Moi University Journals
Not a member yet
    344 research outputs found

    Tathmini ya Mikakati ya Tafsiri ya \u27Vinay na Derbelnet\u27 (2004) katika Tafsiri ya \u27A Good Day\u27 (2019)

    No full text
    Uteuzi wa mikakati ya tafsiri katika mchakato wa tafsiri, ni suala muhimu katika Nadharia ya Tafsiri. Lengo la makala haya ni kutathmini mikakati ya tafsiri iliyotumiwa katika kutafsiri ya riwaya ya Kiswahili Siku Njema iliyotafsiriwa kwenda Kiingereza kama A Good Day. Uteuzi wa mikakati ya tafsiri unaweza kuwa na athari zake katika uhawilishaji wa ujumbe. Hata hivyo, suala hili halijapewa nafasi inayostahiki katika tafiti tangulizi kuhusu kazi za tafsiri. Tathmini za tafsiri hujikita kuchanganua changamoto za tafsiri bila kuonesha kwamba uteuzi wa mikakati ya tafsiri una mchango mkubwa katika kuibua changamoto hizo. Modeli ya Vinay na Derbelnet (2004) ilitumiwa kubaini mikakati ya tafsiri iliyotumiwa na wafasiri Dorothy Kweyu na Fortunatus Kawegere. Wataalamu wanakubaliana kwamba Modeli ya Vinay na Derbelnet ndio msingi wa uainishaji wa mikakati ya tafsiri na wataalamu wengine wanaoainisha mikakati ya tafsiri hutumia modeli hii kama msingi wa uainishaji wao

    Mtagusano wa Uforensiki na Riwaya ya Kiswahili: Mfano kutoka Riwaya ya ‘Mzimu wa Watu wa Kale’

    No full text
    Makala haya yanahusu mtagusano wa uforensiki katika riwaya ya Kiswahili. Pia, yanaonesha namna taaluma ya uforensiki inavyojitokeza katika riwaya ya Kiswahili na kuonesha mtagusano ambao umejenga maudhui na fani katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale kwa kujikita katika vipengele vya: wahusika, msuko wa matukio, muktadha, matumizi ya lugha, mgogoro na mtindo wa usimulizi wa kiforensiki. Aidha, makala haya yanatambulisha uhusiano uliopo kati ya taaluma ya Uforensiki na Fasihi katika kufikisha ujumbe kwa jamii husika. Makala haya yatatumia nadharia ya mwingiliano matini ambayo itasaidia kuweka bayana namna taaluma ya uforensiki inavyojitokeza katika riwaya ya Kiswahili. Makala haya pia, yataibua tafakuri mpya ya riwaya ya Kiswahili na uforensiki itakayoleta chachu kwa wanataaluma na wahakiki wa kazi za fasihi katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia

    Memory, The Return of the Repressed and Healing in John Ruganda’s "The Floods"

    Get PDF
    Memory, the agency of speech and the impossibility of forgetting traumatic experiences is central towards the healing process of survivors of violence. Witnessing through narration, although somewhat traumatizing and damaging in itself, is ironically therapeutic and the only way towards coming to terms with a painful past. This article interrogates how memory and remembering is not only a healing process for victims of abuse in an abusive state but also as a strategy that John Ruganda uses to testify to/against a tyranny of the past in “The Floods” to preserve a nation’ collective memory of repression in a violent  political era

    Fasihi ya Watoto ya Kiswahili na Mshikamano wa Kitaifa

    No full text
    Makala haya yanabainisha nafasi ya Fasihi ya Watoto katika mshikamano wa kitaifa. Waandishi wamerejelea vitabu teule vya fasihi ya watoto ambavyo ni Urembo wa Ngiri (2016) na Sungura Mpanda Ngazi (2008). Mshikamano wa kitaifa nchini Kenya umekuwa ukitikiswa hasa kutoka mwaka wa 2007/2008 wakati ghasia zilizuka baada ya Uchaguzi Mkuu. Tangu wakati huo wameibuka waandishi wapya wanaoandikia masual ya fasihi ya watoto ambayo licha ya kuburudisha ina dhima na mielekeo mipya inayolenga kukuza utaifa na mshikamano. Makala haya yanalenga kuthibitisha kuwa fasihi ya watoto imechukua mielekeo mipya ambapo, sawia na fasihi ya watu wazima, inatekeleza dhima muhimu katika uhamasisho wa kisiasa na mshikamano wa kijamii

    Ushairi na Umoja wa Kitaifa

    No full text
    Ushairi ni utanzu mkongwe wa fasihi. Ulianza na binadamu mwenyewe alipobuni lugha (Fischer, 1953). Inadaiwa kuwa binadamu alianzisha ushairi alipovumbua lugha. Baada ya maendeleo ya mwanadamu, utanzu huu ulijijengea lugha ya kipekee ambayo ni ya mvuto na kunata. Kupitia lugha hii faida nyingi zinaweza kupatikana kwa matumizi yake. Faida mojawapo ni kuhamasisha jamii ya Wakenya kukubaliana, kuvumiliana na kupendana. Mtazamo huu unaleta umoja wa kitaifa ambao unahitajika sana nchini Kenya. Kenya imekuwa na tabia ya mgawanyiko mkubwa kila wakati wa uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi huo. Jambo hili lilitokea 2007/8, 2013 na 2017. Kuna njia nyingi za kukabiliana na tatizo hili. Mojawapo ni matumizi ya ushairi ulio na lugha ya nguvu sana inayowagusa watu katika sherehe na hafla mbalimbali. Unaweza kutumika kama nyimbo, maghani au katika maandishi. Utafiti huu kwa hivyo, unalenga kuchunguza ushairi unavyoweza kuchangia kuunganisha Wakenya wa jamii mbalimbali wanaoongea lugha tofauti tofauti. Kenya ina jamii arobaini na nne tukiongezea jamii ya Wamakonde iliyotambuliwa 2017 na serikali ya Jamuhuri ya Kenya. Utachunguza mashairi ya awali na tenzi zilizozungumzia umoja wa jamii na mashairi ya hivi punde kutathmini iwapo utanzu huu unaweza kuendeleza au kuchangia umoja wa kitaifa nchini Kenya

    Changamoto za Kuunda Programu Tumizi ya \u27Kikagua-Tahajia\u27 ya Lugha za “Runyačitara”

    No full text
    Makala haya yanafafanua changamaoto za kuunda programu tumizi ya kikagua-tahajia cha lugha za “Runyačitara”. Kwa kuwa lugha za “Runyačitara” ni lugha ambishi bainishi, maumbo ya maneno na uchanganuzi wake kimofolojia ni changamani. Uchangamani huu unafafanuliwa na namna unavyozua changamoto za kiothografia, kimofolojia na kileksika katika mchakato wa kuandaa kikagua-tahajia. Data kutoka uwandani na maktabani imechambuliwa kwa kutumia mbinu linganishi. Imebainika kwamba ili maneno yaweze kutumiwa katika mchakato wa kukagua-tahajia, kuna haja ya kuunda kamusi ya leksimu ambayo itaingizwa kweye kompyuta, kuelezea othografia, ruwaza na kanuni za undaji wa maneno na sarufi maumbo ya lugha za “Runyačitara” kwa ujumla. Katika kufanya hivyo, makala haya yanabaini kwamba ingawa kuna maneno mnasaba, kuna changamoto za kimofofonolojia na za kileksika katika maneno ya lugha hizi. Kwa miundo inayofanana kanuni za kuandaa maneno kwa ajili ya kikagua- tahajia zimependekezwa

    Language Police in Code-Switching: A Case of the Language Used by Politicians in Kenya

    No full text
    Kenya is a multilingual nation with about eighty different ethnic languages. Kenyan politicians use language as a weapon with which they woo the electorate. One way of so doing is by code switching or code mixing. This paper shows instances of code switching/code mixing while explaining why the Kenyan politicians do so as they address the electorate. In this paper, the concepts of code switching and code mixing are interchangeably used given the varied morpho-syntactic nature of all the languages in use in Kenya. Data for the paper was obtained from the University of Nairobi students who were Communication major and Sociolinguistics major. The discussions in the paper are anchores on selected tenets of Communication Accommodation Theory as espoused by Howard Giles. The paper demonstrates that Kenyan politicians code switch because of the need to be accepted by those from a particular ethnic group they are addressing at that particular time not that they are deficient in the matrix language

    Mwingiliano wa Kimtindo katika Tendi: Mifano kutoka \u27Mikidadi na Mayasa\u27 na \u27Kalevala\u27

    No full text
    Uwepo wa tendi katika maeneo ya Afrika umezua mjadala na mgogoro mkali mno katika jamii ya usomi.  Hii ni kutokana na rai kuwa wasomi na watafiti wengi kutoka maeneo ya Kimagharibi walidai kuwa Afrika hakuna tendi ila kinachodaiwa kuitwa tendi ni masimulizi ya kisifo tu. Wahakiki wengine wamezifutilia mbali tendi hizi kwa kudai kuwa maudhui yake ni ya kichawi na sihiri. Pia, vigezo vya kuainisha tendi vilivyotumiwa na wanazuo wa Kimagharibi vilikuwa vya kimaeneo na kimakusudi, walidhalilisha tendi za Kiafrika. Licha ya kuwa kuliibuka watafiti wa Kiafrika na kudai kuwa Kusini mwa Sahara ya Afrika kuna tendi, wao pia walielekea kutumia vigezo ambavyo ni vya kimaeneo. Ili kujaribu kutatua mzozo na utata uliopo kuhusu uwepo wa tendi katika maeneo ya Kiafrika, utafiti huu ulinuia kuchunguza iwapo kuna mwingiliano wa kimtindo baina ya tendi za maeneo haya mawili. Madhumuni makuu yalikuwa kutathmini iwapo kuna mwingiliano wa vipengele vya kimtindo baina ya tendi za Kiafrika na zile za Kimagharibi licha ya tendi za Kiafrika kufutiliwa mbali na baadhi ya wasomi wa Kimagharibi. Makala yalichunguza tendi mbili zinazopatikana katika maeneo ya Kiafrika na Kimagharibi. Tendi hizi ni Utendi wa Mikidadi na Mayasa unaopatikana Afrika na Utendi wa Kalevala unaopatikana Finland katika maeneo ya Kimagharibi.&nbsp

    Changamoto Zinazokumba Uchanganuzi, Ufasiri na Ufunzaji Ushairi wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya

    No full text
    Makala haya yanaangazia baadhi ya changamoto zinazokumba taaluma ya ufasiri, uelewekaji na ufundishaji wa somo la ushairi katika shule za sekondari nchini Kenya. Mawazo na kauli zinazoshereheshewa katika makala haya zinazotokana na utafiti wa kisayansi uliofanyika katika kaunti mbili za Mombasa na Trans Nzoia. Pamoja na kufafanua changamoto husika, nimejizatiti vilevile kutoa mapendekezo na suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo. Tunataraji kuwa utafiti huu utanufaisha na kuimarisha ufunzaji wa ushairi na lugha ya Kiswahili kwa jumla

    Mchango wa Wanawake wa Kiswahili katika Uongozi, Dini na Ushairi 1350 B.K-1840 B.K.

    No full text
    Wataalamu wengi wa fasihi ya KiSwahili hawajui kwamba kuna washairi wengi wa KiSwahili wa kike, ambao wamechangia sana katika tasnia hii. Mshairi maarufu anayejulikana na wengi ni Mwana Kupona binti Mshamu. Ni wachache zaidi wanaojua hata kiongozi mmoja mashuhuri wa kike. Katika makala haya, nimeangalia mchango wa washairi na viongozi wa kike wa KiSwahili, wa upwa wa mwambao wa Afrika Mashariki na visiwani. Kwa kutoa ithibati za kimapisi na kiushairi, nathibitisha kwamba wanawake wa KiSwahili wamekuwa katika mstari wa mbele kiutunzi, kidini, kimapisi na kiuongozi, kwa muda mrefu sana. Wameshughulikia sio tu waadhi na mapenzi, mbali pia yale waandishi kwa kiume wa KiSwahili wameshughulikia. Nimejikita kati ya mwaka 1350 B.K na 1810 B.K. Nimeonyesha kwamba ni baada ya majilio ya watawala wa kigeni ambapo mwanamke wa KiSwahili alizidi kukandamizwa, kwa sababu za kidini, kitamaduni na kikoloni. Wa aidha, nimedhibitisha kwamba washairi na viongozi hawa wa kike walipatikana sio katika sehemu moja tu, bali katika upwa mzima na visiwani

    145

    full texts

    344

    metadata records
    Updated in last 30 days.
    Moi University Journals
    Access Repository Dashboard
    Do you manage Open Research Online? Become a CORE Member to access insider analytics, issue reports and manage access to outputs from your repository in the CORE Repository Dashboard! 👇