20 research outputs found

    Tamathali za Usemi na Taswira katika Utenzi wa \u27UKIMWI ni Zimwi\u27

    No full text
    Utenzi wa UKIMWI ni Zimwi ni kazi iliyotungwa na Mahmoud Abdulkadir wa Lamu katika mwaka wa 2001. Huu ni utenzi ambao mwandishi aliutunga kwa lengo la kuwajuza watu athari za janga la UKIMWI. Utenzi huu umeandikwa katika lahaja ya Kiamu. Maudhui na dhamira ya kazi ya fasihi haziwezi kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya kuwako kwa lugha. Matumizi ya lugha ni mapana kwani huhusisha tamathali za usemi, uteuzi na mpangilio wa maneno basi, sajili za lugha, matumizi ya nahau na misemo n.k. Katika makala haya, ninashughuliki hasa matumizi ya tamathali za usemi na taswira katika utenzi wa UKIMWI ni Zimwi

    Politeness among The Swahili of Mombasa: A Family Perspective

    No full text
    This paper discusses politeness strategies within the Swahili community of Mombasa. It focuses on households and specifically on wife and husband interactions to discover what strategies are used and how effective they are. This paper argues that wives and husbands in Swahili households hold mutual feelings and affections that each must mind in communication. The paper uses the Politeness Principle (1978) that looks at politeness on a minimum maximum politeness scale in the relationship between speaker (self) and hearer (other). The six maxims proposed by Leech are discussed and it is shown how they guide a marriage to make it stable, fruitful and friendly, eventually a polite institution. Often in the Mombasa family units, requests are made indirectly and so are corrections. Affective use is also used to make the interactions fruitful. Politeness between the husband and wife seems to rest on a power balance where more politeness is expected of a wife

    Analyzing the Impact of Slavery on the Construction of Self and Gender Identities in M. S. Mohamed’s Novels

    No full text
    The objective of this paper is to analyze and evaluate the impact of slavery on the mapping and construction of self and gender identities in Mohamed S. Mohamed Kiu (1972) and Nyota ya Rehema (1976). The study will use a composite approach comprising New Historicism, Gender Criticism and Stylistics. New Historicism helped to situate and map the works analyzed in relation to particular Zanzibarian epochs. Gender criticism was expended in interrogating how women and men in feudal Zanzibarian society related with each other at all levels of social interaction and the impact on their self and gender identities. Finally, stylistics was used to interrogate and evaluate the dominant structural and stylistic features of the choice texts and their impact on the study topic. The study was guided by two hypotheses, viz, that in feudal Zanzibarian society, racialism and the dominant ideologies (patriarchy and Islam), impacted negatively on self and gender identities of both female and male members of society. Secondly, this study contends that, the stylistic devices used in each one of the choice texts, were important in delineating the mapping and construction of self and gender identities

    Wanawake Wachukua Hatua Nyingine: Analyzing Women’s Identities in Kiswahili Short Stories

    No full text
    Wataalamu mbalimbali wamefafanua dhana ya hadithi fupikwa namna mbalimbali. Kipera hiki cha fasihi andishi ni zao la athari za kimagharibi. Hadithi za fasihi simulizi zimerutubisha hadithi fupi zinazoendeleza majukumu ya tangu jadi ya kuelimisha, kuongoza, kuonya na kuburudisha. Hadithi fupi ya kisasa ina sifa za matumizi ya lugha ya nathari, masimulizi mafupi aghalabu ya tukio moja, mhusika mkuu mmoja au wahusika wachache, msuko sahili na hatimaye mshikamano na umoja wa mawazo na mtindo. Katika makala haya, tunachambua hadithi teule za Kiswahili kuhusu nafasi na ujitambuzi wa wanawake. Kachukua Hatua Nyingine ya Kyallo Wadi Wamitila inajadili hatua ambazo mwanamke anafaa azichukue ili ajikwamue na utumwa wa ndoa zinazompa mwanamume uwezo wote. Nayo Ngome ya Nafsi ya Clara Momanyi inaonyesha hatua anazochukua mtoto msichana kujikomboa dhidi ya mila na desturi zinazomnyima utambulisho wa kibinafsi na kijinsia. Wasia wa Baba ya Ahmad Kipacha inaonyesha jinsi utamaduni na mafundisho chanya ya dini kuwa njia mwafaka za kujengea utambulisho wa mwanamke. Hatimaye Usia wa Mama ya Fatima Salamah inaonyesha mtoto msichana akijihami kupitia utamaduni na mafundisho chanya ya dini dhidi ya ushawishi hasi wa mamake

    Mtazamo wa Kijumla kuhusu Ushairi wa Kiswahili nchini Kenya: Mifano kutoka Pwani na Bara

    No full text
    Kwa karne nyingi, ushairi umekuwa umekita mizizi katika sehemu za pwani ya Kenya hasa maeneo ya Lamu. Ushairi huu ulifika mpaka sehemu za bara, mahali ambapo Kiswahili kilitumika kusambazia biashara na dini. Hata hivyo, bado hakukuwa na kazi za ushairi za watu wa bara hadi miaka ya kukaribia kipindi cha uhuru katika sehemu za Afrika Mashariki. Japo Kiswahili sasa kinatumika kote nchini Kenya, katika makala hii tuaangalia washairi wa kutoka maeneo haya mawili. Aidha, tutabainisha sifa zinazobainisha ushairi huu wa sehemu hizi mbili; yaani unavyofanana na kutofautiana katika sifa zake za kimaudhui na kimtindo. Vilevile, tutaangalia tofauti za watunzi, lugha wanayoitumia na maswala yanayowashughulisha katika ushairi huu. Mbinu kubwa tuliyotumia ni utafiti wa maktabani uliotuwezesha kupata vitabu na rekodi nyingine. Matokeo muhimu yanabainisha kuwa, washairi wa pwani, hawawezi kuepuka athari ya dini ya Kiislamu katika utunzi wao. Pia, tulibaini kwamba, washairi wa pwani walitumia lahaja zao. Swala lingine muhimu tulilolibaini ni kuwa, washairi wa kike ni wachache sana na hata idadi ya machapisho yao yanapatikana kwa uchache sana nchini Kenya

    Uchanganuzi Linganishi wa Suala la Maadili kwa Vijana wa Kiume katika Tenzi Mbili: \u27Siraji\u27 na \u27Adili\u27

    No full text
    Makala hii imeshughulikia maadili kwa vijana wa kiume yanayojitokeza katika tenzi za Siraji na Adili. Katika uchunguzi huu tumeongozwa na nadharia ya maadili ambayo inalenga kazi za fasihi kutatua matatizo ya jamii kwa njia ipasavyo na kujenga jamii bora yenye maelewano. Malengo ya uchunguzi wetu ni kulinganisha jinsi ambavyo watunzi Kijumwa na Robert wamelishughulikia suala la maadili kwa vijana wa kiume katika tenzi Siraji na Adili na hatimaye kubaini sababu za kuwiana kwao. Baada ya kusoma na kuzichambua tenzi- Siraji na Adili tumebaini ya kwamba watunzi Kijumwa na Robert wamewiana kwa jinsi wamelishughulikia suala la maadili kwa vijana wa kiume. Tumeweza kuonyesha kwamba tenzi hizi zina uhusiano wa karibu sana kwa sababu watunzi Kijumwa na Robert wameyafungamanisha maadili hayo na mafunzo ya dini ya Kiislamu ndiposa tukachanganua data yetu kwa njia ya maelezo na ufafanuzi huku tukitoa thibitisho kutoka kwa tenzi- Siraji na Adili pamoja na Kurani Takatifu. Ni matumaini yetu kwamba makala haya yatachangia pakubwa katika taaluma ya kiusomi kwa kuendeleza fasihi andishi

    Utafiti wa Lahaja Kupitia Macho ya Jamii: Matumizi ya Mtazamo Tambuzi wa Elimu Lahaja Katika Kaunti ya Lamu

    No full text
    Utafiti huu unachunguza uainishaji wa mipaka ya lahaja za Kiswahili zinazozungumzwa katika Kaunti ya Lamu, Kenya, kwa kutumia nadharia ya Mtazamo Tambuzi wa Elimu Lahaja (Preston, 1989). Tofauti na tafiti za awali zilizozingatia vipengele vya kimuundo vya lugha, utafiti huu umejikita katika maoni, mitazamo, uelewa na hisia za wasemaji wazawa kama vigezo halali vya kutambua na kuainisha lahaja. Kwa kutumia mbinu ya uchoraji wa ramani za mikono, sauti zilizorekodiwa, na mijadala ya vikundi, washiriki waliainisha maeneo ya lahaja kwa msingi wa tajriba zao binafsi. Data hiyo ilichakatwa kwa kutumia teknolojia ya GIS (QGIS na ArcGIS) kwa njia ya Kernel Density Estimation (KDE). Matokeo yameonyesha kuwepo kwa makundi makuu manne ya lahaja: Kiamu, Kipate, Kisiu na Kitikuu, huku Kishela na Kimatondoni zikiwa kwenye hatari ya kufifia kutokana na ushawishi wa Kiamu. Aidha, vipengele vya kifonolojia, kimofolojia na kisintaksia vilijitokeza kuwa msingi wa utambuzi wa tofauti hizo. Imebainika kuwa asili ya mzungumzaji, uzoefu wa lugha, na uhusiano wa kijamii ni vigezo muhimu vinavyoathiri namna wanavyotambua na kuchora mipaka ya lahaja. Utafiti huu unatoa mchango mpya kwa taaluma ya isimu-jamii na lahaja kwa kusisitiza umuhimu wa data tambuzi kutoka kwa jamii, na hivyo kupanua upeo wa utafiti wa lugha za Kiafrika kutoka katika mtazamo wa jamii kuelekea usomi wa kitaalum

    Changamoto za Kuueleza Msamiati wa Samaki: Mtazamo wa Kiuhusiano

    No full text
    Makala haya yanachunguza maelezo ya majina ya samaki katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Kwa kutumia nadharia ya kiuhusiano imebainika kuwa kunatumika vichocheo au mikakati tofauti tofauti ili kumweleza samaki. Hata hivyo, licha ya vijenzi hivi kutumika bado kuna changamoto nyingi kama vile maelezo fulani kukosa uangavu kwa kuwa ni mapana zaidi au kutochangia kikamilifu katika kumweleza samaki kwa kuwa ni maelezo finyu, kutotumia vichocheo vya kutosha au kichocheo kimoja ambapo vichocheo vingi vingefaa zaidi. Aidha, imebainika kuwa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) imetumia vichocheo vya tabia, chakula, rangi, umbo, vumba na hata picha ili kuwaeleza aina ya samaki ili wasomaji waweze kuwatambua na kuwaeleza. Licha ya vichocheo hivi, ni wazi kuwa KKS bado inakabiliwa na changamoto ya kuwaeleza samaki kwa uwazi, uangavu na kwa kukinaisha

    Uamili wa Ufokasi katika Kudhihirisha Itikadi

    No full text
    Makala haya yanachunguza ngazi ya itikadi na uamilifu wake katika riwaya teule za Kiswahili kupitia kwa ufokasi.  Riwaya teule ni Haini (Adam Shafi, 2003), Makuadi wa Soko Huria (C. Chachage, 2005), Harufu ya Mapera (K. Wamitila, 2012), Hujafa Hujaumbika (F. Kagwa, 2018), Ndoto ya Almasi (Ken Walibora, 2006) na Nyuso za Mwanamke (S. Mohamed, 2010). Ngazi ya itikadi ni mojawapo ya ngazi mbalimbali za ufokasi zilizopendekezwa na wananaratolojia. Kimsingi, ufokasi ni mkabala ambao huchukuliwa katika kuwasilisha simulizi na kuikuza hadithi kwa ujumla. Data ya kuudhibiti na kuthibitisha madai ya mjadala wetu imetolewa katika  riwaya teule.  Uteuzi wa riwaya hizi unahalalishwa kwa misingi kwamba, hizi ni riwaya zilizo na matini pana zinazowezesha udondoaji wa mifano faafu inayodhihirisha ngazi ya itikadi na wakati huo huo kudhihirisha uamili wa ngazi hiyo katika simulizi. Mjadala wa kimsingi katika makala haya umekitwa na kuongozwa na teneti za kimsingi za nadharia ya naratolojia ambayo inatambua ufokasi kama kipengele muhimu katika uwasilishaji wa simulizi. Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa, kupitia kwa ufokasi nje na ndani, waandishi wa riwaya teule wamedhihirisha ngazi ya itikadi. Imebainika kuwa wahusika mbalimbali huwa na tabia, mitazamo, misimamo na hisia fulani kuhusu masuala mbalimbali kutokana na athari za itikadi zinazotawala mazingira au matamanio ya
    corecore