114,196 research outputs found
Week 17a Review: Juma 17a Tathmini
JUMA LA MARUDIO|Kutua Kwa Muda Ili Kupitia Neema Tulilizopokea|Mwongozo: Neema za Kutuingiza Ndani Zaid|Tunatua tena kidogo ili kutoa nafasi kwa neema tulizopokea kupenyeza ndani zaidi mioyoni mwetu. Tunafanya mafungo haya huku tukiendelea kawaida na maisha na shughuli zetu za kila siku. Sasa tumezizoea sana tafakari zetu za kila siku na tayari zimekuwa zikituletea furaha. Tunajitayarisha kusonga mbele kuelekea kweny tafakari ambazo Yesu atatuonyesha kuhusu safari ya maisha yake.|Juma hili halitupeleki katika maeneo mapya, ila linatuingiza ndani zaidi katika eneo tulilopo. Tunalianza juma hili kwa kuzitazama shauku zetu. Naifanya upya shauku yangu, uchu wangu na uchaguzi wangu kuwa na Yesu—kutaka kumjua kwa ukaribu zaidi, kumpenda kwa undani zaidi na kumfuata kwa moyo zaidi. Juma hili si lenye harakati nyingi ndani moyoni au mawazo makali akilini. Hii ni juma la kufanya uthibitisho. Juma zima, kwa kutumia njia zangu mwenyewe, nakusudia kufanya kumbukumbu ya nia yangu kuu itawale akili na moyo wangu wakati wote, au nafanya bidii katika muda ninaopata kusema tena na tena “Ndiyo, hiki ndicho ninachotafuta; Hiki ndicho ninachochagua—Kuwa nawe Yesu wangu.”Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
The Week 2 Guide: Juma 2
JUMA LA PILI|Hadithi ya Maisha Yetu: Kuingia Zaidi Ndani Yake|Mwongozo: Kuangalia kwa Makini Zaidi Hadithi za Maisha Yetu|
Kama tulivyopitia “kitabu cha picha” cha hadithi za maisha yetu wiki iliyopita, zimetujia kumbukumbu ambazo zimetuonyesha uwepo wa Mungu katika safari ya maisha yetu hapa duniani. Zoezi letu juma hili litatusaidia kuingia zaidi ndani ya hadithi za maisha yetu.|Njia mojawapo nzuri ya kupenya ndani zaidi katika hadithi za maisha yetu ni kujiuliza na kujibu maswali yaliyo muhimu. Ni kweli tunaendelea kufanya mafungo haya ya kiroho kwa mtandao kati ya maisha yetu yenye harakati na changamoto nyingi katika juma hili na tutaendelea kuweka taswira fulani katika akili na mioyo yetu iwe “dirisha” kupitia kwalo tunaangalia na kutafakari juma zima, kama vile tulivyofanya katika juma la kwanza (angalia Zana za Kukusaidia Kuanza Juma Hili). Maswali haya muhimu ni rahisi kuyakumbuka na ni muhimu kwa kututayarisha kwa majuma yanayofuata. Kama jinsi Mungu “alivyotuunga pamoja tumboni mwa mama zetu,” kama ituambiavyo Zaburi ya 139, kadhalika matukio mbalimbali na yale tunayotutokea katika maisha yetu huendelea kutufanya kuwa watu tulio leo hii.|Maandiko Matakatifu:|Isaya 49:14-16|Hosea 11:1-4|Zaburi 23Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
Week 11 Guide: Juma 11
JUMA LA KUMI NA MOJA|Mwaliko wa Kupenda — Mwitikio Wetu|Mwongozo: Kufanya Majitoleo ya Nafsi Kikamilifu|Katika Juma hili tuitikie kwa moyo mwaliko wa mapendo tulioupata. Kupitia katika zoezi la juma lililopita, tumeweza kujua kuwa sifa ya mwitikio wetu inategemea kina cha upendo wetu kwa yule atualikaye. Pale mpendwa wetu anapotuuliza kuhusu mwitikio wetu kwa mwaliko wake, jibu ni “Ndiyo”. Hata pale tunapojua kuwa mwitikio huu unaendana na gharama binafsi kubwa sana, bado mwitikio wetu haubadiliki kwa kuwa tunajua upendo daima unatuweka katika ukaribu na umoja wa wapendanao—nasi tunataka daima kuwa na yule tumpendaye.|Kwa mioyo yetu, juma hili tutakuwa tukiitikia mwaliko wa Yesu Kristu. Tunaweza kwa muda mfupi kufanya marudio ya mwongozo wa zoezi la juma lililopita ili kujikumbusha mwito huu na kuamsha hisia za rohoni tulizopata. Tuliguswa sana na mwaliko wa kuungana naye katika mradi wa kuwaleta wengi katika kuwakaribisha wengi katika utawala wa Mungu. Tukiangalia kwa makini, tutaona kuwa mwito huu unatofautiana kidogo kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuwa tuna vipaji, historia na malezi tofauti. Mioyoni, tumezawadiwa neema tofauti baina ya mtu mmoja na mwingine. Hali ya maisha tuliyopitia; namna mbalimbali za kheri na shari, furaha na huzuni, mahangaiko na starehe; vimetujengea kila mmoja namna tofauti na ya kipekee ya kuhurumia na kuwa na wengine katika magumu yanayowasibu. Kila mmoja wetu anapata mwaliko kwa namna yake ya pekee, kulingana na umri na uwezo tuliojaliwa hasa wa ushawishi kwa wengine. Hivi basi tunapenda kusikia mwaliko wa Kristu ukielekezwa kwetu binafsi, kama vile tukialikwa kwa kutajwa majina na yule atupendaye. Hata hivyo, kwetu sote, kuna usawa katika mwaliko na nafasi tunayopewa ya kuuitia. Bila shaka mwitikio wetu ni “Ndiyo”. Hakuna furaha ya kweli maishani ambayo haihusishi kumfuasa Yesu Kristu. Swali la juma hili ni kina au upevu wa mwitikio wetu—jinsi ambavyo tunaweza kuuitikia kikamilifu mwito wa Kristu. Hatujui kwa uhakika bayana “Ndiyo” yetu mwaka huu itakuwa namna ipi na itajumuisha yapi. Kadhalika hatuweze kuwa na habari kamili za “Ndiyo” yetu mwaka ujayo, au miaka kumi kutoka leo.|Maandiko Matakatifu|Isaya 6:1-8|Zaburi 116|Luka 10:1-9; 17-21|Yohana 21:15-19Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
Week 18 Guide: Juma 18
JUMA LA KUMI NA NANE|Namna Tatu za Miitikio|Mwongozo: Motisha|Kabla ya kurudi kwenye maisha ya Yesu, tuchukue wiki moja kuweka msingi wa tafakari zitakazofuata. Tunajua tutavutiwa ndani zaidi katika uhusiano wetu na Yesu na kuwa hii itatuweka huru zaidi katika maamuzi na chaguzi tutakazokuwa tukifanya katika maisha yetu.|Juma hili tukiendelea na shughuli na kazi zetu, tutakuwa ‘tukichambua moyoni’ simulizi ya kitafiti. Tutafanya hali ya kufikirika lakin iliyo katika mfumo wa hali halisi ya maisha, na tutaangalia njia tatu za kuitikia hali halisi inayojitokeza maishani.Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
The Week 8 Guide: Juma 8
JUMA LA NANE|Upendo wa Mungu Kwetu — Huruma Yenye Msamaha| Mwongozo: Vipi Mungu Sharti Afurahie|
Katika juma hili tutazungukia upendo wa Mungu kwetu. Tunataka kuuonja na kufurahia kikamilifu msamaha wa dhambi ambao ni zawadi ya Mungu kwetu.|Japokuwa tumejaribu kufunga kila tafakari ya udhambi wetu kwa uhalisi au ukweli wa huruma ya Mungu, juma hili tutajaribu kutoa nafasi kwa huruma ya Mungu iliyo chanzo cha msamaha wa dhambi iwe ‘kibwagizo’ cha yote katika juma zima.|Tunaanza kwa kumgeuzia macho Mungu. Taswira ya Mama akimpakata binti yake yaweza kutupa motisha kubaki tukitazama uso wa Mungu. Uso wa mama huyu utatusaidia kuanza kutafakari nguvu itokanayo na jinsi Mungu anavyotukumbatia.|Maandiko Matakatifu:|Yohana 4:5–42|Yohana 9:1–4|Yohana 8:3–11|Hosea 14:1–10|Luka 15:11–32Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
The Week 1 Guide: Juma 1
JUMA LA KWANZA|Tuanzie Hapo Mwanzoni: Hadithi ya Maisha Yetu|Mwongozo: Kumbukumbu Zinazotufanya Sisi Kuwa Tulivyo|
Hili ni juma la kwanza la majuma 34 ya safari yetu ya kiroho. Tunaanzia mwanzoni—hadithi ya maisha yetu. Sala huhusu uhusiano wetu na Mungu. Katika juma hili, tutaanza kukua katika uhusiano huu na Mungu katika sehemu zote za maisha yetu kwa kutafakari hadithi ya maisha yetu. Hii inahusisha wazazi, ndugu na marafiki, labda hata na maadui; inahusisha matukio mengi tuliyoshuhudia na pia yaliyotokea lakini hatukuyashuhudia waziwazi kama kuzaliwa kwetu; yahusu hisia mbalimbali za ndani: furaha na huzuni, faraja na simanzi, maliwazo na hasira, vicheko na vilio nk. Inahusu pia watu wengine waliogusa maisha yetu kama waalimu wa dini, shule na vyuo; waongozi na washauri wa kiroho, wahubiri, mapadre, wachungaji na hata wanakwaya au waimbaji.|Maandiko Matakatifu|Luka 12:22-34|Isaya 43: 1-4|Luka 11:1-3|Zaburi 8|Zaburi 139Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
Week 15 Guide: Juma 15
JUMA LA KUMI NA TANO|Kazaliwa Kwetu, Kwa Ajili Yetu|Mwongozo: Neema ya Kuzaliwa Kwake|Akinamama wengi, katika kusherehekea siku ya kuzaliwa ya watoto wao, huwasimulia kwa kwa uyakinifu yaliyotokea siku na wakati walipozaliwa. Mwaka hadi mwaka, simulizi hizi hurudiwa. Katika muda huu wa mafungo yako, tunampa Yesu nafasi atupe simulizi ya kuzaliwa kwake. Hii itatubidi twende mbele zaidi ya simulizi tunazopata katika Injili kama zilivyoandikwa na Matayo na Luka. Tutaingia ndani kabisa ya simulizi kuliko tafakari zetu za kuzaliwa kwa Yesu Kristu. Juma hili tutapokea neema ya kushuhudia kuzaliwa kwa Yesu na kuelewa maana yake hasa na umuhimu wake kwetu.|Uchu wetu unaendelea. Ni lazima kwetu kuiamsha upya kiu hii ndani yetu katika juma hili, (iwapo imefifia)—kiu au uchu wa kumjua Yesu kwa undani zaidi. Kwa kumwangalia na kumwelewa, tunategemea upendo wetu kwake kuwa mkamilifu zaidi. Upendo wetu kwake unavyoongezeka katika ukamilifu, tunapata uhiari mkubwa zaidi wa kuwa naye katika utume wake.|Maandiko Matakatifu:|Matayo 1:18-24|Luka 2:1-21|Matayo 2:1-12|Matayo 2:13-23|Zaburi 98Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
The Week 3 Guide: Juma 3
JUMA LA TATU|Mtazamo—Picha Thabiti|Mwongozo: Ulimwengu Kama Unavyopaswa Kuwa|Baada ya majuma mawili ya kupitia na kutafakari hadithi ya maisha yetu na kuiona kama hadithi ya uwepo wa Mungu asiyetutelekeza kamwe, sasa tunasonga mbele kuwa na mtazamo mpana zaidi.|Katika juma hili tunanataka kutafakari juu ya ufunuo wa nia ya Mungu kutuumba sisi na viumbe vingine vyote.|Mtakatifu Inyasi wa Loyola kautafsiri ufunuo wa nia ya Mungu kwa maneno machache:|Mungu katuumba kumsifu, kumtukuza na kumtumikia yeye|na katika kutakeleza hayo, sisi kupata wokovu wa roho zetu.|Mungu kaumba viumbe vingine vyote|kututusaidia kutekeleza nia hiyo ya kuumbwa kwetu naye Mungu|Katika juma hili tuweke moyoni na kutilia maanani tafakari mbili nzuri:|Ninapokuwa nikifanya kazi zangu za kawaida na kuendelea na shunguli zingine za kila siku, nijitahidi kuwa daima kutanabahi au kuwa na utambuzi wa nia ya Mungu kuniumba mimi:|Kumsifu Mungu.|Kumsimtukuza Mungu: kukua katika kumhimidi na kumpenda Mungu|Kutumikia: kuwa katika utumishi wa Mungu.|Kuwa makini zaidi katika kutambua uwepo wa viumbe vingine na nia ya Mungu ya kuviumba vyote hivyo kunisaidia mimi — vyote vimeumbwa kwa ajili yangu.|Maandiko Matakatiu|Waefeso 1:3–12|Zaburi 138Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
The Week 7 Guide: Juma 7
JUMA LA SABA|Vurugu la Dhambi — Mwelekeo Binafsi|Mwongozo: Kuweka Wazi na Kutegua Fumbo la Dhambi Zetu|Juma lililopita tulipitia uwepo wa dhambi na udhambi wetu katika mtazamo wa upendo mkuu wa Mungu. Juma hili tunajipa muda wa kuchungua mwelekeo au mfumo wa udhambi wetu ili kwamba tuweze kutambua kwa undani zaidi upendo wa Mungu na hamu kubwa aliyonayo Mungu ya kuhusiana nasi kwa karibu zaidi.|Sote tunajua ukweli kwamba kitambaa hufanywa kwa nyuzi nyingi zilizowekwa kwa mpangilio fulani ambao hukifanya kiwe kilivyo; na pengine nyuzi hizi huwa za rangi mbalimbali na hufumwa katika mpango maalum wa kukipa kitambaa sura aitakayo mfumaji.|Nasi hapa tunajaribu kuzichungua nyuzi za dhambi, ili kutambua jinsi dhambi zinavyozalika na mfumo au mwelekeo wake. Kwa kufanya hivi tunategemea kutambua jinsi dhambi itokeavyo kati yetu. Ni kipi hasa kinacholeta mvuto wa kutenda dhambi na ni mivutano ipi ipo moyoni mwangu? Naweza kuanuisha motisha unaojenga ndani yangu silika ya kupingana na matakwa ya Mungu? Naweza kutaja misingi ya ukosefu wa uhuru wangu? Najua chimbuko la hofu yangu?|Maandiko Matakatifu:|Matayo 8:1–13|Luka 9:23–25|2 Wakorinto 12:8–10|Luka 5:1–11|Luka 5:17–26|Matayo 25:31–46Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
The Week 4 Guide: Juma 4
JUMA LA NNE|Picha Thabiti—Kuwa Katika Urari wa Maisha|Mwongozo: Mifano ya Uhuru wa Kiroho|Juma hili tunasonga mbele kutoka katika utoaji shukrani na sifa kwa Mungu; kutoka katika mtazamo wa picha kubwa ya mpangilio wa viumbe vya Mungu — kwenda kuiishi picha hiyo thabiti ya uumbaji wa Mungu. Kuiishi picha hiyo kubwa ipasavyo ni kukubali nafasi yetu katika uumbaji wa Mungu — ni kuwa katika urari wa maisha.|Katika juma lote hili, tuna shauku ya kuvutiwa na watu ambao wanaonekana kuwa katika hali ya kuikubali sababu ya kuumbwa kweo na hivyo basi kuvitumia viumbe vingine vyote katika hali huria inayotokana na kuikubali nafasi yao baina ya viumbe vya Mungu.|Mt. Inyasi wa Loyola anaweka hili katika maneno rahisi:|Sharti tutumie zawadi ya viumbe vya Mungu pale ambapo vinatuwezesha kuitekeleza nia ya kuumbwa kwetu, na sharti tuviweke pembeni vile ambavyo havitusaidii kuitekeleza nia hiyo au vinakuwa kikwazo katika kuiishi sababu ya kuumbwa kwetu.|Maandiko Matakatifu|Waefeso 2|Warumi 8|Matayo 10:29-31Actual date of publication unknown. The date in dc.date.issued is arbitrary and used because a date is required for indexin
- …
