18 research outputs found

    The Pragmatic Import of Humorous Utterances in Kiswahili Buying and Selling Encounters

    No full text
    This paper analyses humour as a pragmatic resource that interactants draw on to promote interpersonal relations between themselves as they engage each other in the negotiation exercise. Humour is discussed as a pragmatic and strategic resource that the interactants tap in order to amicably transact, besides enhancing their solidarity and mutual understanding. They therefore position themselves as equals in the market encounter. Humour is one of the essential tools for exploring the ways in which market conversation achieves serious social effects, while appearing to be no more than ways of having a few laughs together. The author discusses humour in the context of the market negotiation where, the two parties engage each other in a relaxed talk. As such, the two parties interact as “free and equal individuals who are willing to construct a context in which they are free to engage each other in the transaction encounter in the way and manner that pleases them

    Uzingativu wa Yaliyoandikwa kuhusu Mada: Mifano kutoka Baadhi ya Tasnifu za Kiswahili

    No full text
    Makala haya yanajadili nafasi ya yaliyoandikwa kuhusu mada katika taaluma ya utafiti. Mwandishi anarejelea data au kazi mbalimbali za kitafiti katika viwango vya uzamili na uzamivu ili kutoa tahadhari kwa watafiti na wanataaluma wanapokuwa mbioni katika kutekeleza majukumu ya kitafiti. Mwandishi anajadili suala la mchango na manufaa ya utafiti kwa jamii hasa inapotokea kwamba utafiti unaohusika ni wa awali na haujawahi kufanywa na watafiti watangulizi. Makala yanajadili mustakabali wa utafiti katika taaluma za Kiswahili, huku akionyesha namna ya kujiepusha na changamoto zinazoendana na utafiti, katika mapana na marefu yake

    The Anarchy of Numbers: Understanding the Evidence on Venezuelan Economic Growth

    No full text
    This paper studies Venezuelan economic performance from 1950 to 1998. We show that there exist wide divergences in many commonly used estimates of GDP growth and discuss the sources of those differences. We show that the choice of base year and linking techniques are crucial for the diagnosis of economic growth, and argue that the aggregate GDP and TFP growth numbers are distorted by cuts in oil production that came about as a result of the country adopting the OPEC strategy of exploiting market power during the 1970s. We argue that non-oil growth and TFP numbers represent more adequate measures of economic performance and that, while far from satisfactory, these do not deviate significantly from those of other Latin American countries.Economic growth, National accounts, Growth accounting, Oil exporting economies, Latin America, Venezuela

    Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika katika Muktadha wa Utandawazi

    No full text
    Makala haya yanatalii masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika katika ulimwengu na malimwengu ya utandawazi. Kwa muda mrefu, wataalamu wengi wa masuala ya lugha na isimu wamekuwa mbioni katika kuuangazia uhusiano uliopo au unaopaswa kuwepo baina ya lugha na shughuli za kimsingi na maendeleo ya jamii. Mjadala huu hasa umekitwa kwenye mawazo na mikabala ambayo inahusiana moja kwa moja na nguvu na taratibu za utandawazi, ambapo inaaminika kwamba lugha zozote zile ambazo hazitumiwi katika shughuli na harakati za uzalishaji mali huenda zikamezwa na kusahauliwa kabisa hivi karibuni na utamaduni wa Kimagharibi ambao unajitokeza waziwazi katika harakati anuwai za kijamii kama vile uchumi, elimu, uvumbuzi na ugunduzi wa sayansi na teknolojia. Makala haya basi yanaonyesha namna Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika zinaweza kulindwa na kuhifadhiwa ili ziendelee kutumiwa na walio wengi katika shughuli zao za kila siku

    Kikale cha Kifo kama Mbinu ya Utunzi katika Fasihi ya Kiswahili

    No full text
    Makala haya yanachunguza tukio la hatima ya maisha ya kifo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likidhihirika na kutumiwa na watunzi katika kazi za sanaa hususani tamthilia. Kifo ni taashira kongwe ambayo imekuwepo katika kazi za sanaa za jamii zote ulimwenguni na katika vizazi na ustaarabu wa nyakati mbalimbali. Kifo kama kikale kimekuwa kikijitokeza mara kwa mara katika kazi za sanaa kwa njia ya kujirudia rudia kiasi kwamba kinajibainisha kama motifu ya utunzi wa kazi za fasihi inayoathiri muundo na dhamira za kazi hizo. Matokeo ya uchunguzi yanafafanua matumizi ya kifo kama mbinu ya utunzi wa tamthilia ya Kiswahili na kudhihirisha kifo kama kikale kinachojirudiarudia katika kazi za fasihi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhakiki wa vikale iliyoasisiwa na mtaalamu Northrop Frye (1957) kutoka Kanada

    Kisiwa cha Migingo: Diskosi Tepetevu

    No full text
    Makala haya yanaangaza diskosi tepetevu kama inavyojitokeza katika lugha iliyotumiwa na viongozi mbalimbali wa Afrika Mashariki kuhusiana na umiliki wa kisiwa cha Migingo. Wandishi wanajadili matumizi ya lugha ya viongozi hawa, hususan Rais Yoweri Museveni ambaye alidai kwamba pasina shaka, kisiwa cha Migingo kipo chini ya himaya ya Kenya ila maji yanayokizunguka yanamilikiwa na Uganda. Baadhi ya viongozi kutoka Uganda walidai kwamba hapakuwa na sababu ya upande wa Kenya kung’ang’ania mwamba au jiwe lisilozidi kipimo cha uwanja wa mpira. Matamshi haya yalizua mjadala mrefu sana kuhusiana na umiliki wa kisiwa hiki huku pande mbili zinazohusika zikishikilia misimamo mikali ambayo, pasina shaka yoyote, ingesababisha kutoelewana na pengine, machafuko ya kisiasa. Katika makala haya, tunauangazia mgogoro huu ndani ya nadharia ya Diskosi Hakikifu Changanuzi (DHC). Katika kufanya hivi, tutajaribu kuonyesha namna mamlaka na nguvu za kisiasa na kijamii huongoza maingiliano yanayohusu mataifa yanayozozania kipande fulani cha ardhi.Van Dijk (1998) anafafanua Diskosi Hakikifu Changanuzi kama mtalaa unaoshughulikia uhakiki wa matini ama iliyoandikwa au inayosemwa, kwa lengo la kutambua vianzo vya mamlaka, utosawa, na amri juu ya upendelevu. DHC huchunguza namna hali mbalimbali za mamlaka huhifadhiwa na kuendelezwa katika miktadha mahususi ya kijamii, kisiasa na kihistoria

    \u27Sipangwingwi, Watajua Hawajui\u27: Jaribio la Kuelekeza Matumizi ya Lugha Dhidi ya Uhalisia wa Kiisimujamii

    No full text
    Makala haya yanaangazia nyimbo mbili, ‘Sipangwingwi’ na ‘Watajua hawajui’ ambamo mnapatikana maneno mawili Sipangwingwi na Watajua hawajui. Hivi karibuni, Serikali ya Kenya, kupitia Shirika la NCIC imetoa tamko ambalo linaharamisha matumizi ya haya maneno mawili, miongoni mwa mengine kwa madai kwamba huenda yanaweza kuibua hisia fulani ambazo zinaweza kuchangia hali ya machafuko katika na baina ya Jamii-tumizi lugha mbalimbali. Makala haya basi yanajadili matumizi ya vifungu hivi viwili kwa kurejelea nyimbo hizo mbili ambapo waandishi wamejaribu kuonyesha kwamba ni makosa kuelekeza matumizi ya lugha, kwa kuwalazimisha wanajamii kutotumia maneno fulani ambayo, huenda yanatumiwa kwa wingi na mtu au mwanasiasa fulani. Ukweli wa kiisimujamii ni kwamba, lugha inafaa kujiendeleza, kujikuza na kujisambaza kote, kutegemea watumiaji wake, katika muktadha wowote: sokoni, kanisani, msikitini, mtaani, na kwingineko

    Matumizi ya Usambamba kama Nduni ya Kimtindo katika Kuibua Maudhui ya Dini katika Riwaya ya \u27Paradiso\u27

    No full text
    Makala haya yanachunguza matumizi ya usambamba kama nduni ya kimtindo katika kuibua maudhui ya dini katika riwaya ya Paradiso. Tunachunguza miundo mbalimbali ya kiusambamba iliyotumika katika riwaya hiyo kuibua maudhui ya dini. Suala la dini ni la msingi katika jamii mbalimbali kwa vile dini imeshikamana na maisha ya kawaida ya wanajamii. Ndani ya mada ya jumla ya dini, riwaya hii inaangazia dhamira zinazoathiri jamii kama vile ufisadi na ujilimbikiziaji mali, ufungamano wa siasa na dini, pamoja na masuala ya kijinsia. Tulidondoa vifungu kutoka katika riwaya hiyo kwa mkono kwa sababu haipatikani kielektroniki. Data iliteuliwa kimaksudi kwa kulenga maudhui yanayohusu suala la dini. Katika ukusanyaji na uchambuzi wa data tumetumia Nadharia ya Uchimuzi. Orodha ya kategoria za kiisimu na kimtindo ya Leech na Short (2007) ilitumiwa kubainisha ngazi kuu za uchunguzi wa kimtindo. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba usambamba ni njia kuu aliyoitumia mwandishi kuibulia na kusisitizia maudhui kuhusu dini. Usambamba huu unajitokeza katika ngazi za virai na vishazi na unahusisha aina mbalimbali kama vile anafora, epifora, tanakuzi na mjalizo. Usambamba wa aina ya anafora ndio umedhihirika zaidi katika riwaya ya Paradiso. Makala haya yanapendekeza kwamba usambamba wa kisintaksia unafaa kuhusianishwa na usambamba wa kileksika katika kuzichambua kazi za kifasihi za Kiswahili kimtindo

    Athari za Ulumbilugha Miongoni mwa \u27Chokoraa\u27

    No full text
    Makala haya yanachunguza athari za ulumbilugha katika kutimiza nia za wakati husika za Chokoraa. Chokoraahutumia lugha mbalimbali katika mawasiliano yao. Uteuzi wa lugha itakayotumiwa na Chokoraa hutegemea muktadha maalum. Chokoraa hutumia Kiswahili, Sheng’, Kiingereza na lugha za asili katika mazungumzo yao. Ulumbilugha ndio huwafanya Chokoraa wakati mwingine kuchanganya ndimi kwa kutumia lugha ambazo wanazijua huku wakitaka kutimiza nia mahsusi. Kwa hali hii basi tunaweza kusema kuwa wanaulumbilugha huteua lugha kwa mujibu wa muktadha kutokana na ukweli kuwa lugha moja yaweza kuwa faafu katika muktadha mmoja na wala sio mwingine. Pia, makala haya yanaainisha athari za ulumbilugha kama zinavyojitokeza katika mazungumzo ya Chokoraa wa mtaa duni wa Mathare, jijini Nairobi

    Mwingiliano wa Kisimulizi katika Tenzi za \u27Fumo Liyongo\u27 (UFL), \u27Gilgamesh\u27 (UG), \u27Mikidadi na Mayasa\u27 (UMM) pamoja na \u27Simulizi ya Samsoni\u27 (SS)

    No full text
    Makala haya yanajadili suala la mwingilianomatini katika tendi teule na matini ya kidini. Mabadiliko katika jamii yanayoletwa na teknolojia ya kisasa yamesababisha baadhi ya kazi za kijadi kama vile tenzi, kusahaulika. Tenzi ni hifadhi muhimu ya historia ya jamii, hivyo zinafaa kuhifadhiwa kwa kufanyiwa utafiti zaidi ili ziendelee kuwa na manufaa katika jamii. Kutokana na udurusu wa maandishi uliofanywa na watafiti, ilidhihirika kwamba tenzi za Fumo Liyongo (UFL), Gilgamesh (UG), Mikidadi na Mayasa (UMM) pamoja na Simulizi ya Samsoni (SS) zinawasilisha visa mbalimbali kwa njia ya usimulizi. Matini hizi teule zina mwangwi fulani unaohisika kisimulizi. Makala haya yamezingatia Biblia kama matini muhimu ambayo ina wingi wa kazi za kifasihi zinazohitaji kuhakikiwa, mojawapo ikiwa Simulizi ya Samsoni. Makala haya yamejadili mbinu za kisanii zilizotumika kisimulizi ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa
    corecore