Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Michakato ya Utohozi wa Istilahi za Sayansi na Teknolojia zenye Asili ya Kiingereza katika Kiswahili
Makala haya yanachunguza michakato ya utohozi wa istilahi za fani ya tiba na kompyuta zenye asili ya Kiingereza katika Kiswahili. Kiswahili na Kiingereza ni lugha ambazo zimekuwa na mwingiliano kwa muda mrefu, hivyo, zimeathiriana kwa kiasi kikubwa. Kwa kuwa Kiingereza ni lugha ya jamii iliyopiga hatua kubwa katika nyanja za sayansi na teknolojia, wazungumzaji wa Kiswahili wanalazimika kutohoa baadhi ya istilahi ili kuziba pengo la kimsamiati. Utohozi huo umebainika kuambatana na michakato mbalimbali ya kifonolojia na kimofolojia. Michakato ya kifonolojia ni pamoja na mchakato wa udondoshaji, ufupishaji wa sauti, uchopekaji pamoja na mchakato wa ufifishaji wa sauti. Michakato ya kimofolojia iliyoonekana kutokana na data ya makala haya ni kama vile mchakato wa mpangilio wa istilahi zenye maneno ambatani, uambishaji pamoja na upangaji wa istilahi za Kiingereza katika ngeli za Kiswahili
Teaching of Translation Studies in Kenyan Universities
The paper critically examines the translation studies situation in Kenyan universities. Further it seeks to outline the interdisciplinary nature of translation studies, and hence its importance to other closely related disciplines, especially language and communication. It also explores the current state of translator training in Kenya and seeks to create an understanding on the scope, opportunities and challenges of translation in the Kenyan context
Language Crimes: The Grammar and Vocabulary of Hate Speech in Kenya
This study examined utterances, public documents, political statements, and data from Kenyan local languages with the view of explaining the phenomenon of hate speech. Using Van Dijk’s Socio-cognitive approach to discourse, the study found that hate speech is perpetrated through grammatical and lexical manipulations. With regard to grammatical choices, the study found that speakers of different communities appropriated morphological particles and demonstratives which are used for normal communication to communicate a condescending attitude towards ‘other’ communities. The study also found that each of the communities had a ‘hate speech’ inventory from which its speakers drew the disdainful words when they wanted to communicate hate messages. Some of the words included names of places, animals and plants. In addition, some of the hate speech messages were communicated through similes and metaphors. Noticeably, when some of the denigrating words became known to the targeted groups, their meanings were expanded as a means to camouflage the hate message. The paper concludes that given the extent to which hate speech is embedded in both the vocabulary and grammar, there is need for linguists to be involved in the resolution of such cases
Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika katika Muktadha wa Utandawazi
Makala haya yanatalii masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika katika ulimwengu na malimwengu ya utandawazi. Kwa muda mrefu, wataalamu wengi wa masuala ya lugha na isimu wamekuwa mbioni katika kuuangazia uhusiano uliopo au unaopaswa kuwepo baina ya lugha na shughuli za kimsingi na maendeleo ya jamii. Mjadala huu hasa umekitwa kwenye mawazo na mikabala ambayo inahusiana moja kwa moja na nguvu na taratibu za utandawazi, ambapo inaaminika kwamba lugha zozote zile ambazo hazitumiwi katika shughuli na harakati za uzalishaji mali huenda zikamezwa na kusahauliwa kabisa hivi karibuni na utamaduni wa Kimagharibi ambao unajitokeza waziwazi katika harakati anuwai za kijamii kama vile uchumi, elimu, uvumbuzi na ugunduzi wa sayansi na teknolojia. Makala haya basi yanaonyesha namna Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika zinaweza kulindwa na kuhifadhiwa ili ziendelee kutumiwa na walio wengi katika shughuli zao za kila siku
Ufundishaji wa Kiswahili na Changamoto zake Mintarafu Chuo Kikuu cha Moi
Ufundishaji wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu ulisisitizwa sana na Tume ya MacKay (1981) iliyopelekea kuanzishwa Chuo Kikuu cha Pili nchini Kenya. Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret ndicho Chuo Kikuu cha pili kuanzishwa baada ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Chuo Kikuu cha Moi kilianzisha mafunzo ya Kiswahili mwaka wa 1987 kwa wanafunzi wa shahada ya ualimu hadi leo, wakiwemo wanafunzi wa shahada ya Kiswahili chini ya Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika. Idara hii leo imetimia miaka thelathini (30) tangu kuzinduliwa kwake. Kwa hiyo, kimantiki, inatarajiwa iwe imeimarika katika vitabu vya kufundishia na marejeleo, na kuwa na walimu wa kutosha. Maswali ya kudadisi ni: Je, haya yametimia? Je, wanafunzi wanaojiunga na idara hii na kupata mafunzo ya Kiswahili wana umilisi wa kimsingi kukabiliana na mtalaa wa somo hili katika kiwango cha shahada? Makala haya yanapigia mbizi maswali haya na kuweka bayana changamoto zinazomkumba mwalimu wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret. 
Uasilishaji wa Maneno ya Kigeni katika Lugha za Kiafrika: Mfano wa Kitharaka
Kila lugha hukopa maneno ya kigeni na kisha kuyaasilisha ili yaafiki mfumo wa kifonolojia wa lugha pokezi. Kitharaka ni lugha iliyokopa maneno na kuyaasilisha kwa mujibu wa mfumo wa fonolojia yake. Makala haya yanaweka wazi mchango wa michakato ya kifonolojia katika kufanikisha uasilishaji wa maneno ya kigeni katika Kitharaka. Kitharaka ni lahaja ya lugha ya Kimeru inayozungumzwa nchini Kenya. Uasilishaji wa maneno ya kigeni kutoka lugha mbili changishi (ambazo ni Kiswahili na Kiingereza) hadi Kitharaka umeangaziwa. Jumla ya michakato minane ya kifonolojia imeshughulikiwa kama vile uchopekaji wa sauti, kuimarika kwa fonimu, kudhoofika kwa fonimu, ukaakaishaji, ung’ong’oishaji, usilimisho, usilabishwaji na uwiano wa irabu. Hatimaye, makala haya yamependekeza uchunguzi zaidi ufanywe ili kuweka wazi jinsi michakato ya kifonolojia katika Kitharaka inavyokamilishana. Vilevile, makala haya yamependekeza uasilishaji wa maneno ya kigeni katika lugha nyingine za Kiafrika uchunguzwe ili kubainisha jinsi lugha hizi zinavyokamilishana na kufaana kukabiliana na changamoto za mawasiliano katika kipindi hiki cha utandawazi
Lugha na Utandawazi: Nafasi ya Kiswahili katika Kukuza na Kuendeleza Demokrasia nchini Kenya
Lugha huwa na nafasi kubwa katika maisha ya jamii huku mawasiliano yakiwa mojawapo wa majukumu yake. Awali, jamii mbalimbali zilikuwa zikijichukulia kama kwamba zimejitenga na jamii nyingine zikiwa na jinsi ya kufanya shughuli zao kivyao. Hii leo, utandawazi umekita na kila jambo linatazamwa kwa muktadha wa dunia kuwa kijiji. Demokrasia ni falsafa ya kisiasa inayoenea kote duniani kwa haraka. Kwa misingi hii, falsafa inatakiwa kuchanganuliwa kwa mujibu wa taaluma zingine za utamaduni kama vile lugha. Kwa hivyo, makala hii inanuia kubainisha nafasi ya lugha katika kukuza demokrasia na uongozi mwema. Inapendekeza matumizi ya Kiswahili na lugha za kiasili kama nyenzo za kukuza na kueneza demokrasia katika muktadha wa bara la Afrika. Pia, inaangazia jinsi taasisi za kijamiii kama katiba, mahakama, tume za uchaguzi, vyombo vya habari na makundi ya kutetea haki za kijamii yanavyotumia Kiswahili kutetea na kuendeleza demokrasia. Inatazamiwa kwamba makala hii itachangia upanuzi wa maarifa katika taaluma ya isimu-jamii, hasa nyanja za uongozi na utawala na majukumu ya lugha. Hatimaye makala hii inapendekeza kwamba lugha ya Kiswahili itumike kufundisha somo la mawasiliano katika ngazi ya chuo kikuu ili kutilia nguvu matumizi yake na wataalamu wanaohitimu katika nyanja mbalimbali
Changamoto za Kuueleza Msamiati wa Samaki: Mtazamo wa Kiuhusiano
Makala haya yanachunguza maelezo ya majina ya samaki katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Kwa kutumia nadharia ya kiuhusiano imebainika kuwa kunatumika vichocheo au mikakati tofauti tofauti ili kumweleza samaki. Hata hivyo, licha ya vijenzi hivi kutumika bado kuna changamoto nyingi kama vile maelezo fulani kukosa uangavu kwa kuwa ni mapana zaidi au kutochangia kikamilifu katika kumweleza samaki kwa kuwa ni maelezo finyu, kutotumia vichocheo vya kutosha au kichocheo kimoja ambapo vichocheo vingi vingefaa zaidi. Aidha, imebainika kuwa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) imetumia vichocheo vya tabia, chakula, rangi, umbo, vumba na hata picha ili kuwaeleza aina ya samaki ili wasomaji waweze kuwatambua na kuwaeleza. Licha ya vichocheo hivi, ni wazi kuwa KKS bado inakabiliwa na changamoto ya kuwaeleza samaki kwa uwazi, uangavu na kwa kukinaisha
Dhima ya Viakifishi katika Ushairi Huru wa Kiswahili
Ushairi, kama zilivyo tanzu nyingine za fasihi, huwasilishwa kwa matini za lugha zilizoakifishwa ili kuelekeza usomaji, uwasilishaji wa kimantiki, kubainisha zaidi matini zilizotumika na kuondoa utata katika fasiri za jumbe kusudiwa. Washairi hutumia viakifishi kama mtindo na mbinu ya kibinafsi katika uwasilishaji. Hata hivyo, kuna aina mbili za matumizi ya viakifishi katika uwasilishaji wa tanzu za fasihi: Kwanza kuna matumizi ya ‘kawaida’ ambayo ni utaratibu unaofahamika miongoni mwa watunzi. Aghalabu matumizi haya yanajitokeza zaidi katika tungo za mashairi zinazingatia mno arudhi katika uwasilishaji. Pili, kuna matumizi ya ‘makusudi’ ya viakifishi ambayo yanabainika zaidi katika uwasilishaji wa mashairi ya Kiswahili yanayowasilishwa kwa kutozingatia mno arudhi za utunzi. Kutokana na uwepo wa njia hizo mbili za uwakifishaji, kuna haja ya kufafanua na kufasiri dhima ya viakifishi katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii inafafanua namna watunzi wa ushairi huru wa Kiswahili wanavyotumia viakifishi kama mtindo na mbinu elekezi katika kuwasilisha hisi, ubainishaji wa ujumbe na ujenzi wa muktadha wa usomaji. Mifano itatokana na baadhi ya mashairi katika diwani za Kichomi (E. Kezilahabi) na Bara Jingine (K. Wa Mberia). Mwishowe, imependekezwa namna viakifishi vinavyoweza kutumiwa kwa ufaafu zaidi katika uelekezaji wa taratibu za usomaji na uwasilishaji wa ujumbe katika mashairi ya Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Kirai na Neno Ambatani katika Kiswahili
Kirai ni kipashio cha kisintaksia ilhali neno ambatani ni kipashio cha kimofolojia. Vipashio hivi vya nyanja mbili zinazohusiana vimekuwa vikijadiliwa na baadhi ya wanaisimu kwa mitazamo tofautitofauti. Vipashio hivi hutazamwa kama vipashio tofauti na wakati mwingine hutazamwa kama vipashio vinavyohusiana. McCarthy (2002) anadai kwamba neno ambatani ni kipashio kidogo zaidi ya kirai na kwamba kipashio hicho hubebwa na muundo wa ndani wa kirai. Hata hivyo, anasisitiza kwamba kisintaksia neno ambatani hufanya kazi kama neno na siyo kirai. Kwa upande mwingine, Gichuru (2010) anadai kwamba uhusiano wa maneno yanayounda neno ambatani unashabihiana na uhusiano unaopatikana katika miundo ya kisintaksia kama kirai. Madai haya ndiyo yaliyosababisha raghba ya mwandishi kushughulikia uchunguzi linganishi wa vipashio hivyo. Hivyo basi, makala haya yamelinganisha na kulinganua vipashio hivyo kwa kuzingatia muundo, maana, matamshi, uhusiano wa vijenzi na othografia ya vipashio husika