Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Sheng kama Lugha ya Biashara jijini Nairobi: Masiala ya Kijamii Yanayoathiri Nafasi yake katika Utangaziaji wa Biashara
Sheng ni lugha kipindi chini Kenya ambayo imeenea katika utangaziaji wa biashara mbalimbali jijini Nairobi kwa sababu ni lugha pendwa nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana na ambao ndio walio wengi. Vijana wengi jijini Nairobi hutumia Sheng na kuiona kama lugha inayowapa ujitambulishaji, mvuto wa kiujumisia na ubunifu wa aina yake hasa inapotumika katika utangaziaji wa biashara jijini Nairobi. Sheng pia imeonekana kutumiwa na wauzaji bidhaa walio na sifa tofauti tofauti za kijamii kama vile umri na jinsia ili kuivutia hadhira lengwa na kujitambulisha nayo. Lengo kuu la makala haya ni kubainisha masiala ya kijamii yanayoathiri nafasi ya Sheng katika utangaziaji wa biashara jijini Nairobi. Hii ni kutokana na hali kwamba katika karne hii Sheng imetagaa kimatumizi jijini Nairobi hasa katika utangaziaji wa biashara mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa. Data kwa ajili ya Makala haya ilikusanywa na mtafiti kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunguzi shiriki. Watafitiwa 80 ambao ni wauzaji bidhaa walichaguliwa kimaksudi na kushirikishwa. Nadharia ya Maafikiano ya Mawasiliano iliyoasisiwa na Giles na Wenzake (1970) na Nadharia ya Mchezo iliyoasisiwa na John von Nuemann na Oskar Morgentern (1944) pamoja na mikondo ya hivi karibuni kuzihusu nadharia hizi zilitumiwa katika uchanganuzi wa data. Matokeo tuliyopata yameonyesha kuwa kunayo masiala mbalimbali ya kijamii ambayo huathiri matumizi ya Sheng katika utangaziaji wa biashara jijini Nairobi. Miongoni mwayo kukiwepo jinsia, umatabaka, viwango vya elimu, umri na mahali pa makazi ya wahusika jijini Nairobi
The Transatlantic Slave Trade and the Reimagination of Colombian Identity in the Poetry of Jorge Artel
The literary tradition of South America has generally been imagined and legitimized in terms of the continent’s Hispano-American cultural heritage, epistemologies, and genealogies. Amid this hegemonic tradition, Black and Indigenous cultural presences and creative imaginaries have been relegated in favor of Hispano-American worldviews. Artistic creations by these “other” subjects have long been considered secondary to the Creole/mestizo canons, and have thus not benefited from the same degree of critical attention and circulation in mainstream literary circles. However, the trend is gradually changing, at least with regard to Afro-Colombian literature, as new generations of creative voices have gradually gained space and interrogated the generally accepted paradigms of Colombian identity. In the same vein, works long shunned by critics and the reading public have been reevaluated and granted increased editorial attention, critical scrutiny, and legitimizing awards. Jorge Artel’s poetry reinscribes Black bodies, cultural symbols, epistemologies, and legacies of the transatlantic slave trade into Colombian national history. His poetry, which is inscribed within the negrista tradition, reexamines the Colombian Atlantic space, especially his home city of Cartagena de Indias, questioning entrenched cultures of marginalization. His collection, Tambores en la Noche (Drums in the Night), first published in 1940, can be considered a reimagination of that city’s memorial cartography in order to underline the vestiges of enslaved Africans and their continuous configuration of Colombian national identity
Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya \u27Mafuta\u27
Riwaya ni mojawapo ya tanzu za fasihi andishi ambazo zimepiga hatua kimaendeleo katika uandishi wake. Mathalan, riwaya ya Kiswahili imeandikwa na waandishi ambao ni Waswahili na ambao si Waswahili. Kwa hivyo, riwaya ya Kiswahili inaeleza tajriba ya Waswahili na Waafrika wengine wasiokuwa Waswahili. Mazingira wanamotoka waaandishi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, yamechangia na kuathiri uandishi wao. Waandishi hawa wameingiza vipengele vya fasihi simulizi na utamaduni wa jamii zao katika riwaya za Kiswahili wanazoandika. Makala haya yanalenga kuchunguza jinsi uingizaji wa vipengele hivi vya fasihi simulizi za watunzi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, unachangia umahuluti wa riwaya hii. Mahsusi, makala haya yamedadavua mchango wa tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi katika umahuluti wa riwaya ya Kiswahili kupitia mfano ya riwaya ya Mafuta iliyoandikwa na Katama Mkangi. Uchunguzi huu umefanywa kwa kutumia Nadharia ya Umahuluti wa Utamaduni inayoshikilia kwamba panapotokea hali ya mtagusano baina ya tamaduni tofauti, matokeo yake si wingi-tamaduni bali ni mchanganyiko wa vipengele kutoka tamaduni hizi ambao zao lake huwa na sifa za kimahuluti. Nadharia hii imetumiwa kufafanua jinsi umahuluti wa riwaya ya Kiswahili umechangiwa na uingizaji wa vipengele vya tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi kutoka jamii ya mtunzi teule ambaye si Mswahili. Katika kufanya hivyo, makala haya yamebainisha jinsi riwaya ya Kiswahili ilivyo nyumbufu kwa ambavyo inajumuisha vipengele kutoka asili anuai ambavyo vinaifanya kuwa changamano na ya kimahuluti
Tafakuri ya Upolisemia na Usitiari wa Ungonoshaji wa Maneno katika Kiswahili cha Mazungumzo
Kumeibuka tabia ya baadhi ya wawasiliani wa Kiswahili kuyapa tafsiri za kingono maneno ambayo hayahusiani moja kwa moja na ngono. Katika miktadha mingi ya kimawasiliano ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wawasiliani kukihusisha na ngono chochote kisemwacho; iwe kwa misingi ya viungo vya ngono, mitindo ya ngono, au tendo la ngono. Hali hiyo ndiyo ambayo katika makala hii tunaiita ungonoshaji. Licha ya kuwapo kwa viashiria vya kusambaa kwa ungonoshaji, nafasi yake kiisimu bado haijafahamika. Hilo ndilo lililoibua haja ya kufanya utafiti huu kwenye Kiswahili cha mazungumzo, huku tukijiuliza iwapo ungonoshaji unahusiana na polisemia au sitiari. Chanzo cha data za makala hii ni maktabani ambapo data zilikusanywa kwa mbinu ya uchanganuzi wa nyaraka. Data hizo zilihusisha kauli mbalimbali zenye viashiria vya ungonoshaji zilizosemwa na watu mbalimbali na kunukuliwa na kuhifadhiwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika mfumo wa sauti au video. Mitandao ya kijamii tuliyoiteua na kuitumia ilikuwa Youtube, Instagram na Facebook. Makala hii basi imebaini kuwa, kwa kiasi kikubwa, ungonoshaji wa maneno katika Kiswahili cha mazungumzo kwa kiasi kikubwa una sitiari ingawa polisemia pia hujitokeza
Uteuzi wa Lugha katika Mahubiri ya Kikristo Jijini Nairobi
Makala haya yalichunguza hoja zilizoathiri uteuzi wa lugha iliyotumiwa na wahubiri wa Kikristo jijini Nairobi katika mahubiri yao. Wahubiri kadha kutoka kwa makanisa mbalimbali walishirikishwa katika utafiti huu. Wahubiri hao walihitajika kujaza hojaji na vilevile kushiriki kwenye mahojiano ya ana kwa ana wakati wa kukusanya data. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa hoja zilizoathiri uteuzi wa lugha katika mahubiri ya Kikristo jijini Nairobi ni pamoja na: aina ya washiriki katika mazungumzo, muktadha wa mazungumzo, yaliyomo kwenye mazungumzo, uamilifu wa mazungumzo na malengo ya mazungumzo. Aidha, tuligundua kuwa wahubiri wa Kikristo jijini Nairobi waliteua lugha ya kutumia katika mahubiri wakizingatia jukumu mahususi ambalo lingetekelezwa na lugha iliyoteuliwa kufanikisha malengo yao ya Kimawasiliano. Utafiti unabainisha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano ya kidini katika maeneo yaliyo na sifa ya wingilugha
Juhudi za Fasihi katika Kukabiliana na Janga la \u27UKIMWI\u27: Kifani cha Riwaya ya \u27Ua la Faraja\u27
Janga la UKIMWI (Ukosefu wa Kinga Mwilini) limekuwa katika bara la Afrika kwa muda sasa. Licha ya kuzuka kwa majanga mengine ya kiafya kama saratani, korona, kisukari miongoni mwa mengine, UKIMWI bado unatishia kudumaza mustakabali wa bara Afrika. Hali hii inatokana na maambukizi yake kusambaa na kuongezeka kila uchao. Mikakati kadhaa imewekwa na Shirika la Afya Duniani (World Health Organization-WHO) ikiwemo kuwaelimisha watu kuepuka maambukizi ya ugonjwa huu kama hatua ya kukabiliana nao. Fasihi ni mojawapo katika nyenzo hizi zinazotumiwa kufundisha na kuielekeza jamii. Ni kwa misingi hii ambapo makala haya yamezuumu kudadisi na kutathimi mchango wa fasihi ya Kiswahili katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Makala haya yanahakiki riwaya ya Ua la Faraja (2004). Uteuzi wa riwaya hii ulifanywa kimakusudi kutokana na upekee wake wa kuliangazia janga hili kwa mapana. Makala haya hivyo basi yanachunguza namna mwandishi anavyosawiri ugonjwa huu tangu ulipochipuka duniani, namna unavyoambukizwa, athari zake kwa umma na jinsi ya kuepuka maambukizi yake. Mwisho, makala yanadhihirisha kuwa licha ya hatari inayoletwa na ugonjwa huu, yapo matumaini makubwa katika udhibiti wake barani Afrika
Usawiri wa Wahusika wa Kike katika Tamthilia za \u27Sudana\u27 na \u27Dunia Hadaa\u27
Suala la mahusiano ya wanawake na wanaume ulimwenguni limekuwa na linaendelea kuwafikirisha wahakiki na wanafasihi kote duniani kwa karne nyingi. Katika kuikabili kadhia hii, kumeibuliwa nadharia na mitazamo mbalimbali inayojaribu kueleza namna ya kuleta maridhiano ili kutuliza mgogoro baridi usiosita kwa kusudi la kutafuta usawa wa kijinsia. Mtazamo unaohusishwa na mhakiki wa kimarekani, Mary Ellman katika kitabu chake Thinking about Women, mwandishi huyo alielekea kughadhabishwa na jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika kazi zilizoandikwa na waandishi wanaume. Aidha, aliangazia jinsi baadhi ya waandishi wa kike wanavyoendeleza usawiri huo hasi wa wanawake katika kazi zao. Mawazo ya Ellman yaliungwa mkono na Millet (1970) katika Sexual politicsalipowashambulia waandishi wa kiume kwa kuwasawiri wahusika wao wa kike kwa mtazamo hasi. Hali hii inachochea fikira kwamba waandishi wa kiume huwasawiri wahusika wa kike kwa namna tofauti wakilinganishwa na waandishi wa kike. Ikiwa kauli hiyo ina mashiko, basi itakuwa sawa kudai kuwa waandishi wa kiume ndio wa kulaumiwa kwa kuendeleza usawiri mbaya (hasi) kwa wahusika wa kike. Pia, ni sawa kudai kuwa waandishi wanawake wanawasawiri wahusika wa kike kwa mtazamo mzuri (chanya). Lengo la makala haya ni kulinganisha usawiri wa wahusika wa kike katika tamthilia ya Sudana ya Mazrui na Njogu (2006) na Dunia Hadaa ya Kisovi, (2007) ambazo zimeandikwa na waandishi wa jinsia tofauti. Makala haya yanakisia kuwa pana uhusiano wa karibu baina ya jinsia ya mwandishi na usawiri wa mhusika wa kike. Pia, tunachukulia kuwa pindi mitazamo ya waandishi hawa itakapobainishwa itasaidia kukadiria uwezekano wa fasihi kuwa chombo madhubuti katika kufikia usawa wa kijnsia. Ili kufikia lengo hili, tumeongozwa na nadharia ya Ufeministi wa Baada-ukoloni. Nadharia hii imetuwezesha kutambua sifa za mwanamke mwafrika akisawiriwa na waandishi waafrika
Utamaduni Mahuluti katika Ushairi wa Kithaka wa Mberia: Mtazamo wa Baadaukoloni
Kabla ya kuja kwa Waarabu, wamishenari na wakoloni nchini Kenya, Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa jumla, wenyeji walikuwa na mila na tamaduni zao. Waarabu, wamishenari na wakoloni walipoingia, tamaduni na mifumo ya maisha ilibadilika. Waarabu walikuja kufanya biashara na kueneza dini ya Kiislamu miongoni mwa wenyeji. Wamishenari vilevile walileta mafunzo mageni kupitia dini ya Kikristo. Baadhi ya wenyeji waliasi tamaduni na mila zao na kupokea mafunzo ya dini ya kigeni. Wakoloni walipokuja, walileta elimu ya kigeni, iliyofundishwa kwa lugha yao; waliendeleza utumwa na kunyakua mashamba licha ya kudhibiti njia kuu za uchumi. Aidha, walileta mifumo mipya ya sheria na kudhihirisha ubaguzi wa rangi kwa sababu ya mila, tamaduni na mienendo yao ya maisha. Kutokana na ujio na maingiliano ya wageni hawa na wenyeji, athari nyingi za kigeni zilianza kuonekana kama vile unyanyasaji wa kiuchumi, unafiki wa kidini, ukahaba na utumwa. Mambo haya yote yalichangia kuibuka kwa utamaduni mahuluti. Vipengele hivi vya utamaduni wa kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni ndivyo vinaonyesha kuwa utamaduni mahuluti unaweza kuwa mzuri na vilevile mbaya. Katika uchanganuzi huu, udhihirishaji wa athari za utamaduni mahuluti katika ushairi wa Kithaka wa Mberia na namna unavyodhihirika katika jamii ya leo umejadiliwa kwa misingi ya nadharia ya baadaukoloni. Katika makala haya, tunachanganua suala la utamaduni mahuluti kama linavyojitokeza katika baadhi ya mashairi ya Kithaka wa Mberia katika diwani za Mchezo wa Karata (1997), Bara Jingine (2001), Redio na Mwezi (2005) na Msimu wa Tisa (2007)
Zanzibari Poetic Worlds
This article draws on my PhD fieldwork, carried out in late 2019, for which I interviewed just under fifty Zanzibaris who were all involved in the production, performance, publication, and/or criticism of poetic works in Zanzibar. Poetry on the Swahili coast has been highly regarded for centuries and has formed a key part of knowledge production in Swahili society. Poetry remains ubiquitous in Zanzibar, as testified by the sheer quantity of poets who continue to produce, perform, and publish. These poets and their poetry, along with the relevant social and political institutions, play out struggles in a space that intersects all strata of society as they compete for literary capital or relevance. This article uses Pascale Casanova’s idea of a literary “world” or “space” to examine how a specifically Zanzibari poetic space functions, using two examples of poetic practices within this world. In particular, the article seeks to answer the following questions: how do artists, institutions, and poetry within this world relate to one another; what rules or norms govern this space; and how and why are these being adapted or developed to suit modern concerns? 
Mwingiliano wa Kisimulizi katika Tenzi za \u27Fumo Liyongo\u27 (UFL), \u27Gilgamesh\u27 (UG), \u27Mikidadi na Mayasa\u27 (UMM) pamoja na \u27Simulizi ya Samsoni\u27 (SS)
Makala haya yanajadili suala la mwingilianomatini katika tendi teule na matini ya kidini. Mabadiliko katika jamii yanayoletwa na teknolojia ya kisasa yamesababisha baadhi ya kazi za kijadi kama vile tenzi, kusahaulika. Tenzi ni hifadhi muhimu ya historia ya jamii, hivyo zinafaa kuhifadhiwa kwa kufanyiwa utafiti zaidi ili ziendelee kuwa na manufaa katika jamii. Kutokana na udurusu wa maandishi uliofanywa na watafiti, ilidhihirika kwamba tenzi za Fumo Liyongo (UFL), Gilgamesh (UG), Mikidadi na Mayasa (UMM) pamoja na Simulizi ya Samsoni (SS) zinawasilisha visa mbalimbali kwa njia ya usimulizi. Matini hizi teule zina mwangwi fulani unaohisika kisimulizi. Makala haya yamezingatia Biblia kama matini muhimu ambayo ina wingi wa kazi za kifasihi zinazohitaji kuhakikiwa, mojawapo ikiwa Simulizi ya Samsoni. Makala haya yamejadili mbinu za kisanii zilizotumika kisimulizi ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa