababu za kuwiana kwao. Baada ya kusoma na kuzichambua tenzi- Siraji na Adili tumebaini ya kwamba watunzi Kijumwa na Robert wamewiana kwa jinsi wamelishughulikia suala la maadili kwa vijana wa kiume. Tumeweza kuonyesha kwamba tenzi hizi zina uhusiano wa karibu sana kwa sababu watunzi Kijumwa na Robert wameyafungamanisha maadili hayo na mafunzo ya dini ya Kiislamu ndiposa tukachanganua data yetu kwa njia ya maelezo na ufafanuzi huku tukitoa thibitisho kutoka kwa tenzi- Siraji na Adili pamoja na Kurani Takatifu. Ni matumaini yetu kwamba makala haya yatachangia pakubwa katika taaluma ya kiusomi kwa kuendeleza fasihi andishi
Kiswahili na Sera ya Elimu katika Shule za Sekondari Nchini Kenya
Makala haya yanachunguza matatizo yanayowakumba walimu katika utekelezaji wa silabasi ya sasa ya Kiswahili. Utafiti ulifanywa katika Kaunti ya Kakamega, Mkoa wa Magharibi nchini Kenya. Sampuli ya watafitiwa iliteuliwa kwa kutumia mbinu za utabakishaji, uwiano na njia nasibu sahili. Walimu 70 na walimu wakuu 43 walishiriki katika utafiti. Afisa wa Usanifu wa Viwango vya Elimu mmoja na Mkuza mitalaa mmoja katika Taasisi ya Elimu Kenya walishiriki kama watafitiwa maalumu. Nyenzo za ukusanyaji data ambazo zilitumiwa ni hojaji, mwongozo wa masaili na mwongozo wa uchunzaji. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uwezeshaji ya Carl Rodgers. Utafiti uligundua kwamba utekelezaji wa silabasi ya sasa ya Kiswahili unakumbwa na matatizo mbalimbali. Sababu za hali hii ni kuwa, walimu hawakuandaliwa mapema kabla ya kuanzishwa kwa silabasi hii na wengi katika vyuo hawakujifunza baadhi ya mada katika silabasi ya sasa ya Kiswahili. Walimu, vile vile, hawaandaliwi mafunzo nyanjani na walimu hawajiandai vyema kitaaluma. Ili walimu waweze kufaulisha utekelezaji wa silabasi, utafiti umependekeza kuwa, Taasisi ya Elimu ya Kenya iandae semina kadhaa kwa walimu Kauntini ili masuala nyeti katika silabasi yafafanuliwe. Wizara ya Elimu yafaa itenge fedha za kufadhili mafunzo kwa walimu kwa Kiswahili nyanjani pamoja na usimamizi. Aidha, vyuo vinavyoandaa walimu wa shule za upili vitilie maanani mada ambazo zinajumuishwa katika mitalaa ya shule za upili. Mwisho walimu wazingatie maadili ya kazi yao
Nafasi ya Nadharia ya Mwingilianotanzu katika Uhakiki wa Fasihi
Nadharia ya Mwingilianotanzu inashikilia kuwa, kazi yoyote ya fasihi hujengwa kwa kuvunja mipaka ya kitanzu ili kuibuka na kazi mahuluti. Hii ina maana kuwa, hakuna kazi ya fasihi ambayo inaweza kukamilika bila kuingiliana na kazi nyingine ya fasihi. Malengo makuu ya nadharia hii ni kupinga uchambuzi wa kipweke wa utanzu mmoja mmoja wa fasihi kana kwamba upo utanzu unaoweza kujisimamia kiutendakazi bila kuingiliana na tanzu zingine. Mkabala huu wa kutenganisha tanzu za fasihi ndio ambao umezoeleka katika tafiti na chambuzi nyingi za kazi za fasihi. Mkabala huu unaweka mipaka bayana kati ya tanzu za fasihi kuanzia katika kiwango cha uanishaji. Aidha, utenganishaji huu unaendelezwa pia katika uchanganuzi wa tanzu moja moja za fasihi kana kwamba zinaweza kutekeleza wajibu wake bila kuingiliana na tanzu mbalimbali. Makala hii inathibitisha kuwa uchambuzi wa kazi za fasihi unaweza kufanywa vizuri zaidi kwa kutumia mihimili mahsusi ya nadharia ya Mwingilianotanzu
Maumbo ya Fasihi Simulizi katika Mashairi Andishi Teule ya Kiswahili
Asili ya mashairi ya Kiswahili ni nyimbo simulizi za jamii za Afrika mashariki. Pamoja na vipera vingine vya fasihi simulizi, nyimbo huingiliana katika kujenga mashairi andishi ya Kiswahili. Hata hivyo baadhi ya wasomi katika viwango anuwai wamepuuza fasihi simulizi na kuichukulia kama utanzu sahili wenye thamani duni huku ushairi ukidhukuriwa kama utanzu tata. Makala hii inatalii maumbo ya fasihi simulizi katika mashairi andishi ya Kiswahili ili kuonyesha thamani ya fasihi simulizi katika kujenga mashairi andishi. Data sekondari ilikusanywa kwa kudurusu diwani tatu zilizoteuliwa kimaksudi kuwakilisha vipindi vitatu katika historia ya ushairi mathalani Utenzi wa Fumo Liyongo (Kijumwa, 1964) kuwakilisha kipindi cha urasimi, diwani ya Sauti ya dhiki (Abdalla, 1973) kuwakilisha kipindi cha urasimi mpya na diwani ya Kichomi (Kezilahabi, 1974) katika awamu ya sasa. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa mtindo wa uchanganuzi wa matini. Uchunguzi ulionyesha kuwa maumbo manne makuu ya fasihi simulizi hujenga mashairi andishi ya Kiswahili. Matokeo haya ni muhimu kwa kuonyesha nafasi ya fasihi simulizi katika mashairi andishi na hivyo kuonyesha namna fasihi simulizi inavyoweza kutumika kusahilisha uchambuzi wa mashairi