Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Tafsiri Tenge katika Matini Zilizotafsiriwa kwa Tafsiri-Mashine: Uchanganuzi wa Matini za Kiingereza-Kiswahili
Makala haya yanachunguza mchakato wa kutafsiri kwa Tafsiri-Mashine. Tafsiri- Mashine baina ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza hutumiwa na wasomi, wafasiri, watalii, watafiti na wajifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni au ya pili. Kwa hivyo, ni nyenzo muhimu katika mchakato wa kutafsiri matini. Hata hivyo, mchakato huu unakabiliwa na changamoto za tafsiri tenge kama inavyodhihirika katika makala haya. Mbinu ya uchambuzi wa matiniilitumiwa kukusanya data iliyojenga msingi wa makala haya. Matini zilizotafsiriwa kwa kutumia Tafsiri- Mashine (kuanzia sasa, TM) zilichanganuliwa kiulinganishi. Matokeo yanaonesha kwamba tafsiri ya neno kwa neno inayotumika kwa upana katika TM ina upungufu katika kuhawilisha maana kutoka Kiingereza (lugha chanzi) kwenda Kiswahili (lugha lengwa). Tafsiri haihusishi tu maneno na sentensi bali ni mchakato changamani unaohusisha vipengele vingi. Mwandishi wa makala haya ameonesha mifano anuwai ya tafsiri tenge na kutoa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kwamba lugha nyingi za Kiafrika ikiwemo lugha ya Kiswahili, hazijaweza kufaidi katika mbinu hii ya kutafsiri kwa mashine (kompyuta)
Historically Grounded Symbolism and the Thematic Lacuna in Translation: The Translation of \u27Treasure Island\u27 into Kiswahili as \u27Kisiwa Chenye Hazina\u27
This paper avers that the available translations of Treasure Island in Kiswahili literature under the title Kisiwa Chenye Hazina are testimony to translation strategies producing unintended consequences in the target literature. The 1928 translation of Treasure Island by J. Johnson with revisions by M. Saidi in 1981 and the 1956 translation with revisions by Peter Kisia (1993) into Kiswahili as Kisiwa Chenye Hazina are illustrative of translations abounding with paucity of source text details, glossing over the meticulous descriptive details of the source text, blotching the richness of the figurative language in the source text; neutering the source text’s symbolism marked by its figurative language, characterization formats, scenery descriptions as well as names referring to people, places and things. The blotching of these foundational aspects of source text unconsciously generates partial thematic realizations in the target text. Whereas the source text intricately advances a rich medley of subtle subtext(s) suggestive of among other issues colonialism in varied facets, social class hierarchies, interaction between “respectable” society and the posterior sub-culture of piracy. A critical thematic analysis of the Kiswahili translations does not come across this subtext(s) of Treasure Island in Kisiwa Chenye Hazina. Instead, the translations reveal a pseudo-translation and fractional renditions—to use Toury’s (1984) terminology, they also exhibit myriad instances of trite paraphrases, translational shifts of source text descriptions, sceneries and characters, indistinct dialogues, unjustified additions and skewed renditions
Nafasi ya Sitiari katika Mabadiliko ya Kisemantiki ya Leksia za Kiswahili: Ulinganisho wa Kiswahili cha Kabla ya Karne ya Ishirini na Kiswahili cha Kisasa
Makala haya yamejadili nafasi ya sitiari katika mabadiliko ya kisemantiki ya leksia za Kiswahili kwa kulinganisha mifano mahususi ya Kiswahili cha kabla ya Karne ya Ishirini na Kiswahili cha Karne ya Ishirini na Moja. Aidha, imeshughulikia mahusiano kati ya maana za leksia za awali na za kisasa. Makala pia imejadili athari za sitiari katika muundo wa lugha ya Kiswahili. Asili ya data iliyochanganuliwa ni kutoka kwa matini teule za kabla ya Karne ya Ishirini na kutoka kwa wazungumzaji wenye elimu-asilia. Uchanganuzi umeonyesha bayana kuwa mbinu ya sitiari imekuwa muhimu katika kubadilisha maana za leksia na pia muundo wa kisemantiki wa Kiswahili, katika kipindi kilichotafitiwa. Pindi jamii nzima ilivyobadilika kutokana na maendeleo ya sayansi, teknolojia, uchumi, kijamii na kisiasa, ndivyo pia lugha ya sitiari mpya zinazidi kuchipuka
Dhima ya Fasihi katika Mshikamano wa Kitaifa: Tathmini ya Tungo za Tom Olali
Makala haya yanajadili suala la dhima ya fasihi katika kuleta mshikamano wa kitaifa. Hili ni suala zito barani Afrika, ambapo mchakato wa kujenga utaifa ulioanza katika harakati za ukombozi, unakabiliwa na changamoto nyingi. Nchini Kenya, kwa mfano, tumeshuhudia matukio kadha ambayo yametishia kuliporomosha taifa lililozaliwa mwaka wa 1963. Mfano mzuri ni vurugu ya baada ya uchaguzi mwaka wa 2007 hadi 2008. Msimamo wetu ni kwamba fasihi ya kitaifa inaweza kutoa mchango muhimu katika kuleta mshikamano wa kitaifa na amani ya kudumu. Lakini swali ni je, ni fasihi ya aina gani inayoweza kufanikisha hilo? Katika kutafuta jawabu la swali hilo, tunazitathmini kazi za Tom Olali, ambaye ni mmojawapo wa waandishi wa Kiswahili nchini Kenya. Kazi zinazohusika ni: Mafamba (2008), Watu wa Gehenna (2012) na Mashetani wa Alepo (2015). Tumetathmini vipengele vya fani na maudhui ya kazi hizo mintarafu ya mada ya iliyotajwa hapo juu
Feminism Ideology and Institution of Patriarchy in African Novel: Analysis of Selected Works of Women Writers and Gynandrists
This paper uses feminism ideology in reading and understanding the effects of patriarchy in the African Novel, a generic reference to novels articulating African experience. The paper analyses selected works of African women writers and gynandrists from Anglophone and Francophone Africa. Gynandrists are men writers sympathetic to women cause. Specifically, the paper examines feminism and patriarchy in Postcolonial novel, where several gender issues are identified and explored. Even further, the paper discusses the ideology of feminism and its multiple strands is used as an ideological praxis to underline women struggles in taming the institution of patriarchy. The selected novels are Ngugi Wa Thiongo’s Devil on the Cross, Buchi Emecheta’s The Joys of Motherhood, Tsitsi Dangarembga’s Nervous Conditions, Sembene Ousmane’s God’s Bits of Wood, Mongo Beti’s Perpetua and Mariama Ba’s So Long a Letter. Instances of the strategies that women are employing in the aforementioned literary works are analysed and elevated to exemplify the use of feminist ideology in taming patriarchy. The paper also appreciates the bold attempts women have made to reverse men’s dominance in social, political, and economic domains in order to establish gender respect, equality, and partnership for the survival of the society
Athari ya Ukiushi wa Kisarufi katika Tafsiri ya Matini katika Majukwaa ya Kidijiti
Jukumu la kimsingi la lugha kama mfumo wa maana unaowakilishwa kwa maumbo ya kisarufi ni kukidhi mahitaji ya mawasiliano miongoni mwa watumiaji wake. Lugha hupata uamilifu huu pale vipashio vyake vinapopangwa kulingana na kanuni za kimofosintaksia za lugha hiyo. Mpangilio huu ndio unaozalisha matini zenye mshikamano na ambazo hujitosheleza kimaana. Hata hivyo, dhima hii inaweza kuvurugwa pale ambapo maana inayowasilishwa katika lugha fulani imefumwa kutokana na tafsiri. Japo matini chanzi inatarajiwa kuchakatwa kwa usadifu katika matini lengwa, kadhia ya tafsiri na tofauti kati ya lugha chanzi na lugha lengwa huweza kufisidi maana. Hali hii huelekea kudhihirika zaidi kutokana na maendeleo ya Tehama ambayo yameathiri pakubwa matumizi ya lugha ikiwemo taaluma ya tafsiri. Ni kutokana na hoja hii ambapo makala haya yanaangazia jinsi ukiushi wa kisarufi unavyoathiri maana ya matini tafsiri katika Majukwaa ya Kidijiti. Uteuzi wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata sampuli sadifu ya data kutoka tuko.com na bbc.com. Data zilizokusanywa na zilichanganuliwa kinathari huku majedwali yakitumiwa kuweka wazi matokeo. Matokeo ya utafiti huu yanatazamiwa kuwa na umuhimu wa kutoa maarifa kuhusu mbinu na mikakati ya uhawilishaji waujumbe wenye muumano kwa watafsiri wa matini asilia na za mtandaoni. Waaidha, kazi hii itanufaishamashirika ya uanahabari na wanahabari huria wanaonuia kuboresha tafsiri za taarifa zao na vilevile kuchochea wasomi wanaonuia kutafiti kuhusu masuala ya kipragmatiki yanayodhihirika katika tafsiri za lugha mbalimbali
Mchango wa Kazi Teule za Fasihi katika Kukabiliana na Janga la UKIMWI
Janga la UKIMWI limekuwa katika jamii zetu kwa zaidi ya miaka thelathini. Katika kipindi hicho zaidi ya watu milioni 34 wameambukizwa ugonjwa huo ulimwenguni. Isitoshe, kwa mujibu wa UNAIDS (2012), zaidi ya watu milioni 18 wameaga dunia. Tangu kisa cha kwanza cha UKIMWI kugunduliwa nchini Kenya, juhudi mbalimbali zimefanywa kujaribu kupunguza idadi ya visa vya maambukizi mapya. Juhudi hizo ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu mbinu na njia mbalimbali za kujikinga dhidi ya maambukizi. Njia moja muhimu ambayo yaweza kutumiwa kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu UKIMWI ni kupitia kazi ya fasihi. Kwa mintarafu hiyo, makala haya hususan yanatathmini mchango wa kazi teule za fasihi andishi katika kukabiliana na janga la UKIMWI. Kwa vile tiba ya UKIMWI haijagunduliwa, utafiti huu ulilenga kutoa mchango kwa jamii ambao waweza kufahamisha umma kuhusu mbinu na njia za kutumika katika kukabiliana na janga la UKIMWI
Navigating the Worlds of John Ruganda’s "The Burdens" and "Black Mamba"
Elam contends that the world of drama is constructed relative to the world of actuality, which the performer and spectator of drama inhabit. He says the dramatic world “is a spatio-temporal elsewhere represented as though actually present for the audience” but it is counterfactual; not real or factual (Elam, 1987, p.99). The interpretation of the dramatic world, therefore, is based on the conventionality of the world of actuality. This is to say that we access the world of drama from the position of the world of actuality. “The spectator assumes that the represented world, unless otherwise indicated, will obey the logical and physical laws of his own world,” (p. 104). The spectator, it is assumed, enjoys a shared semantic and cultural context with the dramatis personae of the dramatic world. This obtains because the semantic and cultural interactions that are observed in the dramatic world are modeled on those of the world of actuality. It is this shsred cultural awareness and socialization of the individual that enable the spectator to fill in the gaps that exist in the world of drama in order to make the same world complete and meaningful. This paper explores how past experiences of characters in John Ruganda’s plays, The Burdens and Black Mamba,bring into perspective the bearing their past has on their present and future
Usawiri wa Wanawake katika Vitabu vya Kiada vya Somo la Kiswahili katika Shule za Sekondari Nchini Kenya
Makala haya yanachunguza usawiri wa wanawake katika vitabu vya kiada vya somo la Kiswahili katika shule za secondari nchini Kenya. Matini katika jumla ya vitabu vya kiada 21 yalichanganuliwa. Wilaya ya Kakamega ilitumiwa kama eneo la utafiti ili kukusanya data. Shule 33 zilitumiwa kwa lengo hili ambapo walimu wa Kiswahili 72 na wanafunzi 291 walishiriki katika uchunguzi huu. Nadharia ya kifeministi ya uhakiki wa kazi za kisanaa na ile ya uchanganuzi wa usemi zilitumiwa kuupa utafiti mwelekeo. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia programu ya tarakilishi ya SPSS. Uchunguzi huu uligundua kwa jumla kuwa vielelezo vya picha katika vitabu vya kiada viliwasawiri wanaume wengi kuliko wanawake. Vilevile wanaume wengi kuliko wanawake walitajwa. Kama ilivyotarajiwa, wanawake wengi kuliko wanaume walisawiriwa katika majukumu ya kifamilia nyumbani, huku wanaume wakisawiriwa katika ajira za kitaaluma na za hadhi ya juu kuliko wanawake. Maudhui ya vitabu hivi yaliwapendelea wanaume kuliko wanawake. Kutokana na ugunduzi huu, ilipendekezwa kuwa wakuza mitaala wahimizwe kuidhinisha vitabu vya kiada ambavyo vimejumuisha masuala ibuka kama vile jinsia na vilivyosawiri jinsia zote kwa usawa. Aidha, ilipendekezwa kuwa vitabu vitumie mifano ya wanawake waliofaulu na walionawiri katika tasnia mbalimbali kama viigwa bora kwa wanafunzi wa kike. Vilevile wanawake na wanaume wengi wenye mwamko wa kijinsia wajitose katika uwanja wa uandishi ili kuwasawiri wanawake inavyostahiki
Nyimbo kama Mkakati wa Kuimarisha Mshikamano wa Kitaifa na Uwiano Barani Afrika: Uchunguzi wa Nyimbo za Kampeni za Wachuka
Katika makala haya, tumeangazia namna nyimbo za kampeni zinaweza kutumika kuimarisha mshikamano wa kitaifa na uwiano Barani Afrika. Nyimbo za kampeni tunazotilia maanani katika mjadala huu ni zile zilizokuwa zikiimbwa toka 1992-2013 katika jamii ya Wachuka. Makala haya yanatambua ukweli kwamba wanasiasa hutumia si nyimbo tu bali hutumia hotuba, maandishi na hata pesa kuweza kuyapata mamlaka ya kisiasa na hata kujidumisha hapo baada ya kuyapata. Katika mjadala huu, tunaongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Usemi Hakiki (U.U.H). Tutaelezea Wachuka ni kina nani na wanapatikana wapi. Katika uchanganuzi wetu, tutaangalia muktadha wa nyimbo hizi, wahusika wanaopatikana mle, ujumbe uliomo na jinsi lugha ya ushawishi inavyotumika kuuwasilisha. Katika lugha, tutajikita katika masuala matatu: vipashio vya lugha, mshikamano na mtindo unaotumika kuuwasilisha ujumbe wa ushawishi. Baada ya kuyashughulikia masuala hayo yote, tutahitimisha makala yetu kwa tumaini kuwa tutakuwa tumedhihirisha jinsi nyimbo zinaweza kutumika kuleta muumano wa kitaifa na uwiano Barani Afrika kwa manufaa ya wote