Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Matumizi ya Vielelezo vya Kihisabati katika Fafanuzi za Fahiwa Mbalimbali
Isimu ni taaluma ya sayansi ya lugha ya binadamu. Usayansi huu unaorejelewa katika uchanganuzi wa lugha huzingatia sifa anuwai hasa uwazi, utaratibu na urazini au kutoa uamuzi kulingana na data inayorejelewa. Ingawa masuala ya kiisimu hushughulikiwa katika makala mbalimbali kwa kutumia vielelezo maalum vya kiisimu, inabainika vilevile kuwa kuna uwezekano wa kutumia vielelezo teule vya kihisabati katika fafanuzi za dhana anuwai katika isimu. Ingawa vielelezo hivi vinadhihirika katika hisabati, tafiti nyingi zinaonyesha vilevile kuwa vinaweza kutumiwa kikamilifu katika tawi la isimu linalojulikana kama isimu kihisabati. Hivyo basi, makala haya yanazungumzia jinsi tunavyoweza kutumia kikamilifu vielelezo vya kihisabati katika fafanuzi za fahiwa mbalimbali katika Kiswahili. Makala yanadhamiriwa kutoa mchango mkubwa katika mafunzo ya semantiki kileksika pamoja na taaluma ya isimu kihisabati
Nafasi ya Kiswahili katika Utoaji wa Huduma za Afya Tanzania
Lugha ya Kiswahili kama zilivyo lugha nyingine duniani, hufanikisha mawasiliano katika jamii. Mawasiliano hayo yanaweza kuwa ya watu wa utamaduni mmoja au watu wa jumuiya kubwa zenye wazungumzaji wa lugha mbalimbali na wenye tamaduni tofauti. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na jamii kubwa zaidi Afrika Mashariki hususan Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Kongo na kwingineko (Kiango, 2002). Lengo la makala haya si kujadili nafasi ya Kiswahili kwa mwelekeo wa mawanda hayo mapana, bali kujielekeza katika eneo mahususi ili kubainisha na kujadili nafasi ya Kiswahili katika utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania. Makala haya yanazingatia kuwa licha ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha inayofahamika sana kwa Watanzania waliowengi, zipo changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania wanapotumia lugha ya Kiswahili wakati wa kutoa au kupokea huduma za afya nchini. Changamoto hizi ni pamoja na wataalamu wa afya kupata mafunzo kwa lugha za kigeni suala linalosababisha wataalamu hao kukosa msamiati wa kitaalamu wa lugha ya Kiswahili, matumizi ya lahaja mbalimbali za Kiswahili, kutofautiana kwa lugha mama na tamaduni za lugha husika na matumizi ya misimu au lugha za mitaani. Kutokana na changamoto hizi, lugha ya Kiswahili hushindwa kutumika kikamilifu katika mawasiliano baina ya watoaji na wapokeaji wa huduma za afya
Sanaajadiiya Mtandaoni: Misimbo Ibuka Yaimarika ilhali Kiswahili Chaganda
Kama lugha nyinginezo, ubunifu ulioandamana na ngoma za jadi, mashairi, miiko, ngano na masimulizi mengineyo katika lugha ya Kiswahili ulididimia na sanaa hii ikagandama pale tanzu mbalimbali zilipoandikwa kwenye vitabu. Kiswahili kiliposambaa kutoka Uswahilini, hakikujumuisha kimamilifu sanaajadiiya ya tamaduni za wakaazi wa bara. Hivyo basi kumekuwa na haja ya uwiano kati ya sanaajadiiya ya Kiswahili na ile ya tamaduni nyinginezo. Makala haya yanauangaza msimbo ibuka wa Sheng na jinsi umekuwa kielelezo kizuri cha namna vipengele vya lugha ya Kiswahili vinaweza kufinyangwa upya na kuendelezwa ili kusawiri uhalisia wa watumizi wa lugha. Makala inadai kuwa Kiswahili kimeganda katika uwanja wa sanaajadiiya na nafasi yake kuchukuliwa na Sheng hasa katika matumizi ya TEHAMA. Tanzu nne za sanaajadiiya ya Sheng zitajadiliwa; mchongoano, ujinga ni…, methali, na uvumi. Makala haya yatajaribu kujibu maswali kama vile; Je, tanzu hizi ni upotovu wa nidhamu au ni sanaa yenye nafasi yake katika utagusano wa kijamii? na je, ni kwa kiasi gani tanzu hizi za sanaajadiiya zimefanikiwa kutekeleza majukumu yanayotekelezwa na sanaa kwa jumla? Makala yanapendekeza ukubalifu wa misimbo ibuka itakayowasilisha uhalisia wa mikatadha tofauti ya Kiafrika ili kukifanya Kiswahili kukubalika katika sehemu tofauti za Afrika
Mabadiliko ya Kimofofonemiki katika Msamiati Mkopo wa Kikipsigis
Kila lugha ni mfumo huru unaojitosheleza kisarufi. Ingawa hivyo, wasemaji wa lugha tofauti wanapotagusana kimawasiliano, lugha zao huweza kuathiriana kisarufi, na athari mojawapo huwa ni ukopaji wa msamiati. Ni kutokana na hali hii ambapo utafiti huu ulichunguza kanuni zinazofuatwa katika uingizwaji wa msamiati mkopo wa Kiswahili na Kiingereza katika Kikipsigis. Makala haya yalichunguza mabadiliko ya kimofofonemiki yanayotokea katika msamiati mkopo unapoingizwa katika mfumo wa Kikipsigis. Vilevile, sababu za ukopaji zilibainishwa. Data ya utafiti iliteuliwa kimakusudi. Utafiti ulitambua kuwa Kikipsigis hufupisha irabu ndefu katika msamiati mkopo. Vilevile, irabu unganifu husahilishwa ili zikubalike katika Kikipsigis. Kimsingi tulitambua kuwa Kikipsigis hutohoa irabu ngeni kwa kutumia irabu asili zinazokaribiana kimatamshi. Ilibainika pia kwamba Kikipsigis hakiruhusu mfuatano wa konsonanti mwanzoni mwa neno. Kwa hivyo, Kikipsigis hutohoa msamiati wa aina hii kwa kuchopeka irabu. Katika kuchunguza vichocheo vya ukopaji, makala haya yalibainisha kwamba Kikipsigis hukopa msamiati ili kurejelea dhana ngeni isiyokuwepo katika utamaduni wake. Hata hivyo, uchanganuzi ulionyesha kuwa Kikipsigis wakati mwingine hukopa msamiati hata kama kina msamiati asilia kwa sababu ya ubadilishaji msimbo, msamiati mkopo ni sahili na rahisi kutamkwa ukilinganishwa na kisawe chake cha Kikipsigis
Lugha za Kienyeji kama Kizingiti cha Kuleta Umoja wa Kitaifa na Uwiano Barani Afrika
Lugha ni chombo muhimu sana katika kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa na wa kieneo. Katika taifa la Kenya na kanda ya Afrika ya Mashariki, hakuna lugha iliyo na uwezo wa kuleta mshikamano na muungano tunaoutamani isipokuwa Kiswahili. Kiswahili kina wajibu mkubwa wa kuchangia mshikamano wa kitaifa na wa kikanda. Hata hivyo, lugha hii inakumbwa na changamoto nyingi katika kutekeleza wajibu huu adimu, zikiwemo zile za kijamii, kiuchumi, na za kisiasa. Mojawapo ya changamoto kubwa inatokana na lugha za kiasili ambazo huwa ni kikwazo kikubwa kutokana na kutumiwa kwazo na wananchi wengi katika mataifa mengi ya Afrika ya Mashariki. Lugha za kiasili hutumiwa kwa wingi sana katika mataifa mengi ya Afrika ya Mashariki, hususan katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Ni katika nchi ya Tanzania pekee ambapo Kiswahili hutumiwa ipasavyo na ndiposa nchi hiyo inaakisi muungano wa kitaifa. Makala haya yatatathmini jinsi lugha ya Kiswahili inavyoweza kutumiwa kama wenzo wa kuchangia katika kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa na wa kikanda pamoja na changamoto zinazokikumba Kiswahili katika wajibu wake wa kuleta umoja wa kitaifa na wa kikanda. Zaidi itachanganua ushindani unaotokana na lugha enyeji
Juhudi za Kukabiliana na Kuangamia kwa Lugha za Kiafrika
Dhana ya kuhatarishwa kwa lugha imejadiliwa ndani ya muktadha wa dhana ya kufa kwa lugha. Hivyo, makala yamezijadili sababu mbalimbali zinazipelekea lugha, kuhatarishwa, na hatimaye kufa. Dhana za kuhatarishwa na kufa kwa lugha zimejadiliwa kwa pamoja kwa sababu zinasababishana, yaani, ya kwanza inapotokea, uwezekano wa ya pili kutokea ni yakini. Makala yamerejelea takwimu ambazo zinaonyesha kwamba zaidi 50% ya lugha zilizoko ulimwenguni huenda zikahatarishwa na kutoweka kufikia 2100. Hii ni kutokana na sababu za kiuchumi, kisiasa, kisera, hali kadhalika, kuhamia lugha kuu na changamoto ya kuibuka na kuongezeka kwa miji. Hali hii huweza kusababisha wasemaji wa lugha ndogondogo kuhamia lugha kuu kwa ajili ya kusaka kazi. Makala yameonyesha namna lugha hizo zilizo hatarini zinavyoweza kuokolewa, kutokana na juhudi za kisera
Muakiso wa Uhalisi wa Kauli za Mhusika Mlevi na Uchagizaji wa Tafsiri kwa Msomaji katika Fasihi ya Kiswahili
Tamthiliya ya Kiswahili ni miongoni mwa kazi za kisanaa zenye wajibu mkubwa wa kuijenga jamii katika hali mbalimbali kupitia wahusika wake. Kwa kawaida, wahusika hudhibitiwa na kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na muktadha wa utunzi, hasa mawazo yanayowahusu waandishi kulingana na falsafa zao, mazingira yao, utamaduni wao, hali yao ya maisha na harakati zilizopo katika jamii inayohusika. Kwa msingi huo, makala haya yanachunguza muakiso wa uhalisi wa kauli za mhusika mlevi na jinsi zinavyochagiza tafsiri kwa msomaji. Imefanya hivyo kwa kurejelea tamthiliya teule za Lina Ubani (1984) na Mabepari wa Bongo (2007). Uchunguzi ulikuwa wa maktabani uliohusisha uhakiki wa tamthiliya zilizolengwa. Data zilikusanywa katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha kilichopo mkoani Iringa kwa kudurusu kazi mbalimbali zilizohusiana na mada iliyochunguzwa. Uchambuzi na mjadala wa data zilizowasilishwa umeongozwa na nadharia ya Ucheshi. Makala haya yanahitimisha kwamba, mhusika mlevi ni mojawapo ya mawakala wa kazi za kifasihi kwa kuwa huyafichua na kuyaweka wazi yale yote yanayoshindikana kusemwa na wahusika wanaoongea na kutenda wakiwa katika ung’amuzi tambuzi
Orality and Sublimation of Repressed Desires: The Renaming of Everyday Phenomena by the Luo Women of Kenya
The psychoanalytic theory of sublimation within Freudian conceptualizations involves the channeling of socially unacceptable behaviours into approved ones for social cohesion. The human mind, in this context, is capable of protecting itself from painful experiences by repressing unpleasant experiences into the unconscious and sublimating the same safely onto socially correct overt expressions. For Freud, the repressed desires can be unearthed from dreams. Like dreams, myths, legends and other folklore material as works of the human imagination can help unearth the repressed desires of a people. Although repression and its attendant sublimation act as an institution of social propriety and harmony, understanding its underlying presence is important in the interrogation and possible explanations of conflicting undercurrents that may be perceived in society. This paper looks at the renaming of varying objects and ideas among the contemporary women in rural Luo Nyanza as subversions of western feminism. The argument is that the renaming of obvious objects and ideas within the woman’s area of socio-cultural operation is a code that she uses to sublimate her desired expression of sexuality. The phrases used to rename phenomena are analyzed within Freudian theorizations of sublimation as society valuation acts, but which nevertheless exhibit underlying contestations of western feminism by the modern Luo woman. The study focusses on one ethnic group as the issues raised can be interpreted within their conceptualizations of gender relations that subvert the woman’s occupation of power roles and covert suppression of the same. The phrases analyzed are in constant use among the rural Luo women, but some have been appropriated by both men and children. The analysis points to these as creative constructions which belie psychological symbolisms and which can be read as contemporary strategies to resist popular expectations by feminist liberality
Pre-Texts of Black Intellectual Tradition: Some Examples
Any intellectual tradition, it may be argued, emerges through constant acts of transgression, translation and appropriation of prior epistemological positions. These prior epistemological positions may be thought as constituting points of reference for emerging traditions, in fact as pre-texts around and against which new textualities (traditions) announce their presence and distinctiveness. In the context of African literary tradition, which is my concern here, I use the term pre-texts to refer to both oral (African) and written (European) traditions, themselves already inscribing multiple traditions, and whose presence in African texts give the later a hybrid identity
Is the ‘Post’ in Postcolonial the ‘Post’ in Postpone? A Reading of Dreams Deferred in Peter Kimani’s Before the Rooster Crows
In the 1950s and 1960s, nationalism was still regarded as the feature of the victorious anti-colonial struggles in Asia and Africa…By 1970s, nationalism had become a matter of ethnic politics, the reason why people in the Third World killed each other…in cruel and often protracted civil wars…The leaders of African struggles against colonialism and racism had spoiled their record becoming heads of corrupt, fractious, and often brutal regimes (Partha Chatterjee 1999). For JaramogiOginga Odinga nationalism lost its glamour in Kenya when Kenyatta, the founding father of the nation and who was generally perceived as one of the foremost nationalist in the continent failed to mention the role played by the nationalists in his speech ushering independence. He reminds us that "Kenyatta’s own speech inexplicably made no mention of the people who had laid down their lives in the struggle, the fighters of the forests and the camps who have been in danger in Kenya of becoming the forgotten men of freedom fight because it suits the ambitions of the self-seeking politicians to divert our people from the real freedom aims of our people" (p.253)