Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Vijenzi vya Uduara katika Sanaa za Maonyesho za Jamii ya Wangoni
Makala haya yanafafanua vijenzi vinavyouunda na kuushikilia uduara kama kipengele kimojawapo maarufu cha falsafa ya Kiafrika. Hoja kuu ya makala ni kudhihirisha kuwapo kwa dhana ya uduara katika sanaa za maonyesho za jamii ya Wangoni. Makala haya ni sehemu tu ya matokeo ya uchunguzi mpana uliofanyika katika jamii ya Wangoni kuhusu dhana ya uduara. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu ambazo ni usaili, ushuhudiaji wa utendekaji wa shughuli mbalimbali za kijamii, pamoja na udurusu wa kimaktaba. Makala yana sehemu tano. Sehemu ya kwanza ni utangulizi; ambapo dhana za msingi zinazoyajenga makala zimedokezwa. Sehemu ya pili inafafanua vijenzi vya dhana ya uduara. Sehemu ya tatu inahusu tija za dhana ya uduara. Sehemu ya nne ni hitimisho, na sehemu ya tano ni marejeleo. Kwa ujumla, mjadala wetu umeonyesha kuwa sehemu kubwa ya matukio, matendo na vitu vinavyohusiana na Wangoni hufanywa au kuundwa kwa umbo la duara. Katika makala haya, matukio, matendo na vitu hivyo, vimeelezwa kama ni vijenzi. Vijenzi hivyo ni vitatu. Navyo ni: uchezaji wa ngoma, michezo ya watoto, pamoja na ujumi wao unaojidhihirisha kupitia vifaa mbalimbali vya kutekelezea sanaa za maonyesho
Dhima za Kipragmatiki za Kialami Pragmatiki ‘eh’ katika Kiswahili cha Mazungumzo
Vialami Pragmatiki (VIPRA) ni eneo ambalo limepata mashiko katika uwanja wa isimu. Hali hii imepelekea VIPRA kuchunguzwa katika lugha mbalimbali ulimwenguni kama vile Kiingereza (Taz. Schiffrin, 1987 na Zarei, 2013), Kijerumani (Taz. Hogeweg na wenzake 2016), Kidachi (Taz. Hoek, 2013), Kigiriki (Taz Archakis, 2001), Kichina (Taz. Chen na He, 2001), Kiitaliano (Taz. Bazanella, 1990), Kihispania (Taz. Durán na Unamuno, 2001) Kituruki (Taz. Yilmaz, 2004) na Kiindonesia (Taz. Nasir, 2017). Hata hivyo, VIPRA katika lugha ya Kiswahili havijachunguzwa. Makala haya yanakusudia kuchunguza kuhusu dhima za kipragmatiki za kialami pragmatiki (KIPRA) eh katika Kiswahili cha mazungumzo. Data za makala haya zimekusanywa kutoka katika mazungumzo yasiyo rasmi yanayofanywa na wazungumzaji wa Kiswahili katika maeneo yasiyo rasmi kama vile kwenye vijiwe vya kahawa na vijiwe vya mamantilie. Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kwamba licha ya KIPRA eh kuwa na maana yake ya msingi ambayo ni kukubaliana na jambo, huchanuza pia maana nyingine za ziada kama vile mshangao, swali na msisitizo. Tabia hiyo hukifanya KIPRA hicho kuwa na dhima mbalimbali za kipragmatiki
Utohozi kama Mkakati wa Mawasiliano katika Mazungumzo kuhusu Ukimwi katika Ekegusii
Tangu kisa cha kwanza cha ukimwi kugunduliwa nchini Kenya, juhudi mbalimbali zimefanywa kujaribu kupunguza idadi ya visa vya maambukizi mapya. Juhudi hizo ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu mbinu na njia mbalimbali za kujikinga dhidi ya maambuki. Elimu kuhusu Virusi vya ukimwi (VVU) na ukimwi hutolewa kwa lugha mbalimbali kutegemea hadhira lengwa. Tafiti zimefanywa kuhusu umuhimu wa lugha katika mawasiliano mbalimbali yakiwemo mawasiliano kuhusu ukimwi. Mawasiliano kuhusu VVU/ukimwi husheheni mijadala kuhusu sehemu za siri, kitendo cha ngono, matumizi ya kondomu na watu wanaoishi na VVU miongoni mwa mambo mengine. Ingawa mawasiliano ya aina hiyo hufanyika kwa lugha wazi katika Kiingereza, tafiti zimeonyesha kwamba masuala hayo ni mwiko katika baadhi ya lugha za Kiafrika na kwa hivyo hayawezi kujadiliwa kwa lugha wazi. Makala haya yanachunguza utohozi unavyotumka katika mijadala kuhusu VVU/Ukimwi katika lugha ya Ekegusii. Mjadala ambao unajitokeza katika makala haya ulichochewa na sababu kwamba Ekegusii ni mojawapo ya lugha ambazo zimeweka mwiko kwa mazungumzo kuhusu mambo hayo. Aidha, utafiti ulitaka kuchunguza namna lugha ya Ekegusii inakabiliana na suala ambalo limeibuka katika jamii ya sasa. Lengo la Makala haya ni kujadili namna utohozi umetumika katika kujadili sehemu za siri, kitendo cha ngono na matumizi ya kondomu katika diskosi za VVU/Ukimwi
Ujasiriamali wa Kiswahili Nchini Kenya
Makala haya yanatathmini shughuli za kiujasiriamali nchini Kenya kwa kutumia ‘Kiswahili’. Shughuli zinazoangaziwa zinajikita katika maeneo mbalimbali ambamo aina fulani za Kiswahili zinajitokeza kwa kuzingatia kwamba kuna “viswahili” vingi vinavyotumiwa nchini Kenya. Neno viswahili katika muktadha huu linatumika kwa maana ya aina mbalimbali za Kiswahili zisizo sanifu ambazo zinapatikana katika shughuli za kila siku zinazoendeshwa na binadamu. Viswahili hivi hutokana na wazungumzaji kutoka makabila na maeneo mbalimbali nchini Kenya wanaokitumia Kiswahili. Tumeendesha mjadala unaojaribu kuonesha jinsi gani ujasiriamali wa Kiswahili umechangia katika kukua kwa Kiswahili katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita. Mjadala huu umeongozwa na dhana ya ujasiriamali kama inavyofasiriwa na taaluma ya uchumi kwa kuiegemeza katika muktadha wa uchumi na lugha. Kwa hivyo, tumeangazia ujasiriamali katika shughuli mbalimbali kama vile vyombo vya habari, biashara kupitia mabango na uchapishaji. Isitoshe, tathmini imefanywa ili kudhihirisha athari chanya na hasi kisarufi na kimawasiliano katika kukua kwa Kiswahili kutokana na matumizi yake kiujasiriamali ili kufichua msambao wa athari hizo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki
Kiswahili through the Ages: The Question of Lexicon
Kiswahili has over the past several centuries grown from a community language to an international medium of communication. This is greatly atributed to trade, politics, religion and cultural interaction and exchange. These, among others, have over the ages been the chief rollers in Kiswahili’s expansion and development. This means that apart from standardizing it, which was a deliberate effort, there has been no other effort to develop this vital African tongue comparable to the insurmountable effort that was expended to develop English and French, for example, even in the Swahili-speaking area of East and Central Africa. This work obviates Kiswahili’s development over several centuries, including the final decades of the last Century (i.e. the 20th Century). It looks at its Kiswahili’s detaroriation and argues that there is need for deliberate effort to develop the language
Uhusiano Mwema kati ya Mke na Mume kama Njia ya Kudumisha Ndoa: Mifano kutoka \u27Utendi wa Ayubu\u27
Makala haya yanahusu uhusiano wa mke na mume katika ndoa kwa kuangazia Utendi wa Ayubu (UWA). Utendi huu, unamhusu Mtume mwaminifu wa Mungu aitwaye Ayubu aliyebarikiwa na mali nyingi sana. Alikuwa mcha Mungu na aliyeimarika kwa imani yake. Kutokana na imani hii na baraka nyingi alizokuwa nazo, shetani anamwonea wivu. Shetani anamwomba Mungu ruhusa ili aweze kumjaribu Ayubu. Aliporuhusiwa na Mungu, shetani anamfilisi na kumdhuru kiafya lakini Ayubu anasimama imara katika imani yake na wala hakumkana Mungu. Kwa upande mwingine, Rehema mkewe anaibuka kama mwanamke mnyenyekevu, mwaminifu na anayependa mumewe kwa dhati
Mifanyiko ya Kimofofonolojia ya Konsonanti za Nomino Mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili
Makala haya yanahusu mifanyiko ya kimofofonolojia ya konsonanti za nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili. Uchunguzi huu ulikusudia kuchunguza mabadiliko yanayokumba konsonanti za nomino za Kiswahili zinapokopwa na Kiturkana. Nadharia ya fonolojia zalishi asilia ilielekeza uchunguzi wetu katika kubaini mifanyiko ya kimofofonolojia ambayo konsonanti za nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili hupitia na kanuni zinazodhibiti mifanyiko hii. Tulikusanya data yetu maktabani yaani kutoka kwa Bibilia ya Kiturkana, Misali na Kamusi ya Kiingereza — Kiturkana na kuwasilisha kifonetiki na kiothografia. Utafiti huu umebaini kwamba kuna fonimu ambazo zipo katika Kiswahili lakini hazipo katika Kiturkana. Uchunguzi wetu umetambua kwamba konsonanti za Kiswahili zinapokopwa na Kiturkana hupitia mabadiliko ya kifonolojia kama vile udhoofikaji, uimarikaji, udondoshaji, uchopekaji, usilimisho pamwe wa nazali na ubadala wa konsonanti ili nomino hizi zikubalike katika Kiturkana kwa lengo la kusahilisha utamkaji, kupata muundo mwafaka wa silabi na mofu ya jinsia ambayo hutumiwa kuainisha nomino za Kiturkana
Translation and Adaptation of Kiswahili Classics: Lessons in Domestication and Experimentation
The translation of the classical 18th and 19th century Swahili poetry into English was an important step in disseminating this art-form to a global audience way beyond the African continent. Not only did this translation and adaptation of the classical poetry lead to the translation of Swahili prose in the early 20th century but it also offered useful insights into the nature of Swahili poetry in general. But, what was the criteria used in selecting the poetry works to be translated? The paper which is guided by the tenets of the Equivalence theory as expounded by Xie (2014) briefly looks at the major arguments for and against this theory in achieving meaning equivalence between SL and TL. In doing this, it explores the style and language of a number of classical Swahili poems and concludes that although it is difficult, if not impossible, to achieve a perfect equivalence in translating a rigid form such as poetry, varieties in translations are an asset rather than a liability. Secondly, since poetry is a means of expressing personal or national ideology, feelings and attitudes, its translation acts as a bridging tool through which different cultures can get closer. This is best exemplified in case of the translated Swahili classical poetry
Motifu ya Utaifa katika Bunilizi za Kihistoria za Watoto za Mugyabuso Mlinzi Mulokozi: Ubainifu Wake, Sababu na Umuhimu wa Motifu Hiyo
Wachambuzi mbalimbali wa fasihi wamekuwa wakisisitiza kwamba urudiaji unaojitokeza katika kazi mbalimbali za mwandishi mmoja husukumwa na nia ya mwandishi husika kutaka kusisitiza jambo fulani (taz. Okpewho, 1992; Ntarangwi, 2004;Senkoro, 2011). Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Kimbi (2016) katika kazi tatu za Mulokozi, unaonesha kwamba, tofauti na ilivyokuwa inachukuliwa hapo awali, urudiaji wa dhamira katika kazi za fasihi una dhima nyingi zaidi ya ile ya kusisitiza jambo. Utafiti wa Kimbi (2016) unabainisha kwamba Mulokozi alirudia dhamira ya uzalendo katika vitabu vyake vitatu, yaani Ngoma ya Mianzi (1991), Ngome ya Mianzi (1991) na Moto wa Mianzi (1996) kwa nia ya kuweka msisitizo, kukamilisha hadithi au kisa kilichopaswa kukamilika katika vitabu vyote vitatu, kuonyesha falsafa ya mwandishi, n.k. Bila kurudufu matokeo ya utafiti huo wa Kimbi, makala haya yanakusudia kuchambua motifu ya utaifa katika kazi nne za Mulokozi, yaani Ngoma ya Mianzi (1991), Ngome ya Mianzi (1991) Moto wa Mianzi (1996) na Utenzi wa Nyakiiru Kibi (1997). Kwanza makala inavichambua vitabu husika kwa kuangalia namna motifu ya utaifa inavyojitokeza. Pili, makala inatoa ufafanuzi wa kwa nini mwandishi aliamua kutumia motifu hiyo katika kazi zake. Mbali na uchambuzi wa vitabu teule, makala yametumia pia data za uwandani zilizopatikana kutoka katika mahojiano maalumu aliyoyafanya mwandishi wa makala na mwandishi wa vitabu teule. Makala yanaongozwa na mwega wa Nadharia ya Uoniafrika, ambayo hudai kwamba kazi za kifasihi za Kiafrika zinaweza kueleweka kwa usahihi zaidi kwa kujikita katika mazingira ya kijadi na historia ya jamii husika za Kiafrika. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba kazi teule zilizochambuliwa zina maudhui muhimu yenye mchango mkubwa katika ujenzi wa dhana ya utaifa kwa watoto. Makala yanachambua motifu ya utaifa kwa kina na kisha kuonyesha thamani ya kazi teule katika kuwaandaa watoto wa Kitanzania kuipenda nchi yao na kuitumikia kwa moyo wa umoja
Nafasi ya Fasihi ya Watoto katika Ukuzaji wa Mshikamano wa Kitaifa
Fasihi ya watoto ni aina ya sanaa ambayo imeandaliwa kwa ajili ya watoto. Fasihi hii inaweza kuwa imetungwa na kuandikwa na mtu mzima au mtoto, na hulenga watoto kama hadhira teule. Sanaa hii huhusisha tanzu nyingi ambazo zinawapa watoto nafasi za utendaji. Fasihi ya watoto ina tanzu anuai nazo ni nyimbo na ushairi, michezo ya kuigiza, hadithi, mchongoano na misemo miongoni mwa nyingine. Wakati wa utendaji, watoto hujumuika na wenzao ili kutekeleza utanzu wowote. Wanapojumuika pamoja, watoto huonyesha ushirikiano wao kupitia ugawanyaji wa majukumu, vifaa vya kuchezea, uongozi wa nyimbo na kuwakinga wenzao dhidi ya madhara yoyote. Wanapofanya hivyo, watoto hukuza umoja na mshikamano baina yao. Wakati wa kuimba kwa mfano, watoto huimba kwa zamu ili kila mmoja ahisi kuthaminiwa na wenzake. Ni kwa msingi huu ndipo makala haya yanapambanua nafasi ya fasihi ya watoto katika ukuzaji na uendelezaji wa mshikamano wa kitaifa na utangamano