3 research outputs found

    Utekelezaji wa Mitalaa ya Kiswahili Vyuoni na Namna Unavyoathiri Utendakazi wa Walimu Wanaofundisha katika Shule za Upili

    No full text
    Walimu wanaofundisha katika shule za upili hupata mafunzo yao ya kitaaluma kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali. Wanapoandaliwa vyuoni, walimu hawa hupewa mafunzo kwa kutumia mitalaa tofauti inayoandaliwa katika vyuo vikuu hivyo. Baada ya kuhitimu, wao hutarajiwa kuutekeleza mtalaa mmoja unaoandaliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitalaa nchini Kenya (TUMIKE) ili ufundishwe katika shule zote za upili. Utafiti ulifanywa ili kudhihirisha iwapo mafunzo ya kitaaluma yanayotolewa vyuoni kuwaandaa walimu wa somo la Kiswahili yanawapa maarifa na stadi wanazohitaji kufundisha katika shule za upili baada ya kuhitimu. Makala haya yametokana na utafiti uliofanywa ili Kutathmini uhusiano baina ya mitalaa ya Kiswahili inayotumika katika vyuo vikuu vya umma nchini  Kenya na mtalaa ambao umeandaliwa na TUMIKE ili kutekelezwa katika shule za upili. Utafiti ulifanyika katika vyuo vikuu vitano vya umma nchini Kenya. Muundo wa utafiti ulikuwa usoroveya elezi. Data ilikusanywa kwa njia ya usaili, uchanganuzi wa nyaraka na hojaji. Uchanganuzi wa data ulikuwa wa kitakwimu na kimaelezo. Utafiti uligundua kuwa uhusiano baina ya mitalaa rasmi ya Kiswahili ya vyuo vikuu vya umma na mtalaa wa Kiswahili wa shule za upili siyo wa moja kwa moja. Hali hii iliathiri utendakazi wa walimu walipotekeleza mtalaa wa shule za upili. Uhusiano mdogo uliopo baina ya mitalaa rasmi ya vyuo vikuu na mtalaa rasmi wa TUMIKE ulidhihirika kwa kuchunguza vipengele vikuu vya mtalaa ambavyo ni: malengo, mada, utekelezaji na tathmini. Utafiti unapendekeza pafanyike marekebisho ya mara kwa mara ya mtalaa wa TUMIKE kwa kuwahusisha walimu na waandalizi wao ili wakadirie malengo, mada, mbinu za utekelezaji na tathmini mintarafu maandalizi yanayotolewa kwa walimu

    Tathmini ya Mfumo wa Swahilihub katika Ukuzaji wa Kiswahili Nchini Kenya

    No full text
    Swahilihub ni tovuti iliyozinduliwa katika mwaka wa 2012 kwa lengo la kukuza Kiswahili mtandaoni. Makala haya yalitokana na utafiti uliolenga kutathmini mradi wa Swahilihub katika ukuzaji Kiswahili. Ili kulifikia lengo hili, utafiti huu ulikusudia kubaini namna mfumo wa Swahilihub unavyochangia katika ukuzaji Kiswahili nchini Kenya. Mwelekeo mseto wa utafiti unaohusu matumizi ya mbinu za kimaelezo na kijarabati kwa pamoja ulitumika katika utafiti huu. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia uchanganuzi wa matini mtandaoni, mahojiano nyanjani pamoja na hojaji na mijadala miongoni mwa watumiaji wa Swahilihub katika baadhi ya vyuo vikuu nchini Kenya. Aidha utafiti huu ulitumia ARhefs na Similarweb ambavyo ni vifaa vya tathmini ya tovuti ili kutathmini viwango vya ukubalifu na ustahilifu wa Swahilihub miongoni mwa watumiaji wake. Data ya utafiti huu ilichanganuliwa kutokana na malengo ya utafiti na kuongozwa na mihimili ya Nadharia ya Msambao wa Uvumbuzi ya Rodgers (2003). Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia za maelezo, majedwali, picha, michoro na chati. Aidha utafiti huu ulizua tasnifu kuwa utanuzi wa teknolojia pamoja na ustawi wa Swahilihub ni nafasi nzuri ya uundaji wa dira ya ukuzaji endelevu wa lugha ya Kiswahili mtandaoni
    corecore