Moi University Journals
Not a member yet
    344 research outputs found

    Nafasi ya Mwingiliano Fani katika Kukuza Fasihi ya Watoto

    No full text
    Makala haya yanahusu jinsi vipengele vya fani vinavyotumiwa katika vitabu vya fasihi ya watoto ili kufanikisha malengo ya waandishi. Utafiti uliofanywa uliongozwa na nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1916). Nadharia hii inajibainisha kwa kuangalia ujumla wa uhusiano wa sehemu moja kwa nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa kuongozwa na nadharia hii tulichukulia fasihi kuwa kitu kizima kinachojengwa kwa maudhui na fani. Katika ngazi ya pili fani nayo imeundwa kwa vipengele mbalimbali vya lugha kama vile methali, misemo, nahau, taswira, picha na tashbihi. Vipengele hivi vilitambuliwa na matumizi yavyo yakafafanuliwa na kuelezwa. Utafiti huu uliteua kimakusudi riwaya za Kisasi Hapana, Nimefufuka, Sitaki Iwe Siri, na Wema wa Mwanakatika kuchunguza jinsi mwingiliano fani unavyofanikisha kazi za fasihi zinazolenga watoto

    Taasubi katika Shirikana za Kivumba: Mtazamo wa Kisemiotiki

    No full text
    Makala haya yanachunguza baadhi ya shirikina za Kivumba kwa nia ya kubainisha ya kwamba, zinaashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume katika jamii husika. Hakuna usawa wa kijinsia katika masuala kama vile malezi ya watoto na ulaji wa vyakula hasa kwa mwanamke. Ili kukuza mjadala wetu, makala yamefafanua ishara na maana kama zinavyojidhihirisha katika baadhi ya mifano ya shirikina za Kivumba. Makala haya yanachukulia kwamba sio rahisi kufasiri ishara na maana katika shirikina za jamii yoyote nje ya mkutadha wa jamii hiyo. Ushahidi wote unaotegemewa katika mjadala wetu ulitokana na mifano iliyokusanywa kutoka nyanjani

    Uzingativu wa Yaliyoandikwa kuhusu Mada: Mifano kutoka Baadhi ya Tasnifu za Kiswahili

    No full text
    Makala haya yanajadili nafasi ya yaliyoandikwa kuhusu mada katika taaluma ya utafiti. Mwandishi anarejelea data au kazi mbalimbali za kitafiti katika viwango vya uzamili na uzamivu ili kutoa tahadhari kwa watafiti na wanataaluma wanapokuwa mbioni katika kutekeleza majukumu ya kitafiti. Mwandishi anajadili suala la mchango na manufaa ya utafiti kwa jamii hasa inapotokea kwamba utafiti unaohusika ni wa awali na haujawahi kufanywa na watafiti watangulizi. Makala yanajadili mustakabali wa utafiti katika taaluma za Kiswahili, huku akionyesha namna ya kujiepusha na changamoto zinazoendana na utafiti, katika mapana na marefu yake

    Configuring Thematic Tropes in Kiswahili Literature: Translating Mariama Ba’s \u27So Long A Letter\u27 as \u27Barua Ndefu Kama Hii\u27

    No full text
    The scholarly explications of literary translations in Kiswahili have for long been predicated on a paradigm which homogenizes and explicates all translations as unvarying in meaning, habitually focused on the transposition of literary value from English into Kiswahili. This paper contends that the translation of Song Long a Letter into Kiswahili as Barua Ndefu Kama Hii affirms Venuti’s assertions and demonstrates a conscious rewriting that variously configures literary themes in Kiswahili literature. It further contends that literary translation is a cultural undertaking that enables the rendition of literary and cultural material in target paradigms. By foregrounding the social and cultural significance of the source text, the translation is a tour de force that reinvigorates feminist writing in Kiswahili literature, underprops knowledge creation, and refocuses the centrality of translation as enabling the perception of difference and presentation of alternative possibilities

    Tamathali za Usemi na Taswira katika Utenzi wa \u27UKIMWI ni Zimwi\u27

    No full text
    Utenzi wa UKIMWI ni Zimwi ni kazi iliyotungwa na Mahmoud Abdulkadir wa Lamu katika mwaka wa 2001. Huu ni utenzi ambao mwandishi aliutunga kwa lengo la kuwajuza watu athari za janga la UKIMWI. Utenzi huu umeandikwa katika lahaja ya Kiamu. Maudhui na dhamira ya kazi ya fasihi haziwezi kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya kuwako kwa lugha. Matumizi ya lugha ni mapana kwani huhusisha tamathali za usemi, uteuzi na mpangilio wa maneno basi, sajili za lugha, matumizi ya nahau na misemo n.k. Katika makala haya, ninashughuliki hasa matumizi ya tamathali za usemi na taswira katika utenzi wa UKIMWI ni Zimwi

    Nafasi ya Tafsiri katika Ufundishaji wa Kiswahili: Mfano wa Ufundishji wa Kiswahili katika Shule za Upili nchini Uganda

    No full text
    Makala haya yanaangazia maoni ya walimu na wajifunzaji kuhusu matumizi ya tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji Kiswahili katika shule za upili nchini Uganda. Suala mojawapo linalozua mgogoro miongoni mwa wasomi, wataalamu, walimu na wajifunzaji wa lugha ni matumizi ya tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kigeni na ya pili.  Wanafunzi walioshiriki walikuwa wa kidato cha kwanza na cha pili. Data ilichanganuliwa kwa kutumia nadharia ya umotishaji wa lugha iliyoasisiwa na Gardner (1985) na kuendelezwa na Dörnyei (1994). Matokeo yanaonesha kwamba tafsiri ina nafasi kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za upili nchini Uganda. Aidha, imebainika kwamba tafsiri haiwezi kuepukika katika mazingira ya ufundishaji wa Kiswahili nchini Uganda. Hata, hivyo mbinu hii inapaswa kutumika pamoja na mbinu nyinginezo na kwa njia inayofaa

    Athari za Ulumbilugha Miongoni mwa \u27Chokoraa\u27

    No full text
    Makala haya yanachunguza athari za ulumbilugha katika kutimiza nia za wakati husika za Chokoraa. Chokoraahutumia lugha mbalimbali katika mawasiliano yao. Uteuzi wa lugha itakayotumiwa na Chokoraa hutegemea muktadha maalum. Chokoraa hutumia Kiswahili, Sheng’, Kiingereza na lugha za asili katika mazungumzo yao. Ulumbilugha ndio huwafanya Chokoraa wakati mwingine kuchanganya ndimi kwa kutumia lugha ambazo wanazijua huku wakitaka kutimiza nia mahsusi. Kwa hali hii basi tunaweza kusema kuwa wanaulumbilugha huteua lugha kwa mujibu wa muktadha kutokana na ukweli kuwa lugha moja yaweza kuwa faafu katika muktadha mmoja na wala sio mwingine. Pia, makala haya yanaainisha athari za ulumbilugha kama zinavyojitokeza katika mazungumzo ya Chokoraa wa mtaa duni wa Mathare, jijini Nairobi

    Masuala Ibuka katika Fasihi: Mfano wa Insha za Kifasihi za "Staffroom Diary" katika Magazeti ya ‘Sunday Nation’ (Kenya) na ‘Citizen’ (Tanzania

    No full text
    Makala za Staffroom Diary ambazo huwasilishwa kwa mseto wa Kiigereza na Kiswahili, ni aina ya insha za kifasihi za mienendo ambazo mbali na kutekeleza jukumu la kuburudisha na kujipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa wasomaji wa magazeti ya “Sunday Nation” (Kenya) na “Citizen” (Tanzania) hutekeleza jukumu kuu la fasihi ambalo ni kuzindua na kuelimisha jamii kuhusu masuala anuai yanayoikabili. Kwa kuzingatia nadharia za Udenguzi na Uhalisia, makala hya yanabainisha masuala ibuka yanayojumuishwa katika uandishi wa Mwalimu Andrew

    Ecolinguistic Analysis of Kalenjin Narratives: Illustrations from Discourses on River Protection

    No full text
    This paper ecocritically analysed the language forms chosen by the folk narrative composer to establish how the language is used to contribute to the protection of water sources. Fairclough’s Critical Discourse Analysis (CDA) approach was adopted as the method of analysis. Results indicate that there are experiential, relational and expressive values embedded in the folk narrative while verbs and the active voice are the language forms employed. In addition, representation of actions as material processes and foregrounding of agency are language strategies that play an important role in aiding the protection of the environment. Besides, punishment, a non-linguistic strategy is used to persuade listeners to avoid actions that pollute water sources

    Proverbs and Enculturation: The Gender Convergence of Kiswahili and Ekegusii Proverbs

    No full text
    Proverbs in Swahili and Gusii cultures are formulated and deployed in subtle ways that underpin the processes of enculturation and as such, proverbs are implicated in the inscriptions of femininity and masculinity in their respective societies. There is no doubt that both the concept of gendering and the construction of gender itself occupy contested positions in African socio-cultural scholarship. Part of the contestation alluded to here and that has subsisted over a long time is the implication of proverbs as “cultural oralities” in the inculcation of gender as a principle of societal organization. Available scholarly evidence contends that, as artistic phenomena proverbs are crafted with patriarchal bias and as such they are involved in the marginalization and relegation of women in virtually all sectors of human endeavor and social interaction. Like in many other African cultures, proverbs are critical in facilitating the definition of moral consciousness, thought and belief, they are a reflection of “wisdom and truth” preserved and passed from one generation to another. However, it is important to note that in the artistic exquisiteness of proverb folklore are presentations of partiality, prejudice and deprecating image inculcation about women. This formulaic depiction of women in Swahili and Gusii proverbs curtails, blurs and mutes women’s notable contributions in the development of humanity in their respective societies. This paper, therefore, seeks to explore the covert and explicit enculturation of patriarchal bigotry in Swahili and Gusii proverbs

    145

    full texts

    344

    metadata records
    Updated in last 30 days.
    Moi University Journals
    Access Repository Dashboard
    Do you manage Open Research Online? Become a CORE Member to access insider analytics, issue reports and manage access to outputs from your repository in the CORE Repository Dashboard! 👇