Moi University Journals
Not a member yet
344 research outputs found
Sort by
Artwork or Artifact: Reframing Objects within Ethnographic Museums
In this article, I reflect on the reframing of objects in museums. In a Western context, objects of African provenance seem to oscillate between being categorized as artworks and as artifacts. My main objective is to delineate how these categories were historically distinguished, and what contributed to that process. By examining current exhibitions, I demonstrate that this legacy adds a problematic dimension to contemporary museum displays. The problem is, firstly, that only these two categories exist; and secondly, that the distinction between these categories is still linked to distinct display practices that carry on a colonial legacy. This article thus contributes to the discussion of the current transformation of ethnographic museums into postcolonial museums of global art history
Mapendekezo ya Kiuboreshaji dhidi ya Uibukaji wa U-Nigeria katika Tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania
Imebainika kuwa tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya wa Kiswahili nchini Tanzania imetekwa na utamaduni wa nje hususani wa Kinigeria (Mrikaria, 2007; Kasiga, 2022). Athari zake zimebainika katika vipengele kadhaa vya kibunifu (Kasiga, 2021). Pia, misukumo mbalimbali inayowasukuma wasanii kutumia U-Nigeria imebainishwa (Kasiga, 2022). Kimsingi, hali hii inatishia utambulisho wa Kitanzania katika sanaa. Hivyo, makala hii imetoa mapendekezo ya kiuboreshaji dhidi ya U-Nigeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania. Mapendekezo yalitolewa yamehusisha kufanyika uwekezaji wa muziki wa asili wa Kitanzania, kufanyika kwa usimamizi maalumu katika vyombo vya habari, kuwepo kwa sheria na kanuni za kulinda uasili wa muziki wa kizazi kipya, na uanizhwaji wa semina, warsha pamoja na madarasa maalumu kwa wasanii. Pia, makala imependekeza kuwepo kwa agenda mahususi ya kitaifa kujenga uzalendo, kumakinikia mitindo ya sanaa za Kitanzania katika utengenezaji wa muziki, kuharakisha upatikanaji wa vazi la taifa, kuanzishwa kwa vipindi vya uchambuzi wa nyimbo, na wasanii kushawishiwa kutumia mandhari ya Kitanzania katika video zao. Vilevile, imependekezwa kuanzishwa kwa matamasha na tuzo za muziki, asasi za elimu kutengeneza mitaala ya biashara, lugha ya Kiswahili, na utamaduni wa Kitanzania, na kuwe na muumano kati ya biashara, utamaduni na teknolojia
Mtazamo wa Kijumla kuhusu Ushairi wa Kiswahili nchini Kenya: Mifano kutoka Pwani na Bara
Kwa karne nyingi, ushairi umekuwa umekita mizizi katika sehemu za pwani ya Kenya hasa maeneo ya Lamu. Ushairi huu ulifika mpaka sehemu za bara, mahali ambapo Kiswahili kilitumika kusambazia biashara na dini. Hata hivyo, bado hakukuwa na kazi za ushairi za watu wa bara hadi miaka ya kukaribia kipindi cha uhuru katika sehemu za Afrika Mashariki. Japo Kiswahili sasa kinatumika kote nchini Kenya, katika makala hii tuaangalia washairi wa kutoka maeneo haya mawili. Aidha, tutabainisha sifa zinazobainisha ushairi huu wa sehemu hizi mbili; yaani unavyofanana na kutofautiana katika sifa zake za kimaudhui na kimtindo. Vilevile, tutaangalia tofauti za watunzi, lugha wanayoitumia na maswala yanayowashughulisha katika ushairi huu. Mbinu kubwa tuliyotumia ni utafiti wa maktabani uliotuwezesha kupata vitabu na rekodi nyingine. Matokeo muhimu yanabainisha kuwa, washairi wa pwani, hawawezi kuepuka athari ya dini ya Kiislamu katika utunzi wao. Pia, tulibaini kwamba, washairi wa pwani walitumia lahaja zao. Swala lingine muhimu tulilolibaini ni kuwa, washairi wa kike ni wachache sana na hata idadi ya machapisho yao yanapatikana kwa uchache sana nchini Kenya
Dhana ya Utendaji na Dhima Yake katika Tamthilia ya \u27Kitumbua Kimengia Mchanga\u27
Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya utendaji iliyoasisiwa na Wallace Bacon ili kubainisha ikiwa tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga iliyoandikwa na Mohamed (2000) imezingatia kigezo kikuu katika matini za kidrama ambacho ni uwezo wa kuwasilishwa jukwaani au ni majibizano ya usemi tu. Katika utafiti huu tumevitathmini vipengele vinavyochochea na kufanikisha utendaji wa tamthilia kwenye jukwaa. Maelekezo ya jukwaa, mandhari, maleba, miondoko, sauti, uangazaji, kimya na mihimili ni vipengele vya utendaji ambavyo huwawezesha waigizaji kuwasilisha ujumbe wa mwandishi kwenye jukwaa. Utafiti huu umejaribu kubainisha jinsi vipengele hivi vinavyofanikisha uwasilishaji wa ujumbe kwenye jukwaa na pia kutaja kwa ufupi dhima zinazofungamana na matumizi ya vipengele hivi. Utafiti huu ulihusisha kusoma makala na kutumiwa kama data ya utafiti huu ambayo baadaye ilichanganuliwa na mwishowe kuelezea matokeo kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu pia ulihusisha ukusanyaji wa data moja kwa moja kutoka maktabani. Mahali pa utafiti palikuwa ni maktaba katika vyuo vikuu pamoja na maktaba ya kitaifa nchini Kenya na kundi lengwa lilikuwa tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga. Inatarajiwa kuwa utafiti huu utakuwa mchango mkubwa kwa jamii ya wasomi hasa wanaoshughulikia utendaji na vipengele vya kidrama katika fasihi andishi
Changamoto Zinazokabili Umiliki na Matumizi ya Ardhi Barani Afrika: Udurusu wa Riwaya Tatu za Karne ya 21
Makala haya yanachanganua suala la changamoto zinazokabili umiliki na matumizi ya ardhi barani Afrika kama lilivyosawiriwa katika riwaya za karne ya ishirini na moja, kwa kurejelea riwaya za Chozi la Heri (2014), Msimu wa Vipepeo (2009) na Nakuruto (2006). Ardhi ni miongoni mwa rasilimali muhimu katika maisha ya binadamu hasa katika uzalishaji mali. Huwa chanzo cha mahitaji ya kimsingi kama vile chakula na makaazi. Aidha, uwezo wa kumiliki ardhi huwa ni sifa kuu ya maendeleo na mabadiliko mengi katika jamii ambayo yamewahi kushuhudiwa duniani. Tungo za kifasihi tulizoziteua kimakusudi zilifanikisha utafiti huu kwa sababu fasihi huwa imefungamanishwa kibunifu na maisha halisi ya binadamu. Sifa kuu ya riwaya hizi ni kwamba zimeliangazia suala la ardhi kwa mapana. Isitoshe, zimetungwa katika kipindi cha karne ya ishirini na moja ambacho utandawazi umeenea na kuimarika barani Afrika. Ili kufanikisha udurusu huu, tuliligawa suala letu la utafiti katika sehemu tatu kuu: kipindi cha kabla ya ukoloni, kipindi cha ukoloni na kipindi cha utandawazi. Uchanganuzi matini huu wa kimaktaba uliongozwa na nadharia ya Baada-ukoloni. Umuhimu wa makala haya unatarajiwa kuwa pamoja na kudhihirisha mitazamo ya watunzi mbalimbali kuhusu changamoto katika umiliki na matumizi ya ardhi barani Afrika; pamoja na mapendekezo ya namna za kuzitatua. Tunatarajia kutoa mchango wa kitaaluma kuhusiana na suala hili hivyo kuwafaa watafiti wa baadaye na watunga sera zinazohusiana na suala la umiliki na matumizi ya ardhi barani Afrika
Uhalisiamazingaombwe katika Riwaya za Shaaban Robert: \u27Kusadikika\u27 na \u27Kufikirika\u27
Uhalisiamazingaobwe ni mkondo wa usasa leo. Ni mkondo uliochipuka huko Amerika ya Kusini miaka ya 1960 licha ya kwamba dalili zake zilikuwako kabla katika hekaya na fasihi simulizi za mataifa mengi zikiwemo za fasihi ya Kiafrika na Kiswahili (Mulokozi, 2017). Abrams (1999) anaeleza kuwa nadharia hii ilianza miaka ya 1920 ambayo mwanzoni ilitumika kuhusu wachoraji na baadaye katika bunilizi za kinathari Bunilizi za kinadhari za Jorge Luis Borges (1899-1986) wa Argentina, na halikadhalika kazi za waandishi kama vile Gabriel García Marquez (1927-2014) wa Kolombia, Isabel Allende wa Chile, Günter Grass (1927-2015) Mjerumani, Italo Calvino wa Italia, na John Fowles (1926-2005) wa Uingereza. Kutokana na mawazo hayo ndipo tunapata kujiuliza maswali kuhusu chimbuko la nadharia hii katika fasihi ya Kiswahili ni lipi hasa? Kusema Kezilahabi ni mwasisi wa mkondo huu ni sawa? Ilihali kulikuwa na kazi za Shaaban Robert zenye vimelea vya nadharia hii. Kutokana na mawazo ya wataalamu mbalimbali tunaona kuna haja ya kuchunguza endapo riwaya za Shaaban Robert zina Uhalisiamazingaobwe au la. Katika uchambuzi huu tutajikita katika kuchunguza riwaya mbili ya Kusadikika na Kufikirika. Riwaya ya Adili na Nduguze itatumika pale tu itakapobidi
Usimulizi katika Ushairi wa Kithaka wa Mberia
Kithaka wa Mberia ni mtunzi wa mashairi huru. Ametunga diwani kadhaa za mashairi huru yenye maudhui anuwai na masuala ibuka. Katika kuangazia maudhui mbalimbali katika ushairi wake, ametumia mbinu ya usimulizi katika baadhi ya mashairi katika diwani zake. Usimulizi unatumika sana katika utambaji wa hadithi katika fasihi simulizi na katika tanzu za riwaya na hadithi fupi katika fasihi andishi. Ni nadra sana usimulizi kutumika katika ushairi. Ingawa tenzi ndizo zinahusishwa na usimulizi kama vile katika Utenzi wa Fumo Liyongo (1913), inawezekana mashairi mafupi yakawa na sifa ya usimulizi kama tunavyoona katika mashairi ya Kithaka wa Mberia. Katika makala haya, tunajadili aina za usimulizi katika baadhi ya mashairi yake katika diwani zake nne ambazo ni: Mchezo wa Karata (1997), Bara Jingine (2001), Redio na Mwezi (2005), na Rangi ya Anga (2014). Matumizi haya ya mtindo wa usimulizi ndiyo yanayoupa ushairi wake ubunifu mpya, usasa na upekee fulani
Mbinu, Dhima na Athari za Kumuanika Nje Mfiwa katika Utendaji wa Utani wa Wahehe
Utani ni kipera cha mazungumzo/nyambi katika fasihi simulizi chenye dhima mbalimbali kwa jamii husika. Lengo la makala hii ni kuchunguza mbinu, dhima na athari za kumuanika nje mfiwa katika utendaji wa utani wa Wahehe. Maswali tunayojibu ni: Je, ni utani upi unaojitokeza wakati wa kumuanika nje mfiwa? Nini dhima na athari ya utendaji huo wa utani kupitia mbinu ya kumuanika nje mfiwa? Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji wa misiba na kuchambuliwa kwa kutumia Nadharia ya Utendaji na Uamilifu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa mbinu ya kumuanika nje mfiwa pindi anapopatwa na msiba hufuata hatua kadhaa wakati wa utendaji wa utani. Utendaji wa utani huo kupitia mbinu ya kumuanika nje mfiwa huwa na dhima kama vile; kudumisha umoja na ushirikiano, kupunguza majonzi kwa wafiwa, kuilinda amali hii muhimu ya utani miongoni mwa wanajamii, kuonya na kuburudisha. Makala hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu; utangulizi, kiini na hitimisho. Utangulizi unaeleza kwa ujumla dhana ya utani pamoja na nadharia zilizotumika. Kiini kinaelezea mbinu, dhima na athari za kumuanika nje mfiwa katika utendaji wa utani wa Wahehe. Sehemu hii imefuatiwa na mbinu za kiutendaji wa utani wakati wa kumuanika nje mfiwa, dhima, athari zake na mwisho hitimisho
East African Detective Fiction: A Basic Anatomy
This paper provides a basic survey of the current state of the Swahili detective prose. The paper highlights some thematic and formal features that distinguish the East African detective prose. To foreground the basic features of the Swahili detective prose, the generic theory has been utilized. Data was collected through library research by reading primary texts on Swahili detective while secondary data was taken from critical works such as theses and academic papers. This data was analyzed qualitatively by extracting salient features in each text. The paper too highlights some of the factors responsible for the growth and popularity of the detective genre in the East African region. The researchers found out that some of the factors for the rapid growth and popularity of this genre are their use simple plots, attractive language, and the character of the detective figure among others
Ulinganishi wa Kiisimu wa Lugha za Kiswahili na Kiarabu
Makala haya yanalinganisha vipengele vya kiisimu baina ya lugha za Kiswahili na Kiarabu ili kubaini iwapo lugha hizi zina asili moja au la. Itakumbukwa kwamba mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1970 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam palijitokeza mijadala iliyozusha mabishano na malumbano ya kitaaluma kuhusu asili na chimbuko la lugha ya Kiswahili. Kuna waliodai kuwa lugha ya Kiswahili ilitokana na lugha ya Kiarabu na wengine wakaeleza kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu (Massamba, 2007). Ushahidi wa kila upande uwe na mashiko au usiwe na mashiko ulitolewa, lakini ulinganishi wa kiisimu wa lugha hizi bado haujafanyika. Kwa sababu hiyo ndipo tukaamua kulinganisha isimu ya lugha mbili hizi. Data ya uchunguzi huu imekusanywa kutoka maktabani ambapo mwandishi amepitia maandiko na machapisho mbalimbali yanayohusiana na kazi hii. Matokeo ya uchunguzi huu yanabainisha kuwa lugha ya Kiswahili haitokani na Kiarabu. Kwa sababu katika vipengele vitano vya kiisimu tulivyovilinganisha katika makala haya, vyote vinaonesha kuwa lugha hizi zinatofautiana kiisimu. Vipengele vilivyolinganishwa ni msamiati wa msingi, fonolojia, mofolojia, sintaksia na mfumo wa ngeli. Kutokana na tofauti hizo tunaweza kuhitimisha kuwa lugha hizi hazina asili wala mnasaba mmoja