Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Practices of Everyday Life as Urban Cultures: A Reading of \u27Matatu\u27 Slogans in Eldoret, Kenya
A contested site of ‘organized’ chaos, the matatu industry renders itself to analysis due to its nature. The industry, deemed to be for the poor and thus on the peripheries, carries within it intricacies worth appreciation. For a long time, the industry has been marred with chaos, disorder and complete disregard of the rule of law. However, despite this state that forces society to enforce order (uniforms, crackdowns), the matatu industry, for this paper, offers rich fodder for social commentary. This paper, premised on an on-going study, reads the matatu culture as a mirror within which social, political and economic realities are expressed within the mobile text. It is thus an attempt at reading the matatu slogans as the practices of everyday aimed at circulating certain ideologies. The paper’s discussion is grounded on the discourse theory developed by the French philosopher Michel Foucault (1926-1984) and on selected tenets of The Practice of Everyday Life as espoused by Michel de Certeau (1925-1986). Specifically, the paper seeks to examine the extent to which matatu slogans and mottos are a reflection of urban culture, analyse the social relevance and significance of matatu slogans and mottos, and present a syntactical analysis of the matatu slogans and mottos. Adopting a qualitative approach, it reads a mobile text with the intention of inspecting the relationship between matatu slogans and urban cultures in Eldoret . The author relies on ethnographic and social survey methodology to explore the writing of short catchy texts that take the form of ‘creolized proverbs’, not necessarily traceable to any particular oral tradition in Kenya but which seem to be a summary of local experience and distillation of local anxieties and aspirations. The study collected at least 20 ‘matatu proverbs’. An observation checklist and camera were used to collect data. The information collected on the inscriptions was organized in categories based on the most common emerging themes. From the 20 randomly collected slogans, it emerged that the most common theme is on morality and social education. This is followed by religious messages. Overall, matatu slogans are syntactically arranged to emphasize meaning, provoke thinking and make the messages punchy and memorable. Matatu slogans hold significant value to society. They admonish people about hard work and moral uprightness. They also criticise insincerity and dishonesty. Matatu slogans also reflect the inherent urban culture. This culture is chaotic and forces individuals to survive by any means. It is a money-driven culture. While many would do anything to survive in this culture, majority still hold on to their religious and moral commitments
Athari za Mazingira Asilia ya Mtunzi katika Ukiukaji wa Kaida za Uhalisia kama Kipengele cha Uhalisiamazingaombwe katika Riwaya za Shaaban Robert na za Euphrase Kezilahabi
Makala haya yanachunguza jinsi ukiukaji wa kaida za uhasilia kama kipengele cha uhalisiamazingaombwe unavyojitokeza katika riwaya za Shaaban Robert na za Euphrase Kezilahabi. Riwaya zilizoteuliwa ni Kusadikika (1951) na Adili na Nduguze (1952) za Shaaban Robert pamoja na Nagona (1990) na Mzingile (1991) za Euphrase Kezilahabi. Tumefanya uteuzi wa kazi mbili za Shaaban Robert na mbili za Kezilahabi ili kupata kazi zinazosadifu matumizi ya ukiukaji wa kaida zilizoandikwa kabla na kipindi cha usasabaadaye katika fasihi ya Kiswahili. Kazi za Shaaban Robert zilizoteuliwa zimewakilisha kipindi kabla ya usasabaadaye na za Kezilahabi zimewakilisha kipindi cha usasabaadaye katika riwaya ya Kiswahili. Tumechagua riwaya zilizoandikwa katika vipindi hivyo tofauti ili kuchunguza jinsi ukiukaji wa kaida kama kipengele cha uhalisiamazingaombwe ulivyotumika katika nyakati tofauti katika historia ya riwaya ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu suala au tukio fulani linaweza kuonekana la ukiukaji wa kaida au la kawaida kulingana na mabadiliko yanayotokea katika jamii uhusika. Mabadiliko hayo yanaweza kusababishwa na miingiliano ya jamii kiutamaduni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Riwaya za Adili na Nduguze na Kusadikika za Shaaban Robert zimeteuliwa kwa sababu ndizo riwaya zake zilizosheheni matumizi mengi ya ukiukaji wa kaida zenye sifa za uchawi na mazingaombwe zaidi ya riwaya zake zilizosalia; Ilihali riwaya za Nagona na Mzingile licha ya kusheheni matumizi mengi ya ukiukaji wa kaida lakini ndizo riwaya za Kezilahabi zilizoandikwa kipindi cha usasabaadaye katika fasihi ya Kiswahili. Makala imejikita katika kuchunguza ukiukaji wa kaida za mahali au mazingira, ukiukaji wa kaida kati ya mbali na karibu, ukiukaji wa kaida za kimawasiliano kwa kutumia lugha kati ya binadamu na viumbe wengine na ukiukaji wa kaida kati ya uhai na kifo
Nafasi ya Sheng katika Utangazaji wa Biashara Jijini Nairobi
Makala haya yanabainisha nafasi ya Sheng katika utangazaji wa biashara jijini Nairobi. Kichocheo cha utafiti huu kilikuwa kuwepo na chukulizi mpya kwamba Sheng imejitanzua kutoka kwenye upembezwaji na kuingia katika matumizi mapya yaliyo kinyume na chukulizi za awali kuwa ni lugha chafu na ya wahuni. Malengo yalikuwa kubainisha sababu ambazo zimefanya Sheng kutumika katika utangazaji wa biashara jijini Nairobi na kiwango cha matumizi yake katika utangazaji wa kibiashara jijini Nairobi. Nadharia mbili zimetumiwa kuchanganua data tuliyoipata nyanjani. Nadharia hizi ni ile ya Mchezo iliyoasisiwa na Neumann na Oskar Morgenstern (1944) na kuendelezwa na wasomi wengine kama vile Peter (2015) na Samuelson (2016), na Nadharia ya Maafikiano ya Mazungumzo iliyoasisiwa na Mwingereza Giles na wengine (1970). Tumetumia mbinu za mahojiano, kujaza hojajji, upigaji picha na uchunguzi shiriki ili kupata data tuliyolenga. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa Sheng hutumiwa zaidi na vijana kutangazia biashara jijini Nairobi kutokana na sababu mbalimbali. Isitoshe, imebainika kuwa nafasi ya Sheng katika utangazaji wa biashara jijini Nairobi hutegemea hadhira au wateja wanaolengwa hasa vijana, bidhaa zinazouzwa na sehemu ambako biashara inaendeshewa
Uamilifu wa Taashira katika Tamthilia za \u27Zilizala\u27 na \u27Sudana\u27
Makala haya yanahusu matumizi na uamilifu wa taashira katika tamthilia za Zilizala na Sudana. Katika makala haya matumizi ya taashira yalichunguzwa kupitia vyombo vya usafiri, hali za kimaumbile na miundomsingi. Makala haya yaliyojikita katika nadharia ya baada ya ukoloni yanaonyesha kuwa taashira imetumika katika tamthilia zilizopo kama mbinu ya kusana mambo yanayoathiri kitovu cha jamii. Haya ni pamoja na viongozi wa kiimla, ufisadi, ukabila na ubinafsi. Aidha, yanaeleza kuwa taashira imetumika vyema katika tamthilia hizi madhali imesaidia waandishi kuepuka uwezekano wa kusawiri masuala yanayokumba jamii paruwanja, jambo ambalo lingenyima kazi zenyewe mvuto. Badala yake imeonyeshwa kuwa waandishi walifinyanga lugha na kuyasawiri masuala ya kawaida kwa namna ngeni na ya kutendesa kupitia taashira. Yanadhihirisha tadi na inda zinazotumiwa na baadhi ya watawala katika mataifa yanayoinuka kiuchumi kujinufaisha kibinafsi pamoja na vikaragosi wao. Isitoshe, makala haya yamedhihirisha jinsi viongozi wa mataifa hayo hudhibitiwa na watawala katika mataifa yaliyoinuka kiuchumi na kusababisha ufukara wa raia katika mahusiano yanayofichika katika istilahi ya kitasfida ya utandawazi
Miundo ya Viegesho vya Kiwango katika Sentensi za Kiswahili: Mtazamo wa Nadharia ya Eksibaa
Makala yanahakiki viegesho vya kiwango katika sentensi za Kiswahili. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili, ushuhudiaji na usomaji matini ambazo zilihusu ubainishaji wa viegesho vya kiwango. Nadharia ya Eksibaa iliyoasisiwa na Chomsky (1970) imetumiwa kubainisha na kuchambua miundo ya viegesho hivyo. Data zimechanganuliwa kwa kutumia mbinu ya vielelezo vya mchoroti pamoja na maelezo. Matokeo yanadhihirisha kuwa kisintaksia, kuna miundo kumi na nne (14) ya viegesho vya kiwango katika sentensi za Kiswahili. Miundo hiyo imetokana na ushikamani wa viambajengo vinavyounda viegesho vya kiwango katika Kiswahili
Mielekeo ya Watoaji na Wapokeaji wa Huduma za Afya kuhusu Matumizi ya Kiswahili katika Uga wa Afya Mkoani Dodoma
Makala haya yanalenga kuchunguza mielekeo ya watoaji na wapokeaji wa huduma za afya kuhusu matumizi ya Kiswahili katika huduma za afya. Data ilikusanywa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya nne za mkoa wa Dodoma nchini Tanzania ambazo ni: Bahi, Kongwa, Chamwino na Dodoma. Data zimechanganuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Vitendo Vilivyofikiriwa ya Azjen na Fishbein ya Mwaka 1980. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba watoaji na wapokeaji wa huduma za afya ambao ni madaktari, wahudumu wa mapokezi, wagonjwa pamoja na wajawazito wana mielekeo chanya na hasi kuhusu matumizi ya Kiswahili katika huduma za afya. Mielekeo chanya ya juu kabisa ni 98.86% kwa kategoria ya wajawazito na mielekeo hasi ya juu kabisa ni 26.4% kwa madaktari. Kwa ujumla, kiwango cha chini kabisa cha mielekeo chanya na kiwango cha juu kabisa cha mielekeo hasi vyote vilidhihirika kwa madaktari. Sababu za mielekeo chanya ni pamoja na kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa, hivyo, inaelekea kuwa na watumiaji wengi wa lugha. Baadhi ya sababu za mielekeo hasi ni pamoja na kasumba za wasomi kudharau Kiswahili. Makala haya yanapendekeza kuwa mchakato wa kubadili mielekeo ya lugha hasa kwa madaktari ufanywe kwa masilahi mapana ya watumiaji wa huduma za afya
Utambuzi, Hisia na Mabadiliko ya Kisemantiki ya Leksia za Kiswahili
Makala haya yamejadili nafasi ya utambuzi na hisia katika mabadiliko ya kisemantiki ya leksia za Kiswahili. Makala yanaonyesha namna maarifa katika utambuzi hujenga msingi na kuongoza mbinu na taratibu mbalimbali za mabadiliko ya kisemantiki na hatimaye kuchangia katika mabadiliko ya maana. Mifano mahususi ya leksia kutoka Kiswahili cha kabla ya Karne ya Ishirini na cha Karne ya Ishirini na Moja imelinganishwa kudhihirisha mabadiliko husika. Asili ya data ni matini teule za kabla ya Karne ya Ishirini, matini za kilekskografia za Karne ya Ishirini na Moja na kutoka kwa wazungumzaji wa pwani ya Kenya wenye elimu-asilia. Nadharia ya Semantiki Tambuzi imezingatiwa. Imebainisha kuwa tajriba na maarifa yaliyofichamwa kwenye utambuzi huwa nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya maana za leksia. Imegunduliwa kuwa kila kuchao utambuzi huzidi kupanuka kiupeo, kufinyika na kugeuka pindi jamii nzima inavyobadilika kutokana na maendeleo ya sayansi, teknolojia, uchumi, jamii na siasa. Kadhalika fasili tofauti za dhana moja, usisitizo na kuipa dhana kipaumbele ni maswala ya kiutambuzi yachangiayo kuleta mabadiliko ya lugha. Makala haya pia yamedhihirisha mchango na ufaafu wa vigezo vya kiutambuzi vya nadharia ya Semantiki Tambuzi katika kuelezea mabadiliko ya lugha
Of Worlds and Artworks: An Introduction
… in the poetics of Relation, one who is errant (who is no longer traveler, discoverer, or conqueror) strives to know the totality of the world yet already knows he will never accomplish this—and knows that is precisely where the threatened beauty of the world resides (Glissant, 1997, p. 20)
Dhima ya Methali za Kiswahili kwa Jamii za Kenya ni Nini?
Methali hutokana na utamaduni wa watu na hutumika katika kuibulia na kuelekezea busara ya wenyeji. Aidha, methali za Kiswahili zimeshirikisha methali za jamii mbalimbali za Afrika Mashariki. Kwa sababu hii, zina mtazamo unaovuka mipaka ya jamii moja. Kwa sababu hii, ni mwavuli unaohifadhi na unaoibulia utamaduni asilia wa wenyeji. Methali hizo hutekeleza dhima ya uashiriaji, uelezaji na uelekezaji kuhusu maisha kwa kuzingatia ‘undani’ na ‘upana’ wa Wakenya kama jamii moja. Data ya makala hii ilitokana na methali zilizohifadhiwa katika vitabu vya methali za Kiswahili zilizokusanywa kutoka kwa wanajami wa Kenya. Methali hizo zilipata maelezo ya wanajamii wa Wakenya. Kadhalika, wataalamu wa lugha na wahakiki wa fasihi walihojiwa ili kupata fasiri za kijumla kuhusu methali. Katika uchanganuzi wa data, nadharia ya Semiotiki imetumika kubainishia viashiria na viashiriwa vya kitamaduni katika jamii za Wakenya. Kwa hivyo, makala hii inaeleza namna methali hizo zinavyoweza kutumiwa kwa ufaafu zaidi kwa jamii za Kenya
Wahusika wa Kiuhalisiamazingaombwe na Usawiri wa Mivurugo ya Kijamii katika \u27Babu Alipofufuka\u27 (2001), \u27Dunia Yao\u27 (2006) na \u27Bina-Adamu!\u27 (2002)
Makala haya yanahakiki wahusika wa kiuhalisiamazingaombwe na namna wanavyowasilisha mivurugo ya jamii katika riwaya za Babu Alipofufuka (2001) na Dunia Yao (2006) za Said Ahmed Mohamed, na Bina-Adamu! (2001) ya Kyallo Wamitila. Makala yalibaini kuwa wahusika wa kiuhalisiamazingaombwe wanatumia njia zisizo za kisayansi wala urazini kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwasiliana baina yao. Aidha, wahusika wana nguvu za kimazingaombwe zinazowafanya kufanya kazi mbalimbali kwa urahisi. Kwa ujumla, wahusika wana sifa za kimazingaombwe zinazokaidi kaida za Aristotle na Plato. Makala haya ni muhimu kkatika kuelewa matumizi ya mitindo ya uhalisiamazingaombwe na namna inavyowasilisha mivurugo ya jamii